Tujadili kuhusu tafsiri mbalimbali za ujasiri

smarte_r

JF-Expert Member
Nov 8, 2013
4,538
11,868
Ujasiri ni nini?

>>Ujasiri ni kitendo kuacha kazi kabla haujapata kazi nyingine.

>>Ujasiri ni kumzungumzia vibaya boss wako au mkuu wako wa idara mbele ya wapambe wake.

>>Ujasiri ni kuizungumzia vibaya kampuni iliyokuajiri, katika mitandao ya kijamii kwa kutumia jina lako halisi.

>>Ujasiri ni kumtumia pesa demu ambaye mmefahamiana tu kupitia Instagram au Facebook baada ya yeye kukuomba.

>>Ujasiri ni kile kitendo cha wewe ambaye umri wako ni between 35 and 40, kupost videos TikTok ili utuonyeshe ulivyo mahiri wa kukata viuno na vituko mbalimbali.

>>Ujasiri ni kuingia Twitter kujiunga na wanaharakati mbalimbali (wapwa) kumtukana rais na cabinet yake, huku ukijua kabisa hizi ni nyakati za hatari na Twitter handle yako haipo well protected.

>>Ujasiri ni kutumia simu yako kupiga picha kambi ya jeshi, kupiga picha gari la mkuu wa idara ya usalama wa taifa au mkuu wa majeshi likiwa limepaki mtaani.

>>Ujasiri ni kusimama kandokando ya ukuta wa jeshi na kuanza kukojoa.

>>Ujasiri ni kumtumia girlfriend au boyfriend wako picha zako za utupu huku ukijua kabisa siku mkikorofishana, anaweza kuzitumia kukudhalilisha.

>>Ujasiri ni kufanya mapenzi na kahaba bila kuvaa kinga.

>>Ujasiri ni kutoka kimapenzi na mke au mume wa mtu huku ukijua za mwizi ni 40.

>>Ujasiri ni kuupangia apartment mchepuko wako na kuununulia fenicha zote za ndani.

Tuendelee kupeana tafsiri mbalimbali za ujasiri.

Karibu.
 
Well, perhaps he's wondering why someone would shoot a man...before throwing him out of a plane.
 
Ujasiri ni kutukana viongozi wakubwa wa nchi halafu yakikukuta mambo unalalamika eti udikteta wakati wewe ni mkristo na biblia imekuambia heshimu mamlaka na sheria zilizo madarakani.
Hatari hiyo.
 
Ujasiri ni kupuuza kulipa mkopo wako wa bank licha ya vitisho mbalimbali unavyovipita toka kwa maafisa mikopo wa bank husika.
 
ujasiri ni kujipa imani kwamba ipo siku ccm itaondoka madarakani kwa kupitia sanduku la kura.
 
ujasiri ni kitendo cha kusafiri kutoka mkoa mmoja kwenda mwingine kuanzisha mahusiano ya kimapenzi na mwanamke au mwanaume ambaye mmefahamiana kupitia badoo, instagram au facebook.
 
ujasiri ni kitendo cha kusafiri kutoka mkoa mmoja kwenda mwingine kuanzisha mahusiano ya kimapenzi na mwanamke au mwanaume ambaye mmefahamiana kupitia badoo, instagram au facebook.
[/QUOTMtu jasiri ni Yule ambaye ametendewa maudhi yaliyowazi dhahiri,anao uwezo wa kulipa kisasi asilimia 100 akaamua kusamehe! Hakurudisha matusi,hakujivuna juu ya uwezo wake wala mali wala mazoezi ayafanyayo ya karate,wala kusema anamiliki silaha! Huyu ndiye shujaa wa ukweli walobaki ama ni wataka sifa,madaraka,kujipendekezank
 
ujasiri ni kitendo cha wewe graduate wa chuo kikuu mwenye degree, baada ya kusota mda mrefu bila kazi, unaamua kutuma maombi ya kuomba kazi ya umesenja kwenye kampuni, ilhali qualifications walizotangaza ni za mtu aliyeishia kidato cha nne.
 
ujasiri ni pale demu mdangaji kuhongwa fedha na danga lake ambalo linalipwa mshahara mzuri kazini kwake, halafu dada huyo baada ya kufanya maendeleo, anatumia fedha zile kumuhonga bwanaake wa mtaani ambaye ni dereva wa bodaboda.
 
ujasiri ni kupiga picha sehemu zako za siri kwa lengo la kumtumia beibe, lakini kwa bahati mbaya unakosea na kuituma kwenye group la kazini huku ukijua kabisa huna mahusiano mazuri na HR.
 
Ujasiri ni kusema unaishi "jeneva uswizi"



nadhani sauti imetosha
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom