Tujadili kwa pamoja wana jf

Tanganyika1

JF-Expert Member
May 10, 2011
418
81
Leo nimeshtushwa na kauli ya wazir mkuu kuwa bei ya umeme lazima iongezeke. Nkafanya simple analysis kuwa, nishati (mafuta + umeme) juu + bei ya bidhaa na huduma juu = gharama kubwa za maisha. Watu/wafanya kazi watadai nyongeza za mishahara ili wamudau gharama za maisha, hiyo itaongeza zaidi gharama za uzalishaji. Athali ni kupunguzwa kwa namba ya wafanyakazi ili kupunguza gharama, kupunguza ubora wa bidhaa ili kuzalisha bidhaa nyingi/kwa gharama nafuu, mfumuko zaidi wa bei....etc. Sasa hapa jf ndo sehemu pekee iliyo baki kwa kutafuta ufumbuzi wa matatizo kwa sasa. Nawaomba great thnkers tujadili hii hali na ku propose solutions. TAFADHALI SITEGEMEI MAJIBU YANAYO LAUMU WANASIASA. Just changia lakini usitoe lawama coz hzo lawama tusha choshwa nazo. Karibuni.
 

Robert kivuyo

Member
Sep 12, 2011
64
3
Hili balaa ss,kwanza hatuna budi kuelewa kwanza chanzo cha tatizo ndipo 2weze kutafuta uvumbuzi wa tatizo.Kwa upande wangu naona tatizo lipo upande wa serikali yetu kushindwa kucmamia raslimali yake.Ndio najua tatizo la mfumuko wa bei ya mafuta inategemea soko la dunia,lakin pia serikali kupitia wataalam wake upande wa uchumi wangeweza kutafuta namna ya kubalance kipato na matumizi kwa kuzingatia makusanyo ya fedha ya serikali bila ufisadi ndani yake mwananchi wakawaida aweze kumudu gharama za maisha.Serikali pia ingetakiwa kupunguza matumizi yacyo ya lazima kama wenzentu ulaya wanavyofanya ili kukabiliana na kuyumba kwa uchumi.Hilo lingesaidia kufidia sehemu ktk ongezeko la bei ya umeme.Lamwisho,niwakati ss Tanzania kubuni namna ya uzalishaji umeme bila kutegemea chanzo kimoja na kuingia mikataba ya kukodi mitambo ambayo yanachangia kuhujumu kipato cha nchi na pia serikali itoe fursa ya wataalam wetu kutumia utaalam wao kifikra na kimatendo kutafuta uvumbuzi.2kijua kabisa hata nchi zilizoendelea ilitegemea sana wataalam waliokuwa wakibuni mashine na mbinu mbalimbali ya kurahisisha maisha.Kwa kufanya hivyo 2takuwa 2metoka ktk enzi ya kutegemea wenzetu ndo 2ishi,angalia Cuba wanavyoweza kukabiliana na changamoto za kimaendeleo kwa sababu wamejikubal kama Wacuba na co dunia,kwa kufanya hivo itakuwa 2metoka kutegemea dunia ndo 2ishi.Mabadiliko pia kiutawala ni muhimu itaongeza changamoto ktk taifa.
 

Emanuel Makofia

JF-Expert Member
Jan 5, 2010
3,840
628
Pinda nae mbabaishaji tuu anatoa kauli za kejeli na za kinafki kwaq kuwa anajua fika maisha ya wananchi yalivyo
alikubali kutotulia v8 mpya ili walau viongozi wenzake waige lakini toka apewe huu uwaziri naona kila kukicha
anazidi kujisahau sana hajui kuna watu hata buku kwa siku tabu,
Amekwenda musoma ili kufika kwa marehemu baba wa taifa na hii ni baada ya kupigwa madongo bungeni
kuwa toka apewe uwazi mkuu hajawahi kufika kwa mzee.


tuliahidiwa bungeni ifikapo mwisho wa mwezi august mgao utapungua sana kwa kuwa aggreko na symbion watakuwa wanazalisha
karibu megawatt 120 na kufikia december tutasahau machungu ya mgao,mbona imekuwa kinyume???? NA hakuna
msemaji yeyote anaetupa sababu,wala waziri sijamwona hata katembelea hiyo mitambo na boss wake ndo amekuwa msemaji eti
bei ya umeme itapanda .jamani umeme upi???????? huu wa mgao .......................shame on uuuuuuuuuuuuuuuu!!!!!!
 

Filipo

JF-Expert Member
Jan 6, 2011
9,335
5,509
Mimi nadhan wakati umefika tanesco washushe bei ya kuunganisha umeme ili kuongeza idadi ya wateja na kuongeza makusanyo ya mwezi. Waige makampuni ya simu. Line iliyokuwa inauzwa zaidi ya 25,000 leo ni sh 100. Idadi ya wateja inaongezeka na wa makusanyo (faida) yanaongezeka pia. Ila hii itafanikiwa tu endapo mgao wa umeme utakuwa umekwisha! Bila hivyo hatutaweza kufikia mahitaji ya tanesco na umeme utapanda bei kila mwezi.
 

ndetichia

JF-Expert Member
Mar 18, 2011
27,770
6,521
kama wakipandisha bei ya umeme kaa ukijua hapo na yeye pinda anadau lake ndio maana anajitia lazima na sisi watanzania tubadili mfumo wa umeme ni kila kaya kumi mnanunua mtambo wa biogas ili muwe na umeme wenu kuliko kutegemea watu wasiokuwa na utu kwa watumiaji..
 

H1N1

JF-Expert Member
May 29, 2009
4,217
1,575
Mtego wa panya huingia wahusika na wasio wahusika,umeme unapandishwa kutokana na gharama za uendeshaji na uzalishaji wa NISHATI hiyo,gharama kubwa za uzalishaji wa nishati ya umeme zimechangiwa na rushwa,gharama kubwa za uendeshaji pia zimechangiwa na Ruswa ( kumbuka ilisemwa TANESCO Hutumia kiasi cha TZS 7,000.000 Service ya gari moja kwa mwezi,TANESCO wana magari mangapi ?),Rushwa imechangiwa na Uongozi mbaya wa CCM,Uongozi mbaya wa CCM unawekwa na wananchi ambao wengi wao umeme ni moja ya maajabu saba ya dunia,kwa kuwa wananchi wengi hawana umeme hawawezi kwenda na technologia ya mawasiliano wakajua maisha bora ya kwenye umeme,kutokuwa sambamba na mazingira ya dunia hii wanaamini umasikini na ujinga ni TUNU toka kwa muumba na CCM ndiye NABII mleta tunu,kwa imani Hiyo wanachi waliowengi wanaendelea kuiamini CCM ili wasijekosana na Muumba wao.

Huu ni mduara ambao tukiweza kuubomoa hakika pandisha pandisha ya umeme kwa kufidia wizi ama ufisadi wa wachache utakoma kabisa.
 

Lokissa

JF-Expert Member
Nov 20, 2010
7,442
2,466
kuna habari hiii mm sijaprove kwani nliambiwa na mkubwa mmoja yuko tanesco ila sijaprove anaetaka kujua amuulize mtu anaefanya kazi tanesco au songas kujiridhisha kuwa tanesco wananunua umeme kutoka songas kwa dola senti 80 na tanesco wanatuuzia sisi umeme huo huo kwa senti 8 tu pungufu ya senti 72 ambayo hubebwa na serikali kuziba hilo pengo, kwa hivo suala la umeme limekuwa linabebwa na serikali zaidi,kwa upungufu huo tanesco wanashindwa kumudu garama za vifaa na usambazaji.TANESCO ikija kubinafsishwa bei itapanda mara dufu itakuwa ngumu kwa wengi kulipa.Tanzania ni nchi pekee umeme wake bado tunanunua kwa bei ya chini,kwa waliowahi kuishi nje ya tanzania mtajua hali ikoje umeme wanawekewa wenye uwezo mkubwa na hata kulipa ni garama kubwa,mi nadhani bado tuishukuru serikali ya magamba kwa hili wanasaidia sana,

kwa vile sheria itaruhusu wazalishaji na wasambazaji binafsi basi kutakuwa na ushindani mkubwa bei itabadilika kutokana na garama za uzalishaji, pia tuelewe sisi ni nchi pekee shirika la tanesco limepewa majukumu yote ya kuzalisha, kusambaza na kuuza umeme ndio mana garama zinakuwa nafuu lakini huduma mbovu, nchi nyingine kusambaza na kuzalisha ni makampuni tofauti,na hata kulipia inabidi ulipe garama za umeme uliotumia na pia umlipe msambazaji hivo garama zinakuwa juu.
ndio hivo nijuavo kuhusu umeme kwa hivo pinda yuko swa ila sasa waboreshe maslahi yetu ili tuweze kumudu ongezeko
 

Shine

JF-Expert Member
Feb 5, 2011
11,483
1,358
Mimi nadhan wakati umefika tanesco washushe bei ya kuunganisha umeme ili kuongeza idadi ya wateja na kuongeza makusanyo ya mwezi. Waige makampuni ya simu. Line iliyokuwa inauzwa zaidi ya 25,000 leo ni sh 100. Idadi ya wateja inaongezeka na wa makusanyo (faida) yanaongezeka pia. Ila hii itafanikiwa tu endapo mgao wa umeme utakuwa umekwisha! Bila hivyo hatutaweza kufikia mahitaji ya tanesco na umeme utapanda bei kila mwezi.
<br />
<br />
Kama hii % ndogo ya watanzania wanaotumia umeme na hautoshi je watakapoongezeka si ndo itakua balaa kabisa
 

Shine

JF-Expert Member
Feb 5, 2011
11,483
1,358
Je kwa umasikini ambao tunao watz viongozi wetu wakiulizwa watajibu nini?
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

0 Reactions
Reply
Top Bottom