Tujadili kuhusu mtandao wa Halotel

Tujadili kuhusu mtandao wa Halotel

365

JF-Expert Member
Joined
Nov 28, 2014
Posts
1,377
Reaction score
1,460
Mtandao wa simu mpya toka Vietnam Halotel (vietel),utazinduliwa rasmi jumatano 14/10/2015. Ni mtandao utakaotoa Huduma kwa bei ndogo kabisa kuliko mitandao yote nchi nzima na Huduma zao zitapatikana vijijini, njiani, mijini, maporini na baharini, kila sehemu utayokua utakua hewani.

Watazindua na smart phones zao zenye ubora na garama nafuu kabisa,kwa kuzingatia kipato cha mtanzania Wa kawaida,
Mimi nitakuwa Wa kwanza kununua line ya halotel na smart phone ya halotel (vietel) sababu nimechoka unyonyaji Wa Vodacom na Airtel.
 
Huo mtandao ni mkubwa kiasi gani kuweza kutoa huduma vijijini,njiani,mijini,maporini na baharini?maana yake umewafikia watu wote nchi nzima?
 
Actually katika vijisenta vingi na miji kumesimikwa minara ya hili kampuni la mawasiliano hivyo nina imani mambo yatakuwa poa katika maeneo mengi-vijijini, njiani, maporini na baharini kwani kuna minara hadi kwenye isolated areas
 
Huo mtandao ni mkubwa kiasi gani kuweza kutoa huduma vijijini,njiani,mijini,maporini na baharini?maana yake umewafikia watu wote nchi nzima?
mkuu subiri tu uone lakn wamejenga minara nchi nzima na ukisearch wana internet ya 3G hadi vijijini
 
mkuu hadi znzbar watakuepo? mana kiukweli nimechoka na zantel
 
Sisi MAMLAKA YA MAWASILIANO TUNASEMA HIVI LAZIMA HALOTEL BEI ZAO ZILINGANE NA VODA TIGO AIRTEL N.K.
Kwahiyo watanzania jipeni matumaini hewa tu. TCRA
 
Last edited by a moderator:
mkuu hadi znzbar watakuepo? mana kiukweli nimechoka na zantel

Mitambo ipo on kwaiyo ili kujua kama wapo fanya manual seach ya operators eneo ulilopo utawaona wanatumia jina Hit TZ.
1444534561065.jpg 1444534561065.jpg
LAKN pia huko Zanzibar ulishaona wanachimba mitaro na kutandaza nyaya? Maana huku bara wametandaza nyaya karibu nchi nzima.

Mtandao wao una nyaya Inapita ardhini, huwezi ona minara mingi, wana minara michache alafu mirefu sana ile myembamba. Sehemu nyingine wamenyanyua juu nguzo kama za ttcl.

Hao ndio halotel wengine tushaanza watumia kama freelancer
 
Huo mtandao ni mkubwa kiasi gani kuweza kutoa huduma vijijini,njiani,mijini,maporini na baharini?maana yake umewafikia watu wote nchi nzima?

Ni kweli mkuu! Hawa Jamaa makubaliano yao ya kwanza na serikali ni kufikisha mawasiliano maeneo yote ya vijijini!
Pia wavute fibre optic cable maeneo yote ambayo serikali haikumaliza kulaza fibre optic cable
 
kabla ya kusifia huo mtandao inakubidi ujiulize swali hili!

je, huo mtandao utaendeshwa kwa sheria na taratibu za nchi gani?
-maana kama na Tz Kampuni pekee inayoweza kutoa huduma kwa bei nafuu ni ile iliyo chini ya serikali (TTCL) haya mengine hawawezi kwani kufanya hivyo itakuwa hasara kwao.
 
Mmenikumbusha ile kampuni nyingine ilikuja na same colour za orange hivi. Wakauza modem bei rahisi na watu wakabakia na modem Kama souvenir.

Shamba la bibi at your disposal, karibu Mgeni.

Nimekumiss mpaka naumwa...
 
Back
Top Bottom