Kumekuwa na ongezeko la watu wanaotaka kujua ni jinsi gani ya kujiajiri wenyewe, namaanisha kama mtu mmoja au kama kikundi. Naomba tutumie andiko hili hapa kufundishana ni jinsi gani, mbinu zipi, njia zipi tunaweza kutumia katika kujitegemea wenyewe pasipo kutegemea mishahara na kazi za kuajiriwa ambazo kadri dunia inavyosonga mbele ndio jinsi ambavyo kazi hizi zinakwisha. Kila mwenye wazo au uzoefu aweke hapa kwa jinsi ajuavyo yeye ilimradi ujumbe ufike kwa jamii kubwa zaidi.
Moderator naomba utilie mkazo hili na ikiwezekana tukutanisheni na wataalam na walio nautaalam hapa naomba wajitolee; mfano mimi niko tayari kusaidia ama kushauri kwenye upande wa IT na mambo ya Internet cafe
Kitu cha kwanza ninachoweza kuchangia ktk suala la ujasiriamali kwa ujumla, la kwanza ni kujitambua wewe mwenyewe na mazingira yako uliyo nayo ( vipaji,rasilimali,ujuzi,fursa nk). Na la pili ni juhudi ktk kujifunza toka kwa waliofanikiwa na kushirikiana nao.
Mshauri wa biashara na Mtunzi wa kitabu cha Mbinu za biashara
Mimi ni mtunzi wa kitabu cha mbinu za biashara na maarifa ya kupata pesa na utajiri. Pia ni mshauri wa biashara, ninatoa ushauri wa biashara na kuendesha mafunzo ya ujasiriamali, kuandaa michanganuo kuombea mikopo benki na misaada kutoka kwa wafadhili. Mwaka 2009 niliwezesha wateja wangu kupata mikopo ya Tshs. milioni 300 toka mabenki mbali mbali, niliendesha mafunzo na kutoa ushauri kwa watu mbali mbali, Kati ya mafunzo ambayo niliyafanya na yakafana ni yale ambayo yaliandaliwa na Mwang'amba Communication na kufanyika Millenium tower, ambapo wawezeshaji tulikuwa mimi( Charles Nazi) James Mwangamba, Eric Shigongo, Martin Kaswahili, Mr Msemwa na Chris Mauki.
Utafiti nilioufanya nimegundua kwamba watu wengi wanakwama kuendesha biashara zao au kupata maendeleo ya kiuchumi kwa sababu ya kukosa maarifa ya ujasiriamali.Kwa hiyo nimeamua kuwa lengo langu ni kutoa elimu ya ujasiriamali kwa watanzania wote. Kutokana na wito wa mwenzetu natoa ofa kwa Wana JF ambao wako Dar kuwa niko tayali kutoa mafunzo ya ujasiriamali bila malipo yoyote. Nauomba uongozi wa JF usaidie kutafuta ukumbi. Kwa mawasiliano zaidi kwa wanaohitaji kupata mafunzo hayo na uongozi wa JF wanaweza kunipigia simu namba 0755394701. Pia kama una kikundi cha watu ambao wanahitaji kupata mafunzo mnaweza kuniita niko tayali kutoa mafunzo bila malipo mradi mniandalie mahali pa kukutana na muwe idadi isiyokuwa chini ya watu 10.
CHARLES NAZI
Mshauri wa biashara na Mtunzi wa kitabu cha Mbinu za biashara
Babalao,
Hongera kwa kazi yako nzuri. Nashauri pia uongee na TBC ili kuwe na kipindi cha Ujasiriamali kila wiki kwa angalau saa mbili kwa wiki kupitia Televisheni na Radio. Kipindi hiki kinaweza kuwa chini ya JF ila wewe ukawa ndiyo mzungumzaji na muelimishaji mkuu.
wakuu hapa mie nina dokezo la msingi kabsaaa..katika watu 100 wanaoongelea ujasiriamali 99 ni wafanya biashara na 1 ndio mjasiria mali...sasa lazma tujue kuna tofauti ya wafanyabiashara na wajasiriamali.....
Anayenunua nyanya kariakoo tsh. 100 na kuja kupanga gengeni kwake manzese na kuuza tsh. 120..huyu ni mfanya biashara...sawa na wanaokwenda china/dubai/honkong/thailand....MJASIRIAMALI..huyu anatakiwa awe na jicho la ziada la kuona nafasi/fursa zaidi za kutengeneza pesa..na sio kununua na kuuza tuu...say..mjasiriamali atanunua nyanya kariakoo..atazi-preserve zizioze..kisha atazipack vizuri na kuzitia logo yake kisha ataziuza kempinski..na nyingine atasafirisha kwenda nje ya nchi...zilizoanza kuoza pale kariakoo..mjasiriamali atazinunua na kuzitengeneza sauces mbalimbali na kuuza..
ANAKUWA ANA-ADD VALUE before selling..na kwa kuadd value anauza/anapata value for money...ni maoni tuu wadau
..MJASIRIAMALI..huyu anatakiwa awe na jicho la ziada la kuona nafasi/fursa zaidi za kutengeneza pesa..na sio kununua na kuuza tuu...say..mjasiriamali atanunua nyanya kariakoo..atazi-preserve zizioze..kisha atazipack vizuri na kuzitia logo yake kisha ataziuza kempinski..na nyingine atasafirisha kwenda nje ya nchi...zilizoanza kuoza pale kariakoo..mjasiriamali atazinunua na kuzitengeneza sauces mbalimbali na kuuza..
ANAKUWA ANA-ADD VALUE before selling..na kwa kuadd value anauza/anapata value for money...ni maoni tuu wadau
Kwa mapoint ka aya; nashauri ubadili jina kwenda I care tih tih tih tih