kwa vipi atabadilika na njia na penye mwanga tunamwonyesha......katika eneo letu hatuna maji ya kunywa toka dunia hii iumbwe,hatuna barabara.....na mwona kama adui na hii ni vita...nadhani ccm wamsaidie sina fedha ya kumsaidia miccmBaba ana haki ya kuchagua ni mgombea gani anampenda na ni chama gani akiunge mkono hiyo ndiyo demokrasia na hii ni kwa mwanafamilia yeyote hata mke wako anao uhuru wa kuwa na mtazamo unaokinzana na wewe. Hiyo ni siasa na inapaswa kutenganishwa na maswala mengine ya kimaisha. Hebu fikiria kama watu wote wangekua kama wewe unavyotaka dunia ingekuwaje?
Kama unaona unawajibu wa kumsaidia mzazi kama mwanafamilia unapaswa kufanya hivyo bila kujali itikadi zenu. Hilo linaweza kukutokea hata wewe inamaana uko tayari wote wanaokwenda kinyume na mtazamo wako kisiasa wasishirikiane na wewe?
Ni mtazamo tu
Baba yangu mzazi ambaye kwa 100% ananitegemea leo asubuhi nimepata habari kuwa amevunjika mkono wakati anatoka ktk kampeni ya CCM huko Rorya wa mbunge Airo.Cha kushangaza baba yangu tayari ni mzee sana na walichukuliwa na gari toka Kata ya ikoma na kusafiri mpaka maeneo ya bugombi karibu na shirati yapata 40km.Anasema walianguka kwenye gari kutokana na bara bara mbovu....sasa mimi ni chadema damu damu na napigania mabadiliko ili yaje mawazo mapya,watu wapya na sera mpya na hapa napigiwa simu nitoe fedha apelekwe hospitalini but sijisikii kusaidia hilo maana tuko maskini na yeye yuko hivyo(maskini) kwa sb ya sera mbovu za ccm.Je nimsaidie au nichune Nape au Airo amtumie?