Tuitizame ikulu sasa…. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tuitizame ikulu sasa….

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Msanii, Mar 11, 2010.

 1. Msanii

  Msanii JF-Expert Member

  #1
  Mar 11, 2010
  Joined: Jul 4, 2007
  Messages: 6,427
  Likes Received: 370
  Trophy Points: 180
  Ikulu ni makazi ya Tanzania ni ofisi na makazi ya raisi. Ikulu yetu ilijengwa kwanza na wajerumani walipokuwa wakoloni wetu kabla ya kulipuka kwa vita kuu ya pili ya dunia ambapo mwingereza aliitwaa baada ya kumtimua mjerumani. Waingereza waliongeza sehemu ya juu ya jingo hilo pasipo kuathiri asili ya ujenzi wake. Hapo kuna kitu kinaitwa building code yaani viwango vya ujenzi. Wajerumani walijenga ikulu zao ndogo katika baadhi ya miji waliyokuwa na maslahi nayo na ukitizama viwango vya ujenzi wa ikulu hizo (boma) hazina tofauti sana na kitovu cha boma zote yaani ikulu kuu. Hizi ikulku ndogo ziligeuzwa kuwa ofisi za wilaya na makazi ya wakuu wa wilaya nap engine mkoa baada ya uhuru 1961. Majengo mengi ya serikali enzi za wajerumani yalikuwa ni alama ya utukufu na enzi za Ujerumani na hasa hasa viwango vya ujenzi ambavyo serikali ya Ujerumani wameweka.

  Tunapiga hatua za maendeleo katika zama hizi za sayansi na (wizi wa ki-) teknolojia lakini tunasahau vitu muhimu sana kama alama za Taifa letu. Hivi sana tunapiga hatua nzuri katika namna tunavyojenga nyumba zetu ziwe za kuvutia bila kujali aina ya nyumba itakiwayo. Lakini hatuna msingi wa namna ya ujenzi unotakiwa kutokana na hali ya nchi na matumizi. Ingawa kuna utaratibu mzuri ambao unamlazimisha mtu anayetaka kujenga kuomba kibali cha ujenzi, na kibali hiki hutolewa na baraza la madiwani ambapo kwa mtazamo wangu naona ni hatua sahihi sana. Ila tulipaswa kufikiri nje ya hapo zaidi yaani kuwepo na sababu ya mtu kuomba construction permit. Yaani tungelikuwa na building code ambayo imepitishwa na baraza la madiwani/ wakandarasi/ wahandisi et cetera. Hii ingelikuwa ni suluhisho la ujenzi holela unaozidi kushika kasi hivi sasa. Anaweza kuja mlevi hapa akasema kuwa MSANII unaingilia ama unaibaka demokrasia ya ujenzi. Nasema mlevi kwa sababu demokrasia ya ujenzi ndiyo imetufikisha hapa yaani uharibifu wa mazingira. Demokrasia ya ujenzi ingekuwa kwa maeneo machache yaliyotengwa kwa watu wanaotaka kufanya utundu katika ujenzi. Ninaamini kwamba wahusika watapita hapa na kusoma ili wanapokaa huko kwenye kutunga sera zao waje na sera tekelevu za ujenzi kwa mpango. Pia itapunguza uvamizi holela wa maeneo unaofanywa na watanzania wasioelimishwa kuhusu kanuni na sheria zilizopo.

  Pia kwa ufupi tukubaliane kwamba miji yetu hasa jiji la Dar hakuna bustani za watu kupumzikia au hata kufanyia matukio ambayo yana viwango vya kufanyikia bustanini. Watakuja wala mirungi hapa watasema kuna botanical garden (nyuma ya southern sun hotel). Uchuro mtupu maana ile bustani plan yake ni ekari 40 lakini pale ilipo ni kama kitalu cha maua na mimea adimu tu. Bustani ni project kubwa inayohitaji utaalam na uangalizi mzuri kwani huweza kutumika kama tiba ya kisaikolojia na baadhi ya maradhi kwa wanaotembelea bustani. Kuna faida nyingi za bustani ambazo wewe unazijua baadhi.

  Nimeanza na IKULU , namaliza na IKULU. Ikulu yetu katika suala la mazingira ipo ipo tu. Zaidi watendaji wa ikulu watajisifia mandhari nzuri ndani ya maeneo ya ikulu hasa yale maeneo yanaoonekana kirahisi na mkuu wa nchi. Nje ya maeneo ya ikulu ni kichefuchefu kitupu, yaani ni hovyo hovyo tena holela. Hakuna bustani wala mfano wake. Mzururaji yeyote anayepita maeneo ya ikulu atavutiwa na utulivu wa eneo lenyewe lakini ukuta ni mchafu na upo uchi. Barabara zinazopita kuzunguka ikulu hazina mfano wa barabara salama. Hakuna pavements za watembea kwa miguu wala watumia baiskeli. Mvua ikinyesha si ajabu kukutana na vidimbwi vya maji katika maeneo yanayozunguka ikulu yetu. Hata miti iliyopandwa kuzunguka ikulu ni ile ya adam na eva yaani tangu zamani ambapo baadhi imeanza kuanguka. Sehemu kubwa ya miti ipo ndani ya ukuta wa ikulu. Yote ni tisa…. Kumi ni ndani ya uzio wa ikulu upande wa kusini magharibi mkabala na soko la samaki. Kuna provision ya wanyamapori waliojengewa uzio na nje ya uzio huo kuna majengo kadhaa ambayo yameachwa yaanguke yenyewe kwani hakuna dalili ya matumizi wala ukarabati. Au inawezekana yakawa ni majengo yenye matumizi maalumu maana hizi ikulu zetu za kiafrika ni Mungu pekee anayejua yanayotendeka humo ndani. Kwa mimi ambaye ninahaha kusaka nyumba ya NHS ya kukaa halafu ninaona jingo la serikali ambalo linaweza kutengenezwa kasha mfanyakazi wa serikali akapata makazi humo huwa napandisha mori kinoma. Ningependa kufahamu matumizi ya bajeti (isiyorejeshwa) ya utunzaji ikulu inatumikaje? Na kama wahusika hawajaona umuhimu wa kuboresha mazingira ya ikulu ni wazi kabisa hawamsaidii Rais kwani kisaikolojia anapaswa kufanya kazi kwenye mazingira mazuri na maridhawa. Pia kuna maendeleo mazuri kwenye lango kuu la ikulu ambapo kuna bustani na mabalasi ya maua (yamepakwa rangi za bendera ya taifa) yaliyowekwa kwa mpango mzuri ila kuna fyongo imefanyika pale. Nikiwa msanii tena m-bunifu nimesikitishwa na viwango vya upakaji rangi wa mabalasi hayo. Inaonesha Ikulu haina habari wala mfumo wa viwango wa kazi za ubunifu zitakiwazo kukaa ikulu. Yale mabalasi yamepakwa rangi ya bendera ya taifa kiholela pasipo na mfuatano unaoeleweka yaani colo regions boundaries zimepindapinda na zimeingiliana hata ukiwa distance unaona. Na kibaya zaidi wametumia rangi za mafuta zitumikazo kupakia nyumba. Je Ikulu hawana mtaalam/ mshauri wa masuala ya sanaa za mapambo? Nakumbuka enzi za mwalimu (nilikuwa mtoto) kulikuwepo na wasanii waliopata hata kuishi pale ikulu kwa minajili ya kuboresha sanaa-mapambo ya ikulu na mengineyo. Nadhani badala ya Ikulu kutumia sources zake kutafuta wasanii au wabunifu bora (inawafahamu) badala yake watendaji wake wanaingia mtaani kusaka waganga njaa ili wafanye kazi upakaji rangi wa mabalasi ya maua ilhali wapate cha juu. Inji hii bana we acha tu. Ninasita kuzungumzia usafi wa jiji letu kwa kuwa Ikulu bado haijawa mfano wa usafi. Mwanafalsafa mkuu, Yesu alisema.. "… ewe farisayo … Safisha ndani ya kikombe kwanza ili nje kipate kuwa safi"

  Lazima mfano wa land planning uanzie kwenye ikulu yetu ndipo tutajitia adabu ya kuweka viwango bora vya ujenzi wa majengo ya serikali, maafisa wa umma na sisi makabwela. Katika masuala ya kitaifa hasa yanayohusu common interest tunapaswa kuweka mambo ya siasa mbali. Ni lazima tufike mahala tuwe wamoja kwa certain important issues. Tutengeneze sera za taifa kasha kila chama kije na sera za kuwezesha utekelezaji wa sera za taifa. Ninaamini kwamba kama (KWA DHATI) tukiwa makini katika kutunza mazingira kwa dhati ipo siku theluji itaanguka katika ardhi ya Dar es Salaam.

  Source: Wino wa Msanii
   
 2. Waberoya

  Waberoya Platinum Member

  #2
  Mar 12, 2010
  Joined: Aug 3, 2008
  Messages: 11,590
  Likes Received: 3,887
  Trophy Points: 280
  Tuitizame ikulu sasa…. haya, kama wanasikia
   
 3. Msanii

  Msanii JF-Expert Member

  #3
  Mar 12, 2010
  Joined: Jul 4, 2007
  Messages: 6,427
  Likes Received: 370
  Trophy Points: 180
  kama kawaida yao
  tunajua hawajali maana wanadhani wana hakimiliki na jengo lile ilhali wanatukata kodi zetu
   
Loading...