Tujadili: Nani wa kushika bango la vita dhidi ya ufisadi? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tujadili: Nani wa kushika bango la vita dhidi ya ufisadi?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Zak Malang, Apr 24, 2009.

 1. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #1
  Apr 24, 2009
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Tujadili: Nani wa kushika bango la vita dhidi ya ufisadi?

  Baada ya Reginald Mengi kujitolea kushika bango la vita dhidi ya mafisadi, kuna shutuma kali zimetolewa dhidi yake kwamba ama naye pia ni fisadi, ingawa wanaosema hivyo hawataji ufisadi wake ni upi, ama ni msanii tu na anajipendekeza kwa Kikwete eti tu kwa sababu hajamtaja Kikwete katika ufisadi.

  Hawa wanashangaa kwa nini hakumtaja Kikwete kwani yeye ndiyo anawaelea mafisadi kwani ufisadi wao dhidi ya wananchi ndiyo ulimweka madarakani.

  Sasa wana JF tujadili ni nani katika wazalendo washike bango la vita hiyo kwa niaba ya wananchi masikini? Wamejitokeza watu wengine pamoja na wanasiasa lakini wote wameishia kushutumiwa hiki au kile, pamoja na wao kuwa mafisadi pia, wanafiki nk nk nk.

  Hawa ni pamoja na Dk Slaa, Samuel Sitta, Harrison Mwakyembe, Anne Kilango, Ole Sendeka, Alloyce Kimaro, Lucas Selelii, Mark Mwandosya na wengineo wengi tu. Wote hawa nao wameshutumiwa kwa mambo mbali mbali pamoja na ufisadi.

  Watanzania wenzangu, tumefikia njia panda kuhusu vita hii kwani serikali yenyewe ambayo ndiyo ina vyombo vya kisheria kushughulikia suala la ufisadi, nayo iko lawamani kwa kuwaogopa mafisadi, au kwa maafisa wao kununuliwa na mafisadi. Kesi zinazotinga mahakamani ni kiini macho kwani kuna wengine bado hawajakamatwa.

  Nawasihi mtoe mawazo yenu.
   
 2. N

  Nyauba JF-Expert Member

  #2
  Apr 24, 2009
  Joined: Jul 10, 2008
  Messages: 1,098
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  kwanza kabisa DR SLAA yupo kundi la pekee yake..ni mpambanaji mahiri na mwenye nia ya kweli..

  hawa wengine bado nina wasi wasi nao sana kwani ni wapenda sifa tuu kwa wananchi waonekane wamooo.

  wengi wao wamo kwenye mfumo kandamizi kimaamuzi na kuchochea umaskini wa kupindukia.

  mfano wabunge hao wa CCM ni wapambe wa wizi mkubwa wa fedha za umma katika halmashauri zao kwa kulea kutokuwajibika kwa watumishi na madiwani wapenda dezooo na kudumaza maendeleo..

  hawana jipya karibuni wameanza kupata michango ya kufungua SACCOs kwenye majimbo yao kutoka (kwa mengi) ili hali vyama hivyo vyaweza anzishwa na wananchama kwa michango yao wenyewe..

  sita tunaye kwa miaka 40 sasa kama kiongozi mwandamizi asiye na jipya wakuvizia nafasi za uongozi tuu ndani ya ccm na serikali yakee...

  SINA IMANI NAO WOTE ZAIDI YA DK SLAA..
   
 3. Shishye

  Shishye JF-Expert Member

  #3
  Apr 24, 2009
  Joined: Feb 26, 2009
  Messages: 269
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ni rais wa nchi na serikali yake. Huyu asipofanya kazi yake sisi wengine tutaonekana wapiga kelele na watafuta sifa tu. Namshukuru sana Mengi kwa kulianzisha, lakini mafisadi wanakula sahani moja na mkuu wa nchi kwa hiyo sioni matokeo yoyote ya mpambano huu. Wapinzani wabunge ndio hivyo wameshanyamazishwa kwa tishio la nyaraka za wizi wa siri za serikali, hivyo nguvu yao ya kushika bango imepunguzwa makali. Suluhisho ni mtu safi kuchukua nchi tu.
   
 4. The Farmer

  The Farmer JF-Expert Member

  #4
  Apr 24, 2009
  Joined: Jan 7, 2009
  Messages: 1,585
  Likes Received: 437
  Trophy Points: 180
  Raisi peke yake hataweza kupambana na MAFISADI, sisi wananchi tunatakiwa kushirikiana nae katika swala hili. Mengi ameshafungua njia kilichobaki ni sisi wengine kumunga mkono.
   
 5. K

  Kyachakiche JF-Expert Member

  #5
  Apr 24, 2009
  Joined: Feb 16, 2009
  Messages: 911
  Likes Received: 62
  Trophy Points: 45
  Mkuu Mkulima, kwa vipi sasa tushirikiane naye? Hiyo ndiyo mada. Je ni kwa kutoa ushaidi pale utakapohitajika, ama ni kwenda kufungua kesi mahakamani, au ni kwa kujadili tu kwenye majukwaa na kwenye meza ndefu, au ni kwa kuwanyima kura, ama ni kwa kuchukua sheria mikononi? Rais ni taasisi ambayo ina uwezo wa kuyakabili yote haya. Swala ni je ari, kasi na nguvu ya kuyatenda huyo unaye taka tumuunge mkono ameshaanza? Angalia jirani zetu Malawi na Zambia ndipo utagundua tuko miaka mingi nyuma kuweza kuthubutu.
   
 6. Shishye

  Shishye JF-Expert Member

  #6
  Apr 24, 2009
  Joined: Feb 26, 2009
  Messages: 269
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0

  Mada inazungumzia 'kushika bango'. Mimi nimeelewa nani wa kuwa pale mstari wa mbele! Ndio maaana nikasema ni raisi na serkali yake. Wakishatangulia hao sisi wanachi wazalendo tutafuata automatically. Lakini Mengi akiachiwa bango, na wachache wenye ujasiri kama yeye, kama serikali isipotoa ushirikiano usitegemee kuvuna chochote hapo.
   
 7. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #7
  Apr 24, 2009
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,798
  Likes Received: 83,172
  Trophy Points: 280
  Ufisadi unatuathiri Watanzania wote kwa nchi yetu kubaki nyuma kimaendeleo pamoja na kuwa na rasilimali chungu nzima, na kupata mikopo na misaada toka nchi na mashirika mbali mbali duniani. Hivyo Watanzania wote wenye mapenzi ya kweli na nchi yetu inabidi tulibebe bango hilo bega kwa bega na akina Slaa na Mengi, vinginevyo ufisadi utaendelea kukithiri kila kukicha.
   
 8. Msanii

  Msanii JF-Expert Member

  #8
  Apr 24, 2009
  Joined: Jul 4, 2007
  Messages: 6,427
  Likes Received: 370
  Trophy Points: 180
  Kila mwenye nia njema na nchi hii lazima ashike bango dhidi ya mafisadi.
   
 9. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #9
  Apr 24, 2009
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  "Kila mwenye nia njema na nchi hii lazima ashike bango dhidi ya mafisadi."

  *******************************

  Msanii: Tatizo ni kwamba yeyote yule atakayejitokeza kushika bango, hata kama ana nia njema, ataandamwa na kutafutiwa tuhuma mbali mbali pamoja na za ufisadi. Tanzania ndiko ilifikia ktk suala la ufisadi -- hatuendi popopte! Inasikitisja!
   
 10. Msanii

  Msanii JF-Expert Member

  #10
  Apr 24, 2009
  Joined: Jul 4, 2007
  Messages: 6,427
  Likes Received: 370
  Trophy Points: 180
  Mkuu ZAK
  naamini endapo usalama wa taifa au vyombo vya dola wakiamua kulivalia njuga ishu ya ufisadi sidhani kama kutakuwa na mtu atakayewanyooshea vidole maana bado wananchi tuna imani (ingawa chache) nao.
   
Loading...