Tuhuma za Ufisadi, Afisa Mtendaji Ajiua huko Iringa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tuhuma za Ufisadi, Afisa Mtendaji Ajiua huko Iringa

Discussion in 'Jukwaa la Sheria (The Law Forum)' started by bagamoyo, Apr 19, 2011.

 1. b

  bagamoyo JF-Expert Member

  #1
  Apr 19, 2011
  Joined: Jan 14, 2010
  Messages: 4,535
  Likes Received: 2,116
  Trophy Points: 280
  BAADA ya wananchi wa kata ya Ruaha katika Halmashauri ya manispaa ya Iringa kumtuhumu kwa ufisadi wa shilingi milioni 24 .6 za maendeleo afisa mtendaji wa kata hiyo Nuhu Feruzi ameamua kujiua kwa kunywa sumu.

  Kaimu mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Manispaa ya Iringa Mashaka Luhamba alimweleza mwandishi wa habari hizi kuwa kifo cha mtendaji huyo kimeacha simanzi kubwa kwa Halmashauri hiyo na kuwa kifo chake kimekuja ikiwa ni siku tano toka uongozi wa halmashauri hiyo kufika katika kata hiyo kushughulikia malumbano kati ya wananchi wa kata hiyo na mtendaji huyo.  Mwanzoni mwa wiki iliyopita Wananchi wa mitaa mbali mbali ya kata ya Ruaha, walivamia ofisi ya mtendaji huyo wakitaka kusomewa mapato na matumizi ya kata yao, jambo ambalo liliwafanya mtendaji wa kata huyo na yo Nuhu Feruzi na Diwani Alphonse Mlagala , kuondoka ofisini pasipo kuwapa taarifa hiyo.

  Wiki iliyopita wananchi wa kata hiyo waliamua kuifunga ofisi ya Afisa mtendaji huyo wakishinikiza kusomewa taarifa ya mapato na matumizi ya fedha za maendeleo huku wakimtuhumu kuwa amefanya ufisadi wa shilingi mil 24.6 za ruzuku, na kodi ya minara ya simu katika kata hiyo

  Hata hivyo ndugu wa marehemu huyo walipofuatwa na mwandishi wa habari hizi ili kuelezea mazingira ya kifo hicho waligoma kuzungumza chochote kwa madai kuwa si wasemaji wa kifo hicho .

  Kaimu afisa mnadhimu wa jeshi la Polisi Mkoani Iringa, Hamfrey Saganya alisema kuwa afisa mtendaji huyo, alikutwa akiwa amekufa chumbani kwake, baada ya kunywa sumu ambayo haijajulikana aina yake, katika maeneo ya Mwangata, Manispaa ya Iringa.(Imeandikwa naFrancis Godwin)
  Source:francisgodwi.blogspot.com na Mjengwa.blogspot.com
   
 2. Quinine

  Quinine JF-Expert Member

  #2
  Apr 19, 2011
  Joined: Jul 26, 2010
  Messages: 10,934
  Likes Received: 12,202
  Trophy Points: 280
  Du!! RA ana roho ngumu.
   
 3. s

  sentimental Member

  #3
  Apr 19, 2011
  Joined: Feb 20, 2011
  Messages: 24
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 3
  Kwa hiyo kaondoka na hela yetu au wananchi watasomewa mapato na matumizi ya hela zao. Isijekua ndio case closed halafu ndugu yake waendelee kupeta na hela aliyochukua.

  Kama ndugu zake wanampenda wasafishe jina la ndugu yao. Wawaachie wananchiwasomewew na kuhakiki mapato na matumizi hayo kama hakuchukua hela basi jina lake liwe clean na kama kuna hela ziliondoka basi ndugu zake wazirudishe. Ndio uungwana huo.

  RIP
   
 4. malkiory

  malkiory JF-Expert Member

  #4
  Apr 19, 2011
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 272
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ndiyo uwajibikaji wenyewe huu, nawapongeza wananchi kwa mwako wa hali ya juu walioonesha kutaka maelezo ya mapato na matumizi ya fedha zao.
   
Loading...