Tuisaidie Taifa Start ili nchi isipate aibu!

Tuisaidie Taifa Start ili nchi isipate aibu!

Aiseeeee yaani jana niliona aibu jinsi timu yetu ilivyokuwa inapigishwa samba na nchi kama madagascar, jinsi Oscar Joshua alivyokuwa anapigwa tobo, Nyoni alivyokuwa uchochoro upande wa kulia, jinsi boko alivyokuwa anatoa ulimi nje nje kama mbwa anaetoka mawindoni.

Ila iliniuma sana nilipomuona kocha kilaza amevaa kofia yenye rangi ya bendara yetu ya tanzania....
Yaani kwa starz ile ya cosafa kukutana na Misri na Nigeria tutakula kama za Brazil na German.,..

Mkuu, huyu Jamal Malinzi anatakiwa kuchukua hatua kutuepusha na hii dhahama inayokuja.
 
Last edited by a moderator:
uyo kocha wao kama amesahau nguo huku mtu amkimbizie haraka akapande ndege huko huko asirudi huku. ni kocha dhaifu kuliko wote, bora hata wabongo wenzetu wangefundisha. unafungwa na swaziland nchi haina mbele wala nyuma, unafungwa na madagascar? hii aibu gani jamani.

Tatizo sio Kocha tatizo TFF
 
Kwanza huyo Jamal Malinzi aondoke kabisa TFF akatafute kazi nyingine za kufanya, hana ubunifu, hana mawazo, hana ujanja, haijuwi soka, hawezi kuiendeleza soka hata awepo hapo miaka 100.

Sijuwi hao waliomchaguwa walikuwa na kigezo kipi kilichowafanya wachaguwe.

cc Bishanga

Umenena Vema,MALINZI ndo tatizo huyu mtu hatatufikisha popote
 
Last edited by a moderator:
Kwa Taifa Star hii, tutaondoka na kapu la magori katika mechi za kufuzu Afcon.

NOTE: Misri, Nigeria, Chad tupo nao kundi moja.

Kila tutakapocheza na hizo timu nitavaa na kushangilia hizo timu,mpira wa Tanzania hauna maana ni kutiana presha tu
 
Malinzi kwa mda aliokaa ametuangusha sana watu wa soka,,,Taifa stars imepoteza mvuto..timu ipo bora liende tu..Malinzi mawazo yake yeye ni timu kubadili jina,,kubadili jezi,,kupeleka timu tukuyu sijuu maboresho,,kumfungia ndumbaro miaka saba,,,kuhamisha ofisi karume,,,yani jamaa hana mipango ya mda mfupi wala mrefu,,,unakuwaje kiongozi mkubwa hapo TFF..hauna mission wala vision..yako kwenye big organization kama hiyo....Huyu kocha ndo sijui walimtoa wapi...
 
Nimeangalia mechi mbili za COSAFA ilizocheza Taifa Stars. Ukweli inaboa sana kuona timu inayogharimiwa kwa kiwango cha hali ya juu na wadhamini TBL na NMB ikicheza mchezo wa ovyo kabisa. Inaonesha vijana bado hawajajitambua wao ni nani na kwamba kupata opportunity ya COSAFA ni pamoja na kujitangaza. Kwa ufupi timu ilikuwa na mapungufu yafuatayo:
1. Hawakuwa na ari ya mchezo kabisa. Yani walikuwa wanakimbia kimbia tu, pasi hazifiki kwa mlengwa, hawakuwa na malengo.
2. Hawakuwa na hamasa ya kucheza. Kiongozi ambaye ni captain John Boko hakuonesha kama leader, hakuwainspire wenzanke na wala kuonesha ni jinsi gani ya kucheza mchezo kuleta matokeo. Badala yake alikuwa anakimbia na kuanguka ovyo, anacheza faulo na hashambulii. Imagine team imepiga shuti la kwanza dk ya 38 (dhidi ya Madagascar)
3. Mfumo uliotumiwa haukuwa unaeleweka, kocha kasimama hatoi maelekezo, kikosi kapanga kibovu, wachezaji hawana plan B yaani pamoja na kufungwa mabao mawili bado mchezo ulikuwa uleule.
4. Yaonekana timu ya Taifa ni wale vijana wa TP Mazembe. Nilitarajia kuona Ngasa na Msuva wakituonesha kwanini wanastahili kucheza nje ya nchi lakini wapi. Huyu Msuva ndio kabisa hakuwa msaada eti ni mfungaji bora aliyefanya mazoezi na timu ya Wits. Napata mashaka kama kweli alifanya majaribio ya dk 45 tu wala hajui kocha wa timu wala wachezaji waliofanya mazoezi naye.Duh. Sasa alipata dk 270 za kucheza mechi 3 ingekuwa ni opportunity yake kujitangaza ila kiwango kibovu. Mwenzake wa Uganda yule Andrew Mwesigwa kashinda majaribu na kasajiliwa na Wits.
5. Uwakilishi wa taifa sio mchezo. Timu ya Taifa inawakilisha taifa. Kabla ya mechi zinapigwa nyimbo za taifa kuonesha uwakilishi wa nchi kama ambavyo viongozi wakuu wa nchi wanavyopigiwa nyimbo. So wachezaji wanatakiwa kuwa proud kupata nafasi ya namna hiyo waoneshe kiu ya ushindi na kujituma kama wanavyojituma wachezaji wengine. Angalia waliotufunga walivyokuwa wanacheza.
6. Timu ya taifa haina mpango wa kuwajenga vijana wadogo wataokuja kurithi nafasi za wakongwe. Nilikuwa naupenda mfumo wa Maximo ilikuwa kila mchezaji lazima ajitahidi ili kupata namba ila huyu Nooj amekumbatia wachezaji walewale na hakuna ushindani kwani kila mtu amejiwekea namba yake bila kujali kiwango hata kama kwenye timu yake ya ligi hapati namba bado kwenye timu ya taifa ana uhakika.
7. Tangu mwaka 2006 tumekuwa na makocha wa kigeni bila mafanikio ya maana. Tumebadilisha makocha kwa gharama kubwa bila kuwa na mafanikio. Wenzetu Nigeria wameachana na makocha wa kigeni angalia Super Eagles ilivyocheza world cup. Walijitahidi sana na kwa kiwango kizuri.
Mapendekezo:
1. Babu Nooj asifukuzwe bali mkataba wake usitishwe
2 Wachaguliwe makocha wazawa wa Taifa stars, wapewe mikataba minono na malengo. Waangalie wenye haiba ya ufundi na uhamasishaji wa kiwango cha juu. Kuwa na pool kubwa ya wachezaji na wachaguliwe kulingana na viwango vyao.
3. Kuwe na wasaidizi wenye haiba ya uchapa kazi kama Julio, Mexime, Minziro. Makocha wa magolikipa kama Juma Pondamali. Kuwe na msemaji wa timu mwenye hamasa kama Masau Bwire yaani hata maneno yake kabla ya mechi yanahamasisha na wachezaji wanajituma. Hii itachangia sana hamasa. Najua kuna watakaopinga ila mchezo unachezwa uwanjani na nje ya uwanja (psychology)
Kama hakutakuwa na mabadiliko yeyote naona yafuatayo kwenye mchujo wa AFCON
1. Egypt 6 Tanzania 0
2. Nigeria 3 Tanzania 0 na matokeo mengine mabovu.
TFF twaomba mabadiliko makubwa sasa ili kurescue timu yetu ya Taifa. Tumekuwa wanyonge sana.
Mungu ibariki Tanzania.
 
Hiv nyie mpaka leo mnajitesa kuangalia taifa stars?nimeshaacha siku nyingi.
 
Kim alikua kwenye right track kwa vile alianza na timu ya vijana, huyu Malinzi sijui alikula maharage ya wapi kumfukuza
 
Mtanzania toa maoni yako ni kitu gani kifanyike ili timu ya Taifa iondokane na hii aibu ya kila mwaka! Je tatizo ni kocha au? toa mawazo yako hapa ili hata Jamal Malinzi akipitia hapa aweze kuona watanzania wanasema nini juu ya timu yao ya taifa.Hii ni aibu tuisaidie timu yetu.

hata hao COSAFA walifanya makosa kuialika tanzania, kwani hawajui kuwa hakuna tunaloliweza??.
 
Last edited by a moderator:
hivi huyu kocha tangu aingie amesha wahi shinda mechi yoyote ile?
 
hivi huyu kocha tangu aingie amesha wahi shinda mechi yoyote ile?

Mkuu, katika mechi 15 alizoongoza kama kocha taifa starz, ameshinda 3, kupigwa 6 na droo 6,............

Atimuliwe hatufai huyu, baada ya hapo Malinzi nae ajiandae kutuachia shirikisho letu.
 
H20 ubovu wote wa timu umewaona Ngassa, Msuva na Boko basi. Wengine walikuwa wapo vizuri?

Kama ni wote do not name names!

Issue ipo wazi - hatuna kocha. Full stop. Unadhani Messi anaweza kuwika kwenye mfumo wa Mourinho kwa mfano? Kuna wakati timu inaweza kufungwa lakini mchezo ukawa wa kuleta matumaini.

Ubovu wa kocha ni kama homa, kiini cha ugonjwa ni Malinzi.
 
Yaan naona aibu na fedheha ktk game za mbeleni kwa taifa uyu kocha aende zake tu mapema kabla hatujamletea noma,timu haimu ata mwelekeo

Misri na nigeria watatufanya vibaya,yan malinzi mpira unaurudisha kipindi cha fat ww
 
Tupige marufuku taifa starz kama ilivyokuwa miss tanzania. Badae waje wakiwa wamejipanga.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom