Sifa za madiwani wetu zinatosheleza kuwapa mamraka makubwa ya kuwafukuza watumishi wa Halmashauri zetu? kumfukuza mtu kazi kuna hitaji kutafakari kwa kina na kufanya uchuguzi wa kutosha kabla ya kufikia hatua hii kali sana ya kumfukuza mtu kazi. Tukumbuke kuwa mtu anapofukuzwa kazi haathiriki yeye pekee yake, taifa linapata hasara kwa kuingia ghalama za kufanya mchakato wa kuajiri mbadala, familia ya mtumishi pia. Ni lazima kutafakari kwa kina kabla ya kufikia uamuzi huo. Ni lazima kuangalia sifa za watu hawa (madiwani) kama wanao uwezo wa kutafakari kiasi cha kutosha.
Ili kuwatendea haki watumishi hawa ni lazima kujiridhisha vya kutosha juu ya tuhuma wanazotuhumiwa watumishi wetu. Mtindo wa madiwani kuchukua uamuzi wa kumpigia kura tu mtumishi huyu afukuzwe kazi, afukuzwe kazi na kushitakiwa au asimamishwe kazi ni lazima watu wanaofanya maamuzi haya wawe watu wenye busara na hekima za kutosha. Hebu tujaribu kuona uwezo wa baadhi ya madiwani wetu. Wapo madiwani wanaochaguliwa kutokana na uwezo wa kifedha tu wakiwa na elimu ya chini mno kiasi kwamba uwezo wao wa kupambanua mambo hasa katika kipindi hiki cha mabadiliko makubwa ya kila nyaja ukiwa mdogo sana.
Mfano, wapo madiwani wanaowachukia watumishia kwa sababu ya wivu tu wa kimaendeleo ya mtumishi husika, kama vile kakopa fedha benki kajenga nyumba au kanunua gari nk. Wivu unaotokana na madiwani kuwa na posho ndogo ukilinganisha na watumishi wanaowasimamia. Wapo madiwani wanadai serikali iliyopo madarakani inachukiwa kwa sababu ya watumishi hawa kwa hiyo tuhuma hata bila kuthibitika wanakimbilia kuwafukuza kazi kama njia ya kuleta mvuto kwenye chama chao. Wapo watumishi wanaofukuzwa kwenye Halmashauri kwa tofauti za kisiasa tu. Ni lazima kutafakari kwa kina sifa za madiwani hawa na mamlaka walizo nazo la sivyo watumishi wengi watakimbia kufanya kazi katika Halmashari. Kwani kwa sasa afadhari uajiliwe na serikali kuu kuliko Halmashauri.