Tuijadili PCCB: Kwanini tuendelee kuwa nayo? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tuijadili PCCB: Kwanini tuendelee kuwa nayo?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Nsololi, Aug 7, 2009.

 1. N

  Nsololi JF-Expert Member

  #1
  Aug 7, 2009
  Joined: Mar 8, 2007
  Messages: 290
  Likes Received: 34
  Trophy Points: 45
  Je, sheria zetu za kupambana na rushwa haziwaruhusu PCCB kufanya haya ambayo Taasisi ya Kuzuia Rushwa nchini Malawi (ACB) wamejaribu kuyafanya?

  Bila hatua kama hizi ambazo zitasaidia kuweka precedent kwa watu watakaopewa madaraka na kujua nini kinaweza kuwatokea pindi wakifanya madudu yao na kugunduliwa tutafika kweli?

  ============
  Mali za Muluzi zakamatwa Malawi


  TAASISI ya Kuzuia Rushwa nchini Malawi (ACB) imekamata mali za rais wa zamani wa nchi hiyo, Bakili Muluzi, kama dhamana katika kesi ya rushwa inayomkabili.

  Hatua hiyo ya ACB imechukuliwa wakati bado inaendelea na uchunguzi katika kesi hiyo ambayo Muluzi anadaiwa kuingiza kwenye akaunti yake fedha za wafadhili zinazofikia dola za Marekani milioni 11.

  Taasisi hiyo imesema kwamba imekamata jumba analoishi lenye thamani ya mamilioni ya fedha lililoko katika mji wa biashara wa Blantyre. Imesema pia ya kuwa imekamata magari 44 kati ya magari 149 ambayo rais huyo wa zamani wa Malawi anamiliki.

  Vingine vilivyokamatwa ni jumba lake la biashara la Keza Office Park ambalo lilizinduliwa kwa mbwembwe, mgeni mwalikwa wakati huo Rais wa Tanzania, Benjamin Mkapa, na akaunti zake zote za benki.

  Habari zinasema wakati hayo yakiendelea, Muluzi mwenyewe yuko Uingereza kwa matibabu. Ofisa Uhusiano wa ACB, Egrita Ndala, amekaririwa na gazeti la kila siku la Malawi- The Daily Times, akisema taasisi hiyo bado inaendelea na uchunguzi wake.

  "Kikosi cha Kupambana na Rushwa (ACB) bado kinaendelea na uchunguzi wa mali nyingine ili kujiridhisha na umiliki wake. Ni vigumu kwa sasa kusema mali nyingine ambazo zimepangwa kuchukuliwa, " alisema Ndala.

  Katika hatua nyingine, kabla ya tukio hili la wiki hii, hivi karibuni rais huyo wa zamani wa Malawi alizuiwa kusafiri kwenda Uingereza na pasi yake ya kusafiria ikanyang'anywa baada ya kuzuka uvumi kwamba angetorokea Uingereza. Hata hivyo, aliruhusiwa kuondoka kabla ya ACB kuvamia mali zake kama dhamana endapo atashindwa kesi hiyo na hatarejea nchini humo.

  Habari kutoka nchini humo zinasema ya kuwa mwanasheria wa Muluzi, Jai Banda, ameomba zoezi la kukamata mali za Rais huyo lisitishwe. Muluzi aliwahi kukamatwa huko nyuma kwa kwa kesi hiyo hiyo.


  CHANZO: Raia Mwema
   
 2. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #2
  Aug 7, 2009
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 308
  Trophy Points: 180
  We Nsololi,

  Mbona unatusumbua sisi?

  Hujui tuko usingizini, na saa hizi ni usiku?

  Usubiri kuche bana, ndo tutaanza kufanya kazi hiyo!

  Kuna wachache wanataka kusababisha uvunjifu wa amani kwa kelele kama hizo! Hawa si wenzetu, wanatumiwa!

  Lakini kweli jamani...mtu mmoja kumiliki magari 149 ni halali?
  Kula huku kula gani
  Mnakula hata cha Yatima!
   
 3. Buchanan

  Buchanan JF Diamond Member

  #3
  Aug 7, 2009
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 13,203
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  Hapa huelewi nini? Mkapa ajaribu kugombea tena akimchallenge JK kama mali zake hazitaanza kukamatwa kwa kuwa itaaminika ni za kifisadi! Fungua macho uone sababu za kukamatwa kwa mali za Muluzi!
   
 4. Mag3

  Mag3 JF-Expert Member

  #4
  Aug 7, 2009
  Joined: May 31, 2008
  Messages: 9,094
  Likes Received: 6,187
  Trophy Points: 280
  [FONT=&amp]Wanaume kazini - hakuna cha kulindana wala kuoneana haya, shuhudia kwetu Bongo! Mara oh, mwacheni apumzike, mara analindwa na katiba na blah blah - yaani ni aibu tupu.
  [/FONT]
   
 5. Buchanan

  Buchanan JF Diamond Member

  #5
  Aug 7, 2009
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 13,203
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  They are at work to silence the Mutharika's rival Muluzi, who doesnt know African politics?
   
 6. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #6
  Jun 16, 2011
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,448
  Likes Received: 81,661
  Trophy Points: 280
  PCCB: We will not spare anyone in anti-graft war

  By Felister Peter

  16th June 2011

  PCCB Director General Edward Hoseah

  Prevention and Combating of Corruption Bureau (PCCB) Director General Edward Hoseah has said there is nothing to stop them from working on corruption allegations for years levelled against Kagoda Agricultural Company "once we have enough credible evidence in hand".
  The allegations are in connection with the Bank of Tanzania External Payment Arrears Account (EPA) payout scandal.

  "We are not afraid of probing Kagoda. Nobody is above the law. The only problem is lack of evidence," Dr Hoseah said in Dar es Salaam yesterday shortly after the opening of a meeting on corruption.
  He explained that, contrary to popular belief, the bureau deals with all forms of corruption "but the long process involved might make people think we are not doing anything, particularly on cases of grand corruption".

  "We need to have enough credible evidence before taking legal measures against any suspect and, at any rate, it is the courts that have the last word," he added.
  The PCCB chief would not be drawn into citing any specific grand corruption cases the bureau is working on, saying that doing so was unethical. He however noted that Tanzanians are having a better grasp of the impact of corruption in their daily routines and hence playing a bigger role in the war against it.

  Delegates to the meeting meanwhile challenged PCCB to intensify the war against grand culprits.
  Media Owners Association of Tanzania (MOAT) Chairman Reginald Mengi said the government has made a commendable job in the war on the vice but ought to be tougher with the kingpins of grand corruption.

  "In my view, it is difficult to win this war without dealing with the elements behind grand corruption. Once you deal with even just one of them, the others will be scared stiff," he noted, adding that merely reining in bribe takers while bribe givers are off the hook does not help much.

  Mengi explained that grand corruption suspects are filthy rich and sometimes use money to protect themselves "so containing them calls for stern measures and a high degree of accountability on the part of the relevant authorities if corruption rings are to be dismantled".
  He warned that if corruption gets more rampant and vicious, it will turn into some form of national culture and therefore a lot more difficult to tame.

  Civic United Front Deputy Secretary General Julius Mtatiro said PCCB did a recommendable job during the CCM opinion polls last year, including nabbing many people suspected to be bribe givers, "but shockingly it failed to deal with corrupt candidates during the General Election campaigns".
  Tanzania National Business Council Executive Secretary Dunstan Mrutu noted that corruption has made doing business in Tanzania overly costly "since one has to grease several palms before one can start a business".

  Mathias Chikawe, Minister of State in the President's Office (Good Governance), directed all leaders responsible for good governance to make sure that leadership ethics are implemented.
  He issued the order when opening the meeting, also calling on political and religious leaders to combat corruption by talking their followers into at changing their mindset vis-à-vis the vice.
  Meanwhile, Norwegian Ambassador Ingunn Klepsvik said corruption was a major obstacle to meaningful development. She said her country would continue supporting Tanzania in the war on the vice.

  United Nations Development Programme Resident Coordinator Philip Poinsot said winning the war on corruption was a guarantee for society to benefit through improved social services.
  He said the UN has been supporting capacity building training for PCCB staff and police officers and supports the implementation of various other corruption programmes meant at fighting corruption.  SOURCE: THE GUARDIAN   
 7. Steve Dii

  Steve Dii JF-Expert Member

  #7
  Jun 16, 2011
  Joined: Jun 25, 2007
  Messages: 6,416
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  Grrrrrr !!! Fumbling flipping ******!!
   
 8. Steve Dii

  Steve Dii JF-Expert Member

  #8
  Jun 16, 2011
  Joined: Jun 25, 2007
  Messages: 6,416
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  Bila shaka hapo pia kuna posho kubwa imetumika!! Talk talk talk and more talks, year in year out... kisichojulikana kutoka kongamano hilo ni kipi??!!
  Meeting on corruption my loud kinky fart!!
   
 9. Chimunguru

  Chimunguru JF-Expert Member

  #9
  Jun 16, 2011
  Joined: May 3, 2009
  Messages: 9,843
  Likes Received: 270
  Trophy Points: 180
  Kama kuna ofisi inayokula kodi zetu bure basi ni hawa Takukuru, sioni wanafanya kazi gani. Deep green, meremeta, Epa to mention a few lkn kimyaa kama wamemwagiwa maji vile. Siku tukiingia madaraki tutawafungulia mashtaka viongozi wote watendaji wa takukuru!!!!!
   
 10. K

  Kicheruka JF-Expert Member

  #10
  Jun 16, 2011
  Joined: Feb 2, 2009
  Messages: 791
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Hose mwenyewe mla rushwa mkubwa na analinda wala rushwa wakubwa wote huu upuuzi anaongea anafikiri madhambi yake hayajulikani?
   
 11. i

  immasoft Member

  #11
  Jun 16, 2011
  Joined: Mar 2, 2011
  Messages: 96
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 15
  mh mh simo simokabisa
   
 12. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #12
  Jun 16, 2011
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,448
  Likes Received: 81,661
  Trophy Points: 280
  Huyu ni msanii mwingine ambaye alitakiwa awe ameshafukuzwa kazi miaka mingi sana...lakini kama tunavyomjua Kikwete ni muoga mno! anajua dhambi zake hivyo anajua akimfukuza kazi na jamaa akiamua kumchora hadharani basi Ikulu patakuwa hapakaliki.
   
 13. G

  GJ Mwanakatwe JF-Expert Member

  #13
  Jun 16, 2011
  Joined: Mar 26, 2011
  Messages: 241
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Hivi wewe mkurugenzi mkuu mbona unafanya usanii kuhusu rushwa Tanzania? Unasema kwamba huiogopi kagoda, wenye ushahidi nayo wakuletee ushahidi huo waone makali yako, hayo siyo maneno ya kuwazungumzia watz wa leo.

  Wajibu wako ni pamoja na kufanya upelelezi wa tuhuma, wakati unafanya upelelezi ndipo utapata ushahidi, sasa utapataje ushahidi bila kufanya upelelezi? haiwezekani wenye ushahidi wakuletee tu holela bila utaratibu wa kiupelelezi, na wenye ushahidi huo wapo na unawajua ila haujawapa ushirikiano.

  Kwa ujumla kazi hiyo imekushinda, ni busara kama ungeomba kwa aliyekuteua kutoka hapo ili mtz mwingine aje aendeleze mapambano, miye binafsi nimechoka na hadithi zako za kila siku za kusingizia kukosa ushahidi, rushwa inazidi kutokomeza uchumi wa nchi hivyo kuharibu ubora wa maisha yetu, jiuzulu ukafanye kazi nyingine.
   
 14. Amiliki

  Amiliki JF-Expert Member

  #14
  Jun 16, 2011
  Joined: May 6, 2011
  Messages: 2,087
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  Kwa nijuavyo mimi, Ushahidi huwa unatolewa Mahakamani baada ya Mtuhumiwa kupelekwa huko. Sasa huyu Punguani kusema kwamba mpaka apate ushahidi ndio awapeleke Mahakamani maana yake ni nini! Au anajiona yeye ameshakuwa Mahakama kwa hiyo akienda pale awaambie kwamba Ushahidi nilishaletewa kwa hiyo Wafungeni Kagoda!

  Aache Usanii akapopolewe kama jamaa yetu alivyopopolewa na Mwarabu kwenye ule mtandao
   
 15. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #15
  Jun 16, 2011
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  i almost pushed for a ban miself

  hii kauli tumeanza kuisikia tangu enzi za kamazima hadi leo
   
 16. CAMARADERIE

  CAMARADERIE JF-Expert Member

  #16
  Jun 16, 2011
  Joined: Mar 3, 2011
  Messages: 4,427
  Likes Received: 158
  Trophy Points: 160
  PCCB is like a chained dog....bark bark bark no bite bite bite
   
 17. msnajo

  msnajo JF-Expert Member

  #17
  Jun 18, 2011
  Joined: Jan 20, 2011
  Messages: 2,458
  Likes Received: 331
  Trophy Points: 180
  Wadau nawasalimu. Ikiwa imebaki mda mchache kabla ya siku 90 walizopewa wanamagamba wanaotuhumiwa kwa ufisadi kujiondoa wenyewe kwenye chama Cha Magaamba, Najiuliza swali moja,"Nini kazi ya PCCB". Hii ni taasisi ya kupambana na kuzuia rushwa. Tumeshuhudia wazi wale wilotuhumiwa kwa ufisadi ndani ya CCM wakihojiwa na naibu mwkt wa CCM "Pius Msekwa.", tena kwa siri na hakuna kutujuza lolote.

  Kwa nini hii kazi ya kuwahoji hawa mapacha watatu (RACHEL), isingefanywa na PCCB? Imenidhibitishia kuwa PCCB haiwahusu CCM bali Watanzania wengine tena wa hali ya chini! Nikiwa kama Mtanzania, huu ni uozo, tena uvundo ndani ya serikali ya CCM! Tunasubiri siku 90 Ziishe, tuone uamuzi mtakaochukua. Na sitashangaa kuona mmetupotezea, kwani hata Mkuu wa kaya anawafaham wauza unga ila hawataji hata siku moja.

  Wala rushwa pia anawafaham, wahujumu uchumi nao anawajua sio kwa kuambiwa bali kwa kushuhudia! Kazi ni moja, Watanzania tufanye mabadiliko ya kuichimbia kaburi huyu mdudu CCM, atatumaliza tuliopo na watakaokuja! Ni hatari kuliko kimeta, nashangaa tunahangaika na ukimw wakati kuna janga la taifa ambalo ni CCM. Tunaweza kufanikisha uchumi wetu na kuwa na maisha mazuri kama tutaliondoa hili janga la Taifa(CCM)..... Mshikamano wetu utajionyesha hapo tu, kwingine kote ni bla bla... Tuamue na tudhamirie kwa dhati.
   
 18. dazu

  dazu JF-Expert Member

  #18
  Jun 18, 2011
  Joined: Feb 26, 2011
  Messages: 365
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Sheria ya kuzuia na kupambana na Rushwa imewapa uhuru PCCB kutoa allegation tu za rushwa halafu wakishafanya hivyo, ni juu ya mtuhumiwa kuthibitha kwamba yeye si mla rushwa. Kwa lugha ya kitaalam, Burden of proof kwa makosa ya rushwa iko kwa mtuhumiwa. tujiulize hao PCCB wanashindwa nini kutoa tu allegation halafu watuhumiwa hawa wakathibitishe mahakamani kwamba wao si wala rushwa. Au sheria hii wametungiwa mahakimu na maaskari wa vyeo vya chini?
   
 19. Vin Diesel

  Vin Diesel JF Gold Member

  #19
  Jun 18, 2011
  Joined: Mar 1, 2011
  Messages: 8,401
  Likes Received: 736
  Trophy Points: 280
  Hata wale waliokatwa majina kwenye uchaguzi wa bavicha kwa kisingizio cha kutoa rushwa kwa M PESA wapelekwe mahakamani...lazima tuoneshe mfano
   
 20. t

  tambarare Senior Member

  #20
  Jun 18, 2011
  Joined: Mar 1, 2011
  Messages: 148
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  pccb ipo kwa ajiri ya watu wasio na magamba na watu wenye beef na viongozi wa serikali ya magamba ,,,,,,,,victims ni haswa wale wenye kuingilia maslahi ya wenye magamba
   
Loading...