Tujadili Tanganyika | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tujadili Tanganyika

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Jagermaster, Feb 13, 2011.

 1. Jagermaster

  Jagermaster JF-Expert Member

  #1
  Feb 13, 2011
  Joined: Nov 6, 2010
  Messages: 656
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  This opinion is exclusive for Tanganyika's..

  Eti wana jukwaa la siasa katika muungano huu wa serikali mbili upande wetu huu wa Tanganyika kupitia ofisi yetu ya Waziri mkuu Tawala za mikoa na Serikari za mitaa tukiamua kuipa hadhi mikoa yote ya Tanganyika kuwa na serikali zao na wakuu wa mikoa hiyo wachaguliwe na wananchi wa mikoa hiyo kupitia vyama au namna nyingine, na baada ya Mabadiliko hayo hao wakuu wa mikoa waitwe Marais si tutakuwa tumeweza kuipa hadhi mikoa ya Tanganyika sawa na Zanzibar ambayo nayo ina rais wake kwa sasa???!!!....na tutakuwa tumesawazisha bao, kwa maana sasa mabadiliko ya kumi ya katiba ya Zanzibar yanaleta utata, serikali ya Zanzibar inaonekana kuwa na hadhi sawa na serikali ya muungano. Serikali kuu ibaki na mambo yake ya ulinzi na usalama, foreign affairs, fedha na ugawaji wa mikoa uwe unaridhiwa na bunge la jamhuri ya muungano, then ndio tujadili katiba mpya. Maana katiba ambayo tunatarajia kuindika ni ya Muungano na wala haitagusa katiba ya Zanzibar ambao tayari wao wameweka sawa mambo yao sisi Tanganyika tunatapatapa tu. Wabunge wa bara mlio bungeni hili jukumu lenu, tunataka plat form ya kuongea mambo yetu ya Tanganyika, maana sasa tunaingia kwenye mjadala wa Katiba ya muungano ambapo mjadala pia utahusisha Wazanzibar, ambao wenyewe wanakatiba yao na mambo yao wameweka sawa.Ingawa Tanganyika hatuna jukwaa mimi naona kwa kuanzia ofisi ya Waziri mkuu Tawala za Mikoa na Serikari za mitaa mna kazi ya kufanya kwa hili na hili halihitaji UCHADEMA wa UCCM, kama unapenda Tanganyika yako linakugusa

  Nawakilisha!.
   
 2. a

  abdulahsaf JF-Expert Member

  #2
  Feb 13, 2011
  Joined: Aug 31, 2010
  Messages: 859
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Mh Member
  Inaonekana kishwa usaha na hufahamu maana ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar?. Huwezi kushukuwa Zanzibar na kuilinganisha na mkoa wowote wa Tanganyika hata kama Zanzibar ina population ndogo ya watu wake lakini ni nchi ilioungana na Tanganyika na ukapatikana Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.
  Kipengele cha mabadiliko ya katiba ya Zanzibar ya 1984 sio kigeni kwa Zanzibar ni kujiuliza kabla ya Muungano Zanzibar ilikuwa Nchi au mkoa?a.).

  b.) kama kimewakera Watanganyika kipengele hisho basi ni malipo ya Wzanzibar kuwalipizia pale mulipo itisha Bunge lenu la Tanganyika bila kumshirikisha Mzanzibar yoyote na kujifanya muna akili nyingi? mulipo vunja Katiba yenu na nchi yenu ya Tanganyika na kuvaa Koti la Tanzania, kwa hio sisi kuanzia pale tuliwashtukizia kuwa Mumevunja makubaliano ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar na Muungano kuwa Fake na badli. kwa hio muna haki ya kuvunja Muungano na kurudisha Tanganyika yenu na katiba yenu sisi hatuna hamu na Tanganyika yenu na hata kuku wa Zanzibar wanataka leo Muungano uvunjike.
   
 3. L

  LAT JF-Expert Member

  #3
  Feb 13, 2011
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 4,524
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 0
  wewe ni muhogomchungu au...? duh
   
 4. L

  LAT JF-Expert Member

  #4
  Feb 13, 2011
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 4,524
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 0
  wewe na abdulashaf wote ni wamoja.... msituzuge.. anzisheni sarafu na noti ya serikali ya mapinduzi zanzibar halafu tuwaachie kata yenu...
   
 5. D

  Dopas JF-Expert Member

  #5
  Feb 13, 2011
  Joined: Aug 14, 2010
  Messages: 1,150
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  Hivi wewe abdulahsaf una tatizo gani? Kwa kiswahili kibovu namna hiyo[ tazama red] wewe sio mzanzibari wala mzanzibara, wala Mtanganyika. Kwanini unaingilia yasiyokuhusu?

  Mambo ya Tangayika na Zanzibar tuachie sisi wananchi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

  Kama unawashwa, ulete hoja inayohusu nchi yako tujadili, au walau inayohusu Afrika Mashariki, maana naona unatoka mojawapo ya nchi za Afrika Mashiriki. Hakuna hoja za kujadili kwenu kwa maslahi ya nchi yako. CRAP!!!!!!!!!!!

  Lakini kama kweli wewe ni mzanzibari, basi usiridhike kukaririshwa Qur'an, nenda darasani walau upate elimu ya msingi itakusaidia hata kutoa hoja zako. Maana naona hata darasa moja hujaona, walau hata kiswahili kidogo cha kuandikia ungefahamu. Pole
   
 6. Babu Lao

  Babu Lao JF-Expert Member

  #6
  Feb 13, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 2,056
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  :coffee::coffee::coffee::coffee::coffee:
   
 7. m

  mzambia JF-Expert Member

  #7
  Feb 13, 2011
  Joined: Dec 31, 2010
  Messages: 882
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 35
  Tuachaneni na hoja ya tanganyika tujadili mambo ya dowans na katiba.
   
 8. c

  chelenje JF-Expert Member

  #8
  Feb 13, 2011
  Joined: Oct 18, 2010
  Messages: 556
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  wapi madela wa madilu???
   
 9. Jagermaster

  Jagermaster JF-Expert Member

  #9
  Feb 14, 2011
  Joined: Nov 6, 2010
  Messages: 656
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0

  Nashukuru mheshimiwa kwa majibu yako, kinachoonekana hapa majibu yako hayana mantiki yoyote, kama unaijua Zanzibar kwa Historia lini ilishakuwa sovereign state?. Historia ya Zanzibar tokea Sultan Sayyid Said alivyohamisha makao yake makuu kutoka Muscat kwenda Zanzibar, Zanzibar was just a part of Muscat. Kipindi chote toka Utawala Muscat, Mwingereza, Sultan tena mpaka mapinduzi, Zanzibar never been a soveign state. Ni jambo liliwazi kuwa toka mapinduzi ya January 1964, mpaka April 26 1964 wakati wa Muungano Zanzubar was in a precarious condition mlishindwa kusimama kama sovereign State na kimbilio lenu lilikuwa ni kuungano na mbabe mmoja ili kulinda usalama wa Zanzibar.Kama muungwana utambue kuwa mnajiona mnaweza kusimama kwa kuwa mko ndani ya muungano nje ya muungano Zanzibar ni kama Kifaranga mtanyakuliwa kama na vipanga tu. Angalia Comoro ilikuwa na visiwa vingapi wakati wa uhuru na vingapi vinabaki sasa.

  1800'S-1884 (Zanzibar mkoa wa mmojawapo wa Oman, Under Sultan of Oman)
  1984-1963 (Zanzibar mkoa mmoja wapo wa Oman, under British protectorate).
  1963-Jan 12 1964 (Zanzibar again Under sultan rule)
  1964 (One of super powers during cold war grants Zanzibar to Tanganyika otherwise it could to seized by other super power. There after Zanzibar under Tanganyika rule).

  Mabadiliko ya katiba ya Zanzibar hayawatishi Watanganyia hata kidogo, what we need is our plaform to discuss our own matters as Tanganyikas.Mabadiliko ya utawala wa Tanganyika kama yakifanyika kidogo tu kama maada ivyopendekeza, Zanzibar utakuwa mkoa kama mikoa ya Tanganyika tu na hapo ndio utajua Zanzibar si nchi, na wala haijawahi kuwa nchi (kwa maana ya sovereign state) kama (above) historia inavyoonyesha, na haiwezi kuwa nchi mkitoka ndani ya muungano mutanyakuliwa na mabwana wengine, kama visiwa vya Comoro vinavyonyakuliwa au Puetro Rico ilivyojisubmit kwa Marekani.
   
 10. Jagermaster

  Jagermaster JF-Expert Member

  #10
  Feb 14, 2011
  Joined: Nov 6, 2010
  Messages: 656
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0


  Dowans tujadili tuuuuu!!! watu wanasema twende mtaani watu hamtaki, tunabaki kujadili hapa JF tu. Watu wanalipana fedha za jasho letu tunajadili JF tu. Watu hawapendi kujitoa mhanga unadhani tutazuia dowans wasilipwe kwa pupiga polojo hapa JF???. Ishu ya muungano ni baadhi ya mapungufu yaliyondani ya katiba. Sasa wewe sijui unataka kujadili katiba ya Taifa lipi?. Kama wewe si Mtanganyika hii thread haikuhusu, nadhani mwandishi kaeleza hilo.
   
 11. Jagermaster

  Jagermaster JF-Expert Member

  #11
  Feb 14, 2011
  Joined: Nov 6, 2010
  Messages: 656
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Thanks for some spelling correction, ila mimi si Mzanzibar bro, mimi Mtanganyika haswaa, tena umenishushia hadhi kwa kunipa uraia wa hiyo kata yao.
   
 12. Ndjabu Da Dude

  Ndjabu Da Dude JF-Expert Member

  #12
  Feb 14, 2011
  Joined: Aug 29, 2008
  Messages: 3,405
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160
  Mambo ya Vita vya Baridi yaliyo weka vigezo vikuu vilivyosababaisha muungano kati ya Tanganyika na Unguja yaliisha zamani tokea USSR ilivyosambaratika mwisho wa miaka ya 80, na kuashiria mwanzo wa wimbi la demokrasia ya vyama vingi miaka ya 90.

  La ajabu ni kwamba kwa vile bado katiba iliyoanzishwa na CCM since the 80s bado inatawala nchi ya Tanganyika hadi leo hii, ndiyo maana unaona chama kama CHADEMA kimeshindwa kwenye Uchaguzi wa Rais na Wabunge ukilinganisha na CUF ambayo imechukuwa nafasi ya pili kwenye Uchaguzi mkuu uliopita. Kwa mtazamo wangu, sababu moja wapo kuu iliyoleta matokeo haya ni unfair advantage iliyonayo CCM kutokana na huu muungano wa kulazimisha usioridhiwa na Wananchi wa pande zote mbili
   
 13. YeshuaHaMelech

  YeshuaHaMelech JF-Expert Member

  #13
  Feb 14, 2011
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 2,624
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Dissolve SMZ ile mikoa mitano iwe totally integrated ktk JMT. Else sioni kama huu ni muungano!
  May be we find another name
   
 14. mgen

  mgen JF Bronze Member

  #14
  Feb 14, 2011
  Joined: Nov 18, 2010
  Messages: 13,905
  Likes Received: 1,345
  Trophy Points: 280
  Huna uchungu na Tanganyika kwani wewe ni mtutsi toka rwanda au ni mmetu toka msumbiji?
  Tulipo jikwaa ni kuigeuza Tanganyika kuwa haina mwenyewe na kugeuzwa shamba la bibi.
  Sasa wenyewe tumeamua kujadili tulipo jikwaa sio tulipo anguka.
  Tutangoa kisiki ili tusijikwae tena
  Habari ndio hiyo.
   
 15. Mallaba

  Mallaba JF-Expert Member

  #15
  Feb 14, 2011
  Joined: Jan 30, 2008
  Messages: 2,561
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 133
  utajadirije hiyo katiba bila kutaja Tanganyika?
  Huo muungano utakuwaje bila kujua mstakabari wa Tanganyika?
   
 16. Jagermaster

  Jagermaster JF-Expert Member

  #16
  Feb 14, 2011
  Joined: Nov 6, 2010
  Messages: 656
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Kiongozi ni wabishi hao, wala hawawezi kukubali, bora kufuata kilichopendekezwa
   
 17. popiexo

  popiexo JF-Expert Member

  #17
  Feb 14, 2011
  Joined: Oct 26, 2010
  Messages: 743
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Hoja hii ina umuhimu wake, mie naona tupige kura ya Maoni kumaliza ubishi, kwasababu uzalendo wa wazanzibari kuitumikia na JMT ni mdogo sana zaidi wanaangalia Zanzibar yao. Hata walioko kwenye Bunge hawana mchango wowote wapowapo tu kwao ni sehemu ya ajira na sio sehemu ya kusimamia maendeleo ya nchi hii, wenyewe wanasubiri tu mtu aseme zanzibar sio inchi ndio wamshupalie vinginevyo hakuna kitu. SAA YA UKOMBOZI NI SASA, tuiridishe TANGANYIKA YETU.
  Zamani kipindi kile muungano huu labda ulikuwa na maana lakini sio sasa, kwa sasa hauna maana yoyote.
   
 18. mgen

  mgen JF Bronze Member

  #18
  Feb 14, 2011
  Joined: Nov 18, 2010
  Messages: 13,905
  Likes Received: 1,345
  Trophy Points: 280
  Sema Inshaalah.!
   
 19. Edward Teller

  Edward Teller JF-Expert Member

  #19
  Feb 14, 2011
  Joined: Oct 31, 2010
  Messages: 3,817
  Likes Received: 77
  Trophy Points: 145
  hata viongoz wa ccm wengi wanakimbia mijadala ya muungano-ndo mana kila siku matatzo yanazid kuwa mengi-tukijadili katiba ni lazima tujadili na muungano pia-
  kumbuka kukimbia tatizo si kusolve tatizo-ni bora tulijadili tu
   
Loading...