Tujadili njia za asili za kufukuza au kuzuia nyoka shambani au nyumbani kwako

Kuna mzee mmoja yupo Lindi, aliwahi kuniuzia dawa flani ipo katika chupa ndogo sana kama nusu ya robo lita hivi. Ile dawa unachanganya na maji then unamwaga kuzunguka shamba/nyumba/kiwanja etc. Hapo nyoka hawasogei. Nlijaribu shambani kwangu Pawaga Iringa tangu hapo sijawahi kuona nyoka. Nkaagiza tena nikaweka shambani kwangu vianzi (vikindu) pia sijaona nyoka na ninalala chini ya miti saaaafi.
 
Mkuu kama ni dawa za asili fuatilia basi utupe mchanganyiko (ingredients) wake
 
Ninasikia oil chafu hufukuza nyoka na pia ukichoma matairi ya magari moshi wake unafukuza nyoka.Jingine...paka asali kwenye karatasi halafu uichome hiyo karatasi,nyoka woote watakimbilia kusiko julikana.
Ngoja nijaribu hiyo ya kupaka asali kwenye karatasi na niichome maana miezi 6 iliyopita tulikuta nyoka ndani mpaka leo hata nikiona jani nastuka.
 
Wakuu habari,

Naomba tupeane uzoefu wa njia za asili za kuzuia nyoka wasiingie shambani kwako au nyumbani kwako, nafahamu kuna baadhi ya wanyama wanakula nyoka lakini hawawezi kuzuia nyoka kuingia shambani au nyumbani, nafahamu pia kuna dawa za kitaalamu ambazo ukinyunyiza nyumbani au shambani kwako zinapunguza kwa kiasi kikubwa nyoka kwenye shamba lako lakini dawa hizo zina madhara na ni gharama kubwa sana, ninaposema njia za asili ninamaanisha kupanda mimea fulani, kwa mfano ukipanda pilipili kuzunguuka shamba tembo hawasogei kwenye shamba lako, asanteni

Labda nitoe mfano mwingine, ukitaka kuzuia kanga au kwale shambani mwako, chukua gongo kali au konyagi changanya na pumba weka kwenye shambani mwako halafu subiri, wakila tu yaani unawakamata kama kumbikumbi na kuwaweka kwenye magunia na kwenda kuwabanika kwa ajili ya kitoweo na kugawa kwa ndugu, jamaa na marafiki

NB; wakuu hii sio mada tafadhali tujadili mada hiyo hapo juu😂😂
Kwanza anza kulipa kodi.

Kuhusu nyoka ni simple sana. Nunua chumvi ya mawe kisha mwaga ktk maeneo wanayokatiza sana ama zungushia mipaka ya shamba. Nyoka akiguswa na chumvi ndo safari inaanzia hapo.. Fanya majaribio kwanza kwa nyoka waliopo maeneo yenu mwagia chumvi uone shughuli yake..

Huu ujanja nimepewa na wazee wa Lindi
 
Mkuu hiyo ni gharama sana inaingia kwenye kundi la dawa zenye gharama
 
Mkuu wewe ulithibitisha?
Ukweli miaka hiyo sikuwa naishi maeneo rafiki wa nyoka. Ila babu yangu ndiye aliyekuwa mbali na mji. Hata hivyo nnilikuuwa nakwenda kumtembelea tu na kurudi siku hiyo hiyo.

Hata hivvyo kwasasa nipo nje ya jiji. Mara chache nimeona nyoka bustanini. Hivyo ningali ni mwenye kuitafuta mimea hii au mmea mbadala niweze. Kuiotesha
 
Mkuu siku ukienda huko kijijini jaribu kuulizia lazima kutakuwa na watu wanaofahamu
 
Kuna aina fulani ya ukoka wa majani mapana ambao ukiupanda mipakani nyoka anaogopa kupita kwani utamchana
Enheee hapo sasa mkuu umepatia kabisa, naomba ukikumbuka jina lake na inapopatikana utufahamishe kwenye uzi huu kwa maslahi ya wengi
 
Back
Top Bottom