Tuikubalie DR Congo kujiunga na EAC?

Mkuu Malcom Lumumba umemaliza kila kitu, binafsi sikuwahi kuafiki Rwanda, na Burundi kujiunga EAC pia siafiki hili la Congo DRC kujiunga EAC, lakini sababu ulizozitoa zimenifundisha vitu vingi sana na the moment namaliza kuisoma nukta ya mwisho tayari kichwa changu kilishajenga Action Plan.
Uliyoyaongea naona yanafanyika kinyume yakionyesha tabia halisi za kiafrika ni kama tunataka kuanzia pale wenzetu walipofikia yaani kwenye success point za wenzetu badala ya kurudi chini na kutengeneza njia zetu.
Pia, kwa kudhani wingi wa rasilimali ndiyo huleta nguvu na mshikamano wenye tija tunakosea sana, kwetu Congo DRC anaweza akawa ni fursa nzuri kuliko mwana jumuia mzuri, tunaangalia zaidi rasilimali na rangi yake hatujiulizi rasilimali za Kenya na Tanzania zimeinufaisha vipi Jumuiya.
Kwa mchanganuo ulioutoa EAC inaweza ikajulikana zaidi kama EAVC (East Africa Violence Community)
 
Mkuu Red Giant!

Malcom Lumumba amemaliza kila kitu, na nikiongeza tu, NITAHARIBU!!

Unajua kwanini nitaharibu?!

Mosi, nami nilitaka kuongea hivyo hivyo kwamba DRC tusimkaribishe, lakini kinyume na Malcom ambae ameongea Kizalendo zaidi na kwa hoja zilizoshiba mbolea, mimi nilitaka kuweka maneno ya kizalendo na ya kibeberu kama yale ya kutaka tuwaunge mkono Misri dhidi ya Ethiopia kwenye suala zima la matumizi ya maji ya mto Nile!

Wakati malofa wangetupongeza kwa "ubinadamu" wa kuwahurumia Mafarao wasio na chanzo kingine cha maji, kumbe moyoni tunataka kumzuia Ethiopia asiwe ndie Super Power wa Umeme kwenye ukanda huu!!!

Kwanini tuwaache Ethiopia wawe ndio East and Central Africa Energy Pool tena kwa umeme cheap wa maji wakati na sisi tuna gas kibao ya kuweza kuzalisha umeme na hatimae kuwa ndio kuwa East and Central Africa Energy Pool?!

Yaani ningekuwa na hoja zile zile za Kibeberu za kutaka "tuwaunge mkono" ndugu zetu Wakenya dhidi ya Mchina pale iliposemekana eti kwa madeni waliyokuwa nayo Wapwa zetu Wakenya, basi kulikuwa na hatari Wachina wangeibeba Bandari ya Mombasa kama ilivyosemekana kuhusu Wachina na Hambantota Port.

Dunia na Afrika kwa ujumla wangetushangilia na kutupongeza kwa "kuwapigania" Wapwa zetu Wakenya kumbe deep inside our imperialism mentality, tunajua Mchina akiingia Mombasa basi Bandari ya Dar es salaam ijiandae kuwa bandari ya kupokea majahazi yenye mizigo kutoka Mombasa!!

Ni mawazo hayo hayo ya Kibeberu ambayo kimsingi yamejaa "umimi na ubinafsi", ndiyo yangenisukuma zaidi kutaka DRC isiingie EAC!!

Kwanini nisilete Ubeberu ili hatimae potential ya DRC tuifaidi peke yetu?! Na ninaposema potential, wala sizungumzii raslimali za DRC, kwanza I don't believe in mining economy na ndio maana mara kadhaa nimekuwa nikizungumzia "too much" energy anayowekeza JPM kwenye sekta ya madini.

Hapa nazungumzia Geographical Potential!!

Na Malcom umeongea jambo la msingi sana... kwamba sisi na Wakenya tumefanana mno, na matokeo yake tumekuwa kama Sunche na Kapeto!!! Ni kutokana na hilo, ndo maana mara zote tumekuwa ni watu wa kuhujumiana tu! Na upande mmoja unapokuwa na Mabeberu kama chige, ndo basi tena!!!

Ila tuache masihara! Hawa Wapwa zetu ni Manyang'au yaliyokubuhu haya!! Usipoyaendea Kinyang'au nyang'au haya, yanakutoa nishai mapemaaa halafu yanakucheka 🤣🤣🤣!!!

All in all, Malcom Lumumba umeongea mambo mazito sana, tena umeyaelezea kisomi sana ingawaje kwa lugha nyepesi inayoeleweka!!

Much respect!
 
Hawa wakina MK254 ni watu wenye tamaa na manyang'au kweli, wala siyo wongo lakini ni watu muhimu sana kwetu: Yani Tanzania na Kenya ni kama Siamese Twins inabidi tushirikiane sana kujijenga. Tukiwa imara ndiyo tuanze kupeleka mikono huko kwingine. Japo nafahamu siyo jambo rahisi hata kidogo kwa watanzania kuwaamini hawa jamaa.
 
Points muhimu ziko ktk posts hizi

Kikubwa kwanza Congo ijijenge zaidi ndani ,kisha ndio ifikirie kujiunga EAC ,Congo siasa za ndani bado kdg

Harakati za sasa za kupunguza mapigano Mashariki ziongezwe
 
Of course, na mimi ni mfuasi mkubwa sana, tena sana kwenye masuala ya ushirikiano na ndio maana mara nyingi kwenye hili suala nimekuwa nikitumia terms mbili... Ushirikiano na Uhusiano!

Linapokuja suala la ushirikiano, I don't judge no body provided taifa kama taifa linanufaika kwenye ushirikiano! Ni kama ambavyo nilipata kusema kwamba, there's no way taifa kama Israel linaweza kuwa na undugu na Tanzania (international relation) lakini hiyo haiwezi kuwa sababu ya kufanya Tanzania isifanye partnership na Israel (international cooperation)!

Kwa Kenya, weather we like it or not, sisi ni ndugu tena ni undugu unaoenda mbali zaidi ya common international relation! Lakini mbali na kuwa na uhusiano, Kenya ni partner in business kwa levels zote... from individual to state level, so there's no way unaweza kukwepa ushirikiano na taifa lenye sifa kama hizo!

Na ukichukua nchi zote za Afrika Mashariki (tradional + modern EA), pamoja na ujanja ujanja wao wote, bado Tanzania tuna nafasi kubwa zaidi (in terms of monetary value) ya kuuza Kenya kuliko nchi nyingine yoyote ile ukanda huu!

Pamoja na unyang'au wao wote, kwangu mimi Kenya is an Opportunity and not a Threat! Kenya anaweza kuwa threat only if you don't know how to handle mataifa kama ya Kenya!

Isitoshe, Tanzania anaweza kuwa na fursa ya kuuza zaidi Kenya kuliko Kenya alivyo na fursa kama hiyo kwa Tanzania ukiondoa financial sector, ambayo mabenki ya Tanzania ni kama yamesharidhika na soko la ndani ingawaje ukweli ni kinyume chake!
 
Hakika Mkuu, Hakika!
 
Moja ya vitu ambavyo Rais Felix anajaribu kuviweka sawa ni hilo la USHIRIKIANO NA UHUSIANO

Lkn hayo hayatofanyika km kule mashariki hapajatulia ,na juhudi za sasa EAC na SADC ni kusolve issue ya kule kisha kuangalia hili tunalojadili

Mashariki pakitulia na Congo ikatulia ,Hili linawezekana
 
Mkuu Malcom Lumumba , ahsante

Hili suala tulilijadili sana kabla ya Rwanda na Burundi na hata South Sudan au Somalia

Nitaanzia kwa hoja ya Chige kuhusu mahusiano ya Tanzania na Kenya na ushindani uliopo

Tanzania ijalaumu ndani ya EA. Ni nchi iliyo na rasiliamali arable land , utalii na madini.

Uwepo wa EA ilikuwa fursa ya soko la Tanzania. Tuna mifano michache.

Katika miaka ya karibuni Kenya imeitegemea sana Tanzania kwa nafaka kama Mahindi.
Bado Kenya ina export Ulaya vitunguu vya Karatu na Maua ya Arusha.

Soko la nafaka kwa EA na SADC ni kubwa sana, tunashindwaje kutumia ardhi kuliteka?

Hii maana yake kama tungetumia ardhi yetu kwa Kilimo sisi ndio tungelisha EA na SADC

Tungeuza matunda ya Tanga, Vitunguu, mboga mboga, Maharagwe, Mchele, Mahindi n.k.

Nyanya zinazooza Morogoro na Iringa, matunda yanaharibika Muheza na Lushoto.
Mahindi yamekwama Sumbawanga , Mbeya na Ruvuma.

Mpunga hauna soko Shinyanga, Morogoro n.k. Sababu kubwa ni kushindwa kuuza, kushindwa kuhamasisha uzalishaji wa biashara.

Tunatumia muda mwingi kufanya ''intelejensia'' za watu wetu na si za uchumi

Kosa letu ni kushindana na Kenya maeneo ya Utalii na Viwanda wao wakiwa na upper hand

Tunaweza kufanya utalii na viwanda huku tukilisha EAC yote bila tatizo.

Kuhusu Kupanuka kwa EAC, hili ni kama ulivyoeleza.

Nchi za Ulaya hazikuanza juzi zilianza kuanzia miaka ya 50.
Kilichotokea siku za karibuni ni Expansion hasa kutoka na mabadiliko geopolitical ya dunia.

Tulipaswa kuimarisha EAC ya Kenya , Uganda na Tanzania ili wajao wakute misingi imara

Expansion ya kuwaingiza Rwanda na Burundi imerudisha nyuma sana jitihda za Jumuiya
Migogoro ya nchi kama Burundi ilisababisha mkutano wa wakuu kutofanyika

Tulitegemea South Sudan kama nchi yenye rasiliamali, nako ni matatizo tu.
Tumeshindwa kutumia fursa ya soko lililopo na linalopanuka, leo tunadhani DRC ni muhimu

Ikiwa DRC ni muhimu kwa rasilimali kama wanavyodai, basi wasingekuwa na matatizo
Kuwakaribisha ni kukaribisha migogoro zaidi ya mafanikio

EAC ya 1977 ilikuwa na nguvu sana na tungeweza kutumia ushirikiano na mataifa jirani

Kuwakaribisha hakujaonyesha kama kuna tija kiuchumi zaidi ya changamoto za usalama

EAC inatakiwa ijengwe kwanza kiuchumi halafu ipanuke kukiwa na misingi imara
Ndivyo EU ilivyojengwa na mataifa machache kisha kuwakaribisha akina Lativia n.k.

Kwa Tanzania, tunapakana na nchi 8 kubwa! swali tusilojiuliza na tusilotaka kuuliza, ni kwanini tumeshindwa kutumia fursa iliyopo kwanza hadi tudhani tunahitaji DRC na Somalia?

JokaKuu
 
Mkuu Nguruvi3!!

Umemaliza kila kitu! Na hata niliposema Tanzania ina fursa zaidi ya kuuza Kenya in terms of monetary value kuliko ilivyo Kenya kwa Tanzania, focus yangu ilikuwa ndiyo eneo hilo hilo uliloelezea... agribusiness! Inasikitisha kuona hatuitumii fursa hii ipasavyo!
 
Na Tanzania tupo vizuri sana kwenye suala la siasa za uhusiano lakini huwa tunafeli kwenye suala la ushirikiano! Kuna siku niliwahi kueleza hapa kwamba, moja ya maeneo tunayofeli ni pale kwenye balozi tunazotakiwa kuwa na wabobezi wa masuala ya ushirikiano wa kimataifa, tunajaza wabobezi wa masuala ya uhusiano wa kimataifa!
 
Nakubaliana na wewe kwa asilimia kubwa, Tanzania kdg ina mapungufu ktk balozi zetu

Ila kwa Congo kdg ilikua tuzembee ila naona kuna juhudi zinafanyika kuboresha ushirikiano na uhusiano
 
Juzi kati M7 na Tshisekedi wamekubaliana kusafisha waasi huko mashariki. Macroni naye kaahidi kumsaidia kwa kigezo kuwa hao ADF wanamahusiano na ISIS, ni mwanzo mzuri. Kama ulivyosema, EAC na SADC zinaweza saidia kama ilivyoundwa ECOMOG japo kwahili kufanikiwa mnatakiwa wote kuongea lugha moja msije ongeza ukubwa wa tatizo.
 
Hili suala nimewahi uliza humu, kwanini tusiwe na soko huru la chakula EAC? Tungefaidika sana. Mapinduzi ya kilimo hayaletwi na ruzuku bali soko la uhakika na bei nzuri. Leo EAC kuna soko la watu 168mln. Tumepoteza sana hapa. hatuna sababu ya kujifungia, maana, paradoxically, kufunga mipaka huleta njaa kuliko uhakika wa chakula.
 
Tuangalie vizuri..
Nchi wenye misuguano kila siku hakufai .
Adui ana milango mingi ya kupitia...
 
Una akili kuliko serikali nzima ya magufuli combined, kuanzia mawazili mpaka watendaji.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…