Ubarikiwe sana, naamini wengi tutafaidika nimechukua namba, wanajamii Forum jamani si tungechagua mmoja wetu awe coordinator hapa tujiorodheshe na tuanze darasa mara moja?Mimi ni mtunzi wa kitabu cha mbinu za biashara na maarifa ya kupata pesa na utajiri. Pia ni mshauri wa biashara, ninatoa ushauri wa biashara na kuendesha mafunzo ya ujasiriamali, kuandaa michanganuo kuombea mikopo benki na misaada kutoka kwa wafadhili. Mwaka 2009 niliwezesha wateja wangu kupata mikopo ya Tshs. milioni 300 toka mabenki mbali mbali, niliendesha mafunzo na kutoa ushauri kwa watu mbali mbali, Kati ya mafunzo ambayo niliyafanya na yakafana ni yale ambayo yaliandaliwa na Mwang'amba Communication na kufanyika Millenium tower, ambapo wawezeshaji tulikuwa mimi( Charles Nazi) James Mwangamba, Eric Shigongo, Martin Kaswahili, Mr Msemwa na Chris Mauki.
Utafiti nilioufanya nimegundua kwamba watu wengi wanakwama kuendesha biashara zao au kupata maendeleo ya kiuchumi kwa sababu ya kukosa maarifa ya ujasiriamali.Kwa hiyo nimeamua kuwa lengo langu ni kutoa elimu ya ujasiriamali kwa watanzania wote. Kutokana na wito wa mwenzetu natoa ofa kwa Wana JF ambao wako Dar kuwa niko tayali kutoa mafunzo ya ujasiriamali bila malipo yoyote. Nauomba uongozi wa JF usaidie kutafuta ukumbi. Kwa mawasiliano zaidi kwa wanaohitaji kupata mafunzo hayo na uongozi wa JF wanaweza kunipigia simu namba 0755394701. Pia kama una kikundi cha watu ambao wanahitaji kupata mafunzo mnaweza kuniita niko tayali kutoa mafunzo bila malipo mradi mniandalie mahali pa kukutana na muwe idadi isiyokuwa chini ya watu 10.
CHARLES NAZI
Mshauri wa biashara na Mtunzi wa kitabu cha Mbinu za biashara
Ningekuwa DSM ningefanya hii kazi lakini kwa sasa niko nje ya jiji. Ambaye anafikiri anaweza kufanya hili please ajitokeze na kutoa mrejesho hapa na kuwa anawasiliana na Babalao moja kwa moja kwa namba ya simu aliyotoa.Ubarikiwe sana, naamini wengi tutafaidika nimechukua namba, wanajamii Forum jamani si tungechagua mmoja wetu awe coordinator hapa tujiorodheshe na tuanze darasa mara moja?
Nashukuru kwa wale wote wanaoendelea kuchangia mada.
Kwa mfano mtu mmoja ana kiwanja maeneo ya Bunju na hana uwezo wa kujenga kwa sasa kutokana na ufinyu wa mshahara anaolipwa lakini benki ana shilingi milioni moja. Amekaa na kufikiria kuwa ni bora akafungua kituo cha kufyetulia tofali na kuuza sementi hapo lakini ukumbuke benki ana shilingi milioni moja tu na kazini kwake hawadhamini wafanyakazi kuchukua mikopo benki kwa kutumia jina la kampuni. Na ukumbuke kuwa kuna mahitaji mengi ili kuweza kuanzisha kituo hicho cha kufyetulia tofali mbali na kiwanja ambacho tayari kipo. Mahitaji mengine yanayotakiwa na yeye hana ni kama vile kontena au servant quatre, materials kama sementi, mapipa ya maji, pamoja na wafyetua matofali ambao watahitaji fedha za kuwalipa wakati kazi inaanza pamoja na mahitaji mengine madogo madogo.
Je hii ni biashara au ujasiriamali kwa mujibu wa maelezo ya Who Cares?
Je atafanyaje hili aweze kuianzisha kazi hii anayotaka kuanza kuifanya?
Am a farmer cum civil servant . Nafuga nguruwe kwa kwenda mbele, Kuku wa kienyeji, migomba ya kisasa etc. Then nimeajiriwa, nalipwa sh. 280,000 kwa mwezi mzima. Nikiuza mayai napata 300,000. Nikiuza Kitimoto moja tu kwa mwezi napata 200,000-300,000 kuendana na uzito.
Nikiuza kuku 50 tu kwa mwezi napata 200,000.00. Nyumbani nina mahindi gunia 5 , mchele , na maharage. Mama analima mboga mboga ,na midizi. So cost of foods kwangu ni negligible.
Nina watoto wawili wa primary school na madogo wawili relatives secondary ya private.
Ninaendesha pickup na starlet. Ila nina mpango wa kununua lililobora zaidi kifamilia.
Jumla minimum ni napata 700,000. mazimum 1,500,000.
Zile 280,000 nawalipa wafanyakazi wawili kila m2 140,000 na wako very happy. Shamba nilinunua eka moja u nusu miaka hiyooo na ndipo nimejenga ikulu yangu. Here I am . Mjasiriamali/ civil servant.
.UJASIRIAMALI...unahitaji extra senses...creativity in business....an inborn touch of doing things in a different But EFFECTIVE WAY....
tunayo safari ndefu ya kwenda kuwa wajasiriamali wa kweli..ila tusikate tamaa..tutafika..
mjasiriamali kisha unakuwa...soo easier said than...
kuwe na siku maalum ya kuwasilisha ili wadau wote tuweze kujua kwama leo kuna somo ukumbini.
Huyo ni mjasiriamali. Kitendo cha kugundua kwamba kiwanja ambacho hawezi kukiendeleza kwa sasa kwa kukosa fedha bali anaweza kukitumia kupata fedha kinamweka kwenye kundi la wajasiliamari.
Mjasiliamari ni mtu anayeweza kuona fursa za kutengeneza pesa pale ambapo wengine hawaoni. Na ndio maana mfano Dar kuna biashara nyingi sana za kuigana. Wafanyabiasha wengi wa Dar (sio wajasiliamari) wana madala dala, hair saloon za kike na kiume (barber shop), baa za kitimoto na bia na migahawa!
Huyo mwenye kiwanja cha kwake, na mtaji wa shilingi milioni moja tayari ana mtaji mkubwa kuliko anavyofikiria. Tatizo lake anaona kwamba hizo milioni moja ni kidogo sana kwa hiyo hawezi kuanzisha hiyo biashara. Pia ana mawazo ya kwenda kukopa benki.
Mjasiliamari halisi huwa anaanza na mtaji sifuri na haendekezi mambo ya mikopo. Kama ameweza kujikusanyia shilingi milioni moja kama ''saving'' pamoja na kiwanja bila kukopa, ipo siku atajikuta ana Shs. milioni mia moja na kiwanda cha simenti bila mkopo! Achotakiwa kufanya kuendeleza kanuni zake za kujikusanyia mapato, kujiwekea akiba na kufirikia fursa nyingine za kujiongezea kipato.
Looser always say it is possible but it is very difficult, where as winners always say it is difficult but it is possible.
please naomba hili wazo/ombi liende hata kwa mwingine yeyote mwenye kuweza kutoa elimu hii hapa hapa JFMimi nilikuwa na wazo ambalo nahisi litatusaidia wote sisi tulio nje ya DSM na nyie mlio DSM. Wazo hili ni la kumuomba babalao pamoja na kutoa offer ya kutoa mafunzo kwa watu kumi (10) nilikuwa namuomba awe anatoa mada hapa kwenye thread hii kwani inaonekana ndio sehemu ambayo watu walioko sehemu mbalimbali wanaweza kufaidika zaidi. Sijapinga wazo la kutoa elimu kwa wale walioko DSM ila nimejaribu kuangalia jinsi ambavyo huyu mtaalamu wa masuala ya ujasiriamali anaweza kusaidia watu wengi zaidi. Sijui wezangu mnaonaje wazo hili. Kama limekaa vizuri tumsisitizie babalao hta kwa PM
If you can't make money without money, you can't make money with money. Period!
Heshima sana mkuu, hili nalo neno. Lakini pia wadau wanasema vitu ambavyo wewe ni mteja (ambavyo hutumia sehemu kubwa ya kipato chako) yaweza kuwa sehemu ya ubunifu unapofikiria kuanzisha biashara. Kielelezo ukiwa wewe mwenyewe.jamaniiiiii...mjasiriamali haitaji MTAJI....kwa maana ya PESA...mjasiriamali anaitaji MTAJI WA AKILI NA UBUNIFU ULIO TOFAUTI NA WENGI KATIKA MAZINGIRA YALIYOMZUNGUKA...
1-akili/wazo
2-Ubunifu tofauti
3-Mazingira yaliyomzunguka
Hivi ni vitu muhimu sana kwa mjasiriamali wa kweli..baada ya hapo...vitu kama PESA ndipo hufuata ili kuliwezesha (lile wazo lilojaa ubunifu tofauti katika mazingira yalokuzunguka)liwe la kweli...
Natoa changamoto kwa wadau..jaribu kujiba mazoezi ya say unaishi sinza..kila nyumba imejaa baa na guest house na kitimoto, fastfood, boutique etc...jiulize unachoweza kufanya katika hizo biashara wanazoigana ukaweza KUSIMAMA kidedea na tofauti na wao then ukaouza au kuingiza pesa kuliko wao...hapa ndipo napoongelea mtaji wa AKILI...sio pesa