Mikopo ya 10% Kigamboni, shida ipo wapi.?

Mikopo ya 10% Kigamboni, shida ipo wapi.?

Manyasi jr

New Member
Joined
Oct 4, 2026
Posts
1
Reaction score
1
Mikopo ya 10% Wanawake na Vijana Kigamboni tumesainishwa mikataba tangu September lakini mpaka leo hatupewa fedha.
Sisi vikundi vya wanawake na vijana katika halmashauri ya wilaya ya Kigamboni tuliopitishwa kupata mikopo ya 10% ya mapato ya halmashauri tulisaini mkataba wa kupewa mikopo hiyo tangu tarehe 10 September 2026, kati ya Vikundi husika ( mkopaji) na Halmashauri ya wilaya ya kigamboni ( Mkopeshaji), mkataba pia unaeleza mkopaji anatakiwa kuanza marejesho baada ya grace period ya miezi mitatu.
Cha kushangaza ni kwamba Sasa hivi ni mwezi umepita fedha hazijaingiwa ktk account zetu, na tukiingia kwenye mfumo inaonekana mpaka mkurugenzi mtendaji ameshapitisha tupewe huo mkopo. Tatizo lipo kwa DT yeye hajapitisha, Sasa hatujui DT amegoma kupitisha au la, hakuna taarifa yoyote tuliyopewa na kumekuwa na ukimya mkubwa sana.
Kumbuka sisi ni intake ya Juni- September 2026
Tukiwauliza maafisa maendeleo wa kata zetu wanatuambia wao wameshamaliza sehemu yao, kulipobaki ni huko manispaa.
Tunaomba mkurugenzi mtendaji Kigamboni atuelezee shida ni nini..?
 
Back
Top Bottom