Nimependa njia yako, unatumia mifano ya watu wa karibu, mitaani au macelebrities kuprove points zako?
Nakumbuka nimeharibu sana tu, wakati nakua; mama ndugu zangu walikuwa wakiniasa nilikuwa nawaona au wamepitwa na wakati au washamba.
leo kuna mengi nayakumbuka na ninajuta kama kaka yangu alivyowahi kuniambia "Kaunga, kuna muda wa majuto".
Nashukuru Mungu, sijaturn up to be worse (thanks to sala za mama yangu).
Lakini, ningekuwa mbali sana kama ningesikiliza na ku-slow down a bit.
Makosa yangu nimeyachukulia kama funzo, na kila nikipata nafasi nashare uzoefu na watu wengine (wadogo kiumri) na mwanangu pia.
Mara nyingine inakuwa ngumu sana na inauma unapomuona binti, kijana anapoelekea so unatumia hata vitisho (una-exaggerate issue) ili mradi tu asifanye kile unachomkataza (baada ya reasoning kushindikana of course).
Hii ni kutokana na kwamba, niliishi yale maisha once (nilipata nafasi ya kukosea na kujifunza kutokana na makosa hayo)
sasa maswali au changamoto zangu ni kwamba;
-ni kwa mambo gani tunaruhusu wanetu, dependants wetu wakosee hoping watajifunza kutokana na makosa?
-kwa mambo gani tunakuwa strict mpaka mwisho?
-ni sahihi kutumia vitisho (pale inapolazimika) ili kuprove point au kumscare kijana (mf: ushoga)?
-kwa utandawazi, maswala ya dating kwa teenagers tunafanya nini (i started dating when l was a teen)?
-is it fair kumzuia mtoto yale ambayo wewe uliyapitia? au kuna jinsi ya kumguide ili asipate madhara au awe responsible/
karibuni kwa mjadala, na samahani mtiririko unaweza kuwa sio mzuri sana.
Je ni muda (umri) gani wa mtoto unakuwa reasonable kuanza 'mazungumzo' haya? Huwa naogopa sana kuanza akiwa mdogo sana nahisi kama naweza kuwa chachu ya yeye kujaribu, au ni uoga wangu tu?
Kwa mtazamo wangu ni hivi, si vizuri kumwacha mtoto apitie yale makosa uliyopitia wewe wkt unakua.ni vema ukae naye/nao na kuwaeleza ukweli wajue positive na negative ya mambo mbali mbali hususani wakiwa wanaelekea ktk teen ages.akishajua positive and negative then risk iko kwake mwenyewe kama ataamua kufanya ama kuavoid.Kuna makosa ambayo tulifanya wakati tunakuwa kwa vile wazazi wetu hawakuwa wazi kutuelekeza what to do,so unajikuta tayari umeshatumbukia ktk tatizo na huna msaada.mi nadhani pamoja na mengineyo ni vzr kuweka wazi kila kitu then maamuzi yabaki kwake.
Too bad mama yangu aliondoka mapema ila since niko mtoto kulikuwa na constant battle kati yake nami kila nililokuwa nafanya alikuwa anani critisize like nimepata 90 kwenye maths nikija homu na furaha na kumwonyesha utasikia anasema wenzio wanapata mia wewe wa tisini wafurahia nn? Kiukwel ilikuwa inanivunja moyo sana so nilikuwa nafanya mambo mengi kwa juhudi ili nimprove wrong,nilikuwa vizuri kwenye michezo tabia,kanisani nilikuwa mwanakwaya mzuri misa ya watoto nk na wengi walikuwa wananisifu kuwa ni mtoto wa pekee bt to me haikuleta maana, nimekuja kumwelewa mwishoni kuwa alitaka niwe the best among the rest !!!
Maisha tuliyoishi na maisha ya malezi ya watoto au wadogo wetu wa sasa yameebadilika sana hata kufikia hatua ya kuitwa washamba kwenye kila jambo la msingi tunalolikaripia.....Kuna wale walezi waliamua kuwa bendera kila upepo ulipo nae yupo hawa hawataki kuwaeleza vijana ukweli kwa kuhofia kuonekana washamba ama wazamani....tofauti na mimi na kundi la walenzi wanaotetea maadili hata kama tutaonekana washamba au waliopitwa na sayansi na teknolojia. Hakuna tofauti ya maadili zamani na sasa ila kilichobadilika ni namna ya kutoa ujumbe mfano zamani ilikuwa ukivunja maadili hata asiyekufahamu alikuadhibu na ukifika nyumbani ukasimulia kama ulikera kichapo kinaanza tena ila sasa hata watoto wa dada/kaka yangu wa damu siwezi kuwakaribia au kuwaadhibu, hatari baadhi ya wazazi hawawezi kuwakaripia/kuwaonya watoto waliowazaa.....Ndio maana wakati wako ulitambua makosa na sasa unajutia, ila wa sasa hawayajui makosa na hivyo muda wa kujutia hawaupati na mwisho wanaangamia
Do people plan on making mistakes or its just something that occurs spontaneous? and to the kids, making mistakes is the part of learning and growing process
Afu shule zenyewe za siku hizi wanafundishwa mambo meeengi wakiwa wadogo bora kwenda nao sambamba tu.
Angalau mzazi utamfundisha ukweli.