Tuhuma nzito za ufisadi dhidi ya Mwakyembe pale ATC

Tuhuma nzito za ufisadi dhidi ya Mwakyembe pale ATC

Status
Not open for further replies.
Nimepanda hii ndege inayotuhumia jana tu, from Dar to....! ukweli management ya ATC ime change sana, wapo very serious na biashara, wahudumu ni wazuri na wapo committed hasa, kabla ya uzi huu kubandikwa, kwasababu na mimi ni mTanzania nilifanya mahesabu yafuatayo:-
Trip moja from Dar to Mwanza ni Tsh 166,000/= kwa abiria anaenda one trip only, lakini kwa wale wanaokata go and return Mwanza to Dar ni Tsh 257,000/= well, let us just assume kwamba abiria wote ni wa go and return, of course nia hapa ni kua na hesabu ambayo ni most minimum, kama kila Trip ndege itabeba abiria 50 tu it mean kwa trip moja ndege hiyo itakua imetengeneza pesa hizi, chukua nusu ya hiyo 257,000/= gawanya kwa 2 itakupa 128500/= then kwa hao abiria 50 itakupa 6425000/= ndege hii hufanya safari sita kwenda na kurudi Mwanza, yaani asubuhi ya saa 12 to Mwanza, then saa 2 to Dar, kisha saa za mchana to Mwanza again, machana huo huo hurudi Dar tena then saa 11 jioni inatia timu Mwanza while mbili usiku inarudi Dar, weka hesabu hiyo mara sita yaani 6425000 kwa 6 sawa 38,550,000/= sasa hiyo ni pesa ya siku moja, weka kwa hiyo miezi 3 ya ukodishwaji, assuming mwezi utakua na siku 90 then jumla ya pesa kama Gross itakazo zipata ATC kwa deal hili ni Tsh 3,469,500,000/= mbona hili deal linalipa sana tu, anyway twende kwenye hiyo bill ya mwezi ya USD 200,000, kama exchange rate ni 1=1550 then USD 200,000 ni sawa 310000000/= wakati siku moja umelala na Tsh 38550000, kumbukeni pia, Distance from Mwanza to Dar kwa ndege ni Km 450 tu, Mmmm, wakuu, tuache majungu, Mwakyembe ameweka dira, hata bei za Precion naona kama zimeshuka hivi, i think because of compitetion!

Asante mkuu,mleta uzi nadhani ana matatizo binafsi na Mwakyembe!
 
  • Thanks
Reactions: MTK
Mimi nadhani huyu mleta mada hii ndiyo maadui wa maendeleo ya tanzania. Hili siyo suala la kisiasa ni suala la utalaam zaidi. Hata ilivyoandikwa na wanaotuhumiwa inaonekana wazi ni wale waziba mianya ya wizi wa rasilimali za watanzania wachache. Ndiyo hawa hawa wanaipinga usafari wa train dar es salaam kwa madai eti wamekopa fedha benki kufanya biashara hivyo kwa ajili ya mikopo yao tusitafute suluu ya matatizo ya usafiri dar hadi walipe madeni yao benki na kutunyonya.

Mwakyembe endeleza hiyo vita hadi kieleweke. Maana inaonekana tayari watu wameanza kuhemea mipira. Lazima tuwazike.
 
[Ndugu yangu chuki hazilipi, badala yake unajitafutia laana bure. Kweli wewe unamsingizia huyo baba wa watu MWAKYEMBE wakati ameshajitolea muhanga kila Mtu anaona! Hapa Wizarani ni nani asiyejua kuwa Mweakyembe ndiye Waziri pekee aliyethubutu kakata ulaji wa haya majizi?, OMBA RADHI NA UTUBU Mungu huenda akakusamehe]



Ni mkanganyiko fulani wa mawazo!

Mleta mada anaonyesha mweelewa kidogo sana wa mambo ya usalama wa anga,Umri wa ndege haupimwi kwa muda iliotengenezwa tuu, bali masaa ya kuruka .

Pia mwenye chuki binafsi na Mwakyembe, Amezidi kujikanyaga hasa alipomuhusisha CAG.Namshauri kwanza atatue mgogoro wake wa ndani ili aweze kuweka mtiririko unaoeleweka. Atenganishe tuhuma, chuki binafsi na majungu.

Pia ajifunze na kupokea ushauri kwamba uropokaji hadharani siyo njia muafaka ya kuwakilisha ujumbe.

Tunataka data!!
:glasses-nerdy:
 
Mbona tunakimbilia kumhukumu kwa ufisadi badala ya kuelezea tatizo? Sidhani Kama ni swala la ufisadi ila ni jinsi maamuzi yalivyochukuliwa. Sio I dalili za ushiriki wa wataalam (competent) katika uandaaji wa mkataba na maamuzi ya aina ya ndege. Ki ukweli hiyo ni ndege ambayo haiwezi kushindana hata na ATR za precision kwa ufanisi kwani gharama zake za uendeshaji zitakuwa juu na Itaigharim sana Serikali kiuendeshaji. Kwa hilo la matengenezo na aina ya mkataba (wet lease), nadhani haikuwa lazima kuingia mkataba wa aina hiyo ukitilia maanani uwezo wa pilots na maintenance facilities/technicians (up to check B kama sikosei) wa ATC kwa ndege ya aina hiyo. Mh. Waziri alikuwa na nia nzuri ila maamuzi ndio questionable! Ajitahidi sana Kutumia wataalam hata kama ni nje ya mfumo wake rasmi kama anauona kuwa unamashaka kiutendaji na kiuwezo - huwa hawachelewi kumchomekea.
 
Umekurupuka kutoa tuhuma kwa Ofisi ya taifa ya ukaguzi , Suala la ukodishaji wa ndege chakavu CAG kapiga kelele sana, rejea taarifa yake kuhusu ukaguzi wa mashirika ya umma kwa mwaka wa fedha unaoishia juni 30, 2010 amebainisha kuwa , kuhusu atcl, serikali itafakari upya juu ya shirika ila tube wavumilivu katika kipindi hiki atcl inajaribu kufufuka, haya mengine unayotuambia Leo hatuyaamini kwa sababu wengine nyie mnaweza kuwa mawakala wa washindani wa atcl yani precision nk.

Kaka hajakurupuka anajaribu kujustfy imprest aliyopewa na vidume kuwa kaifanyia kazi!!!
 
Sijaona la maana toka kwa muanzisha mada!
Mwakyembe ni mzalendo wa taifa hili,anastahili pongezi za dhati.
 
Nimepanda hii ndege inayotuhumia jana tu, from Dar to....! ukweli management ya ATC ime change sana, wapo very serious na biashara, wahudumu ni wazuri na wapo committed hasa, kabla ya uzi huu kubandikwa, kwasababu na mimi ni mTanzania nilifanya mahesabu yafuatayo:-

Trip moja from Dar to Mwanza ni Tsh 166,000/= kwa abiria anaenda one trip only, lakini kwa wale wanaokata go and return Mwanza to Dar ni Tsh 257,000/= well, let us just assume kwamba abiria wote ni wa go and return, of course nia hapa ni kua na hesabu ambayo ni most minimum, kama kila Trip ndege itabeba abiria 50 tu it mean kwa trip moja ndege hiyo itakua imetengeneza pesa hizi.

Chukua nusu ya hiyo 257,000/= gawanya kwa 2 itakupa 128500/= then kwa hao abiria 50 itakupa 6425000/= ndege hii hufanya safari sita kwenda na kurudi Mwanza, yaani asubuhi ya saa 12 to Mwanza, then saa 2 to Dar, kisha saa za mchana to Mwanza again, machana huo huo hurudi Dar tena then saa 11 jioni inatia timu Mwanza while mbili usiku inarudi Dar, weka hesabu hiyo mara sita yaani 6425000 kwa 6 sawa 38,550,000/= sasa hiyo ni pesa ya siku moja, weka kwa hiyo miezi 3 ya ukodishwaji, assuming mwezi utakua na siku 90 then jumla ya pesa kama Gross itakazo zipata ATC kwa deal hili ni Tsh 3,469,500,000/= mbona hili deal linalipa sana tu, anyway twende kwenye hiyo bill ya mwezi ya USD 200,000, kama exchange rate ni 1=1550 then USD 200,000 ni sawa 310000000/= wakati siku moja umelala na Tsh 38550000, kumbukeni pia, Distance from Mwanza to Dar kwa ndege ni Km 450 tu.

Mmmm, wakuu, tuache majungu, Mwakyembe ameweka dira, hata bei za Precion naona kama zimeshuka hivi, i think because of compitetion!
upo sahihi kabisa ndugu yangu, majungu yote haya ni ya watu wa precision na lengo lao ni kuona ATCL hairushi ndege ili wao wapate super profit kwa kujipangia bei nna wanaringa kweli kweli, tuache majungu tuiache menejimenti ya ATCL wafanye kazi ili watanzania wasione usafiri wa ndege kama luxury na wautumie kwa bei rahisi.
 
Inavyoonekana Kambi ya Lowasa imeanza kazi yake dhidi ya Mwakyembe.
 
Dr-Harrison-Mwakyembe.jpg


Mimi katika vitu vilivyonishinda humu ni mabishani ya nani zaidi kati ya CCM na CHADEMA. Sasa nimeona bora nikufahamisheni Mwakyembe ambaye anajisifia kuwa mpinga rushwa mkubwa alivyokuwa fisadi na ushaidi wote nauweka hapa na kama kuna mtu anabisha aendelee.


Kwa kifupi wafuatao wanahusika kwenye huu wizi:

HARRISON MWAKYEMBE
MANAGEMENT NZIMA YA ATC
BODI YA ATC
KAMATI YA BUNGE YA MASHIRIKA YA UMMA
EXTERNAL AUDITORS WA ATC
LUDOVICK UTUOH AMBAYE NI MKAGUZI MKUU WA SERIKALI



Tuhuma zenyewe ni kama ifuatavyo:

1. Shirika la ndege la taifa (AIR TANZANIA) waliamua kukodisha ndege yenye umri wa miaka 32 aina ya B737-200 iliyozeeka na mbovu kutoka kampuni ya Africa Kusini inayoitwa Star Air Cargo.


2. Ndege hii ilianza kufanya kazi mwaka 1980 kule UK, na ilikuwa inatumiwa na kampuni inayoitwa BRITISH AIRTOURS na baada ya hapo ilikodishwa na mashirika zaidi ya 20 Ulaya na Latin America.

3. Mwakyembe, Menejimenti na bodi mpya ya ATC walikubali na kupitisha ukodishaji wa hii ndege kwa kiasi cha dola laki 2 (200.000 US Dollars) kwa mwezi katika miezi 3 ya awali ya ukodishaji kinyume na ushauri ambao Mwakyembe na maswahiba zake wa ATC walipewa.

4. Mkataba unaonyesha kuwa itabidi ndege hii itabidi iruke kwa masaa 150 kwa mwezi at a rate of 1.350 US Dollars for each hour.

5. Mkataba unaendelea kusema kuwa ATC LAZIMA wagharimie gharamza zote za ma crew ambayo iko estimated to be in the region of a further $80 – $100 PER DAY & PER INDIVIDUAL !

(Katika mazingira ya kawaida msomaji utaona gharama ni ndogo lakini ukweli ni kubwa sana uzingatia kuwa ndege yeneyewe inasafiri kwenda sehem 3 tuu yaani kati ya Dar es Salaam – Kilimanjaro – Mwanza na hii yoye iko funded na walipakodi wa Tanzania).

Sasa ukweli ni kuwa kama kweli Mwakyembe & kundi lake wana nia nzuri wasingekubali dili hii ipitishwe kwa kuzingatia kuwa kwanza ndege inge cost less kuikodisha kuliko gharama ambazo hawa mafisadi wamepitisha, na pia hizi gharama za malipo kwa saa ni kubwa mno na hapa ndipo Mwakwembe na kundi lake la mafisadi wanakula zaidi kwenye huu mgao.

Suala lingine la kuzingatia hapa ni operating costs ambazo Mwakyembe & his crew wa ATC ni uhuni mtupu kwani ndege ina miaka 32 na gharama za uendeshaji na hasa za matumizi ya mafuta ni kubwa mno ukilinganisha ndege za kisasa.

Kwa msiojua ni kuwa gharama za mafuta (fuel costs) kwa kawaida zinachukua around 40% ya overall costs lakini kama shirika linatumia ndege za kizamani basi ni wazi kuwa gharama zitaongezeka zaidi. Na uhuni uliofanywa na ATC wakishirikiana na wahuni wenzao pale wizarani kwa Mwakwembe ni kupiga rangi hizi ndege wakati wakijua wazi kuwa walipa kodi wanataka kujua mikataba iko kwa maslahi ya taifa (NATIONAL INTEREST).

Moja kati ya maswali ya kujiuliza ni kwa nini Mwakyembe na ATC walikataa kuchukua ndege kama CRJ ambazo ni ndogo zaidi lakini zina fly economically lakini pia ni kubwa kiasi kiasi cha kurestart hii biashara ya shirika kama ATC. Lakini hii pia ni mfululizo wa uhuni unaoendelea kama ule wa awali wa kukodisha ndege toka kampuni ya Arabuni ambayo intugharimu sana sisi walipa kodi kama ile ya uhuni wa awali wa ukodishaji wa Airbus.

Sasa huyu Mwakyembe ambaye anajifanya ni kinara wa kupiga vita ufisadi anakubali na amepitisha huu uhuni wa ATC ambao utamgharimu zaidi mlipa kodi. Huu ni uthibitisho kuwa wanaolack vision si wale wa (Pemba + Zimbabwe ) pekee lakini mpaka huyu mwanasheria kama Mwakyembe ambaye anaendeleza uhuni wa stop gap measures.

Sasa kaeni mkao wa kuona wanaleta maombi ya kutaka wapewe pesa zaidi ili waendelee kula. Na news zilizopo kwenye corridor za ATC ni kuwa wana haha kama mbwa mwitu ili warejeshe safari za nairobi na hasa baada ya player mpya chini ya Shirika la ndege la Kenya (FAST JET) kuingia kwenye soko.

BTW

Nadhani mnaikumbuka ile ndege ya ATC iliyoanguka kule mwanza? bas ndio model hiyo hiyo aina ya B737-200 kama hii mbovu na iliyozeeka ambayo Mwakyembe & his crew wanatuleta.


huyu mleta hoja anaonyesha anauhasma na huyu mpiganaji,Mwakyembe endelea kupiga kazi sisi wananchi tupo pamoja na wewe.
 
hahaha nadhani we utakuwa una fanya kazi bandarini sasa unaogopa
 
Muda wa watanzania kuumizwa vichwa na hawa wajinga wa ccm na mitandao yao umekwisha
hatuna muda na conflict zenu,uamuzi wetu ni kuchukua hili dude ccm zimazima na kuliweka pembeni
mkaendeleze hiyo mivutano yenu huko porini si kwenye taifa letu.
 
Unataka ndege ikodiwe Tsh 300,000/= kama coaster ya harusi? Hakuna kitu km hicho. Kubadili rangi hujui km ni janja ya kukwepa madeni ya atcl ili ndege hii isikamatwe na wadaiaji
 
Muda wa watanzania kuumizwa vichwa na hawa wajinga wa ccm na mitandao yao umekwisha
hatuna muda na conflict zenu,uamuzi wetu ni kuchukua hili dude ccm zimazima na kuliweka pembeni
mkaendeleze hiyo mivutano yenu huko porini si kwenye taifa letu.

Mgogoro meya wa jiji la mwanza ulikuwa unashabikia upande upi
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom