msnajo
JF-Expert Member
- Jan 20, 2011
- 3,066
- 1,143
Mkuu ndo maana nimesema kuwa PCCB haina madhara kwa CCM, ina madhara kwa Watanzania wengine tena wadogo kama hao uliwataja. Kazi ni moja, kuikataa tu! Hapo tutaonyesha mshikamano wetu Watanzania. Vinginevyo tuendelee kusindikiza watu huku dunia wma kuangalia wanavyofanikiwa, hasa majirani zetu ambao wengine wametoka vitani miaka michache iliyopita.Sheria ya kuzuia na kupambana na Rushwa imewapa uhuru PCCB kutoa allegation tu za rushwa halafu wakishafanya hivyo, ni juu ya mtuhumiwa kuthibitha kwamba yeye si mla rushwa. Kwa lugha ya kitaalam, Burden of proof kwa makosa ya rushwa iko kwa mtuhumiwa. tujiulize hao PCCB wanashindwa nini kutoa tu allegation halafu watuhumiwa hawa wakathibitishe mahakamani kwamba wao si wala rushwa. Au sheria hii wametungiwa mahakimu na maaskari wa vyeo vya chini?