Sultan Suleiman Khan anaingiaaaaaaaa,
Pisha njiaaaaaaaa...!!!
Ukisikia hivyo basi inabidi msimame na muinamishe vichwa chini. Na kama mlikua mnapiga story basi mkae kimya maana mkulu anapita hapo mida hiyo.
Huyu ni aliekua ntawala wa Ottoman Empire, Himaya iliyotawala Mabara Matatu, wenyewe walimuita Mtawala wa Dunia. Himaya hii chimbuko au makao makuu yake ni Uturuki.
Ilikua ni himaya nyingine kuchagua either kua chini ya himaya hii au kuchapana mkono (vita). Na kwa vile himaya/dola/utawala huu ulikua na nguvu basi wengine walikubali bila vita, na waliokaidi walichapwa.
Sultan alikua ni Mtawala Strong, anaeogopwa na mataifa/himaya zingine. Na hata ndani kwake pia watu walimuheshimu na kumuogopa pia, ila udhaifu wake tu ni pale alipoingia kwenye penzi la Suriya Mtumwa wa Kirusi aitwae Alexander (Baadae alikuja kubadili dini na kuitwa Hurem- Mburudishaji).
Sultan alikua akimuona huyu mdada hapindui kabisa, kufikia kuachana na Mwanamke aliezaa nae awali (Mahdevran) na kumuoa huyu. Huyu Mahdevran pamoja na kuachwa still aliendelea kuishi kwrnye Kasri.
Mama yake Sultan (Afsa Hattum) au Validen kwa cheo aliupinga kwa nguvu zote uhusiano huu lakin Sultan hakusikia la yoyote. Ikawa ni mashindano kati ya Alexander (Hurrem) vs Validen & Mahdevran kwa pamoja. Ila sababu Hurrem ana backup ya Sultan mpenzi wake, aliweza kuruka vihunzi.
Hurrem alikua na wafuasi wake miongoni mwa vijakazi, walinzi, mamesenja, etc. Vivyo hivyo kwa Valide& Mahdevran, so haikua bifu au vita ya kitoto between them.
kifupi ni hivyo.