Duuu inakera sana asee ilitokea hata kwenye shughuli yangu kuna watu waliitumia kama fursa. Kumbe kamekuwa ni kautaratibu ka mahali pengi!!
Hapo huyo alotunzwa naye alitunza wenzie kama hivo ni kama anarudishiwa na hapo msemo wa kutoa ni kuweka ndio hutumika
Hata sio jambo baya huku kwetu kuna vikundi hasa ikitokea mwanakikundi akaozesha au kuoza anatunzwa na wenzie japo harusi s yake tena huku kwetu ikiwa ni mwanamke anaolewa bas hao wenye vikundi hutunzana vyombo vya ndani ikiwa n mwanaume anaoa wanatunza vitenge, kanga, madira,mitandio na vitu vingi tu
Na si lazima kutunzana ila ukiona wameamua kutunzana ujue mifuko yao inaruhusu.
Kila sehem na utaratibu wake n kila mtu anayo jinsi anaishi anavyojua yeye,Suala si mifuko ila ni ile hali ya kuiba spotlight ya mwenzio. Mambo yafanyike mahala na wakati sahihi; si kutumia sherehe ya mwenzio kuwa eneo lako la mavuno!
Ulituza wenzio hatukatai, subiri sherehe yako au labda ya mwanao utuzwe nawe sio sherehe ya binamu, ya mpwa nawe unakaa kwenye kiti unafunikwa vitenge.
Kwanini usiandae sherehe yako mwenyewe hata ya kumshukuru Mungu kwa uhai?