Tufanye kazi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tufanye kazi

Discussion in 'JF Chit-Chat' started by JIKO LA SHAMBA, Aug 14, 2011.

 1. J

  JIKO LA SHAMBA Member

  #1
  Aug 14, 2011
  Joined: Apr 21, 2011
  Messages: 7
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  Matukio yanayotokea sasa katika nchi yetu ni mchanganyiko wa mambo mengi na la msingi zaidi nionalo
  kwetu sisis watanzania kulalamika kwamba hali ngumu na viongozi hawawajibiki. Ok yawezekana kweli hawawajibiki wanakula rushwa au
  wanajali maslahi yao kuliko ya nchi yao na wananchi wao.
  Sasa wananchi sisi tunaolalamikia kila kitu tunawajibika vipi? Utakuta mtu yupo mitaani badala ya kuwa kwenye meza yake saa za kazi na
  wakati mwingine mtu yuko kazini lakini yupo kwa sababu yupo hafanyi kazi ipaswavyo ni soga tu na matokeo yake kazi zinarundikana
  hazimaliziki on time! mwisho wa siku kunakuwa kuna viporo na mwisho wa yote tunaingiza hasara katika makampuni na mashirika.
  Tufanyeni kazi tuche kulalamikia kila kitu bila kazi uchumi wetu utakuwaje na maisha bora yanapatikanaje bila kukuza uchumi?
   
 2. Mwendabure

  Mwendabure JF-Expert Member

  #2
  Aug 16, 2011
  Joined: Mar 10, 2011
  Messages: 2,056
  Likes Received: 296
  Trophy Points: 180
  <br />
  <br />
  Ni wazi Mkuu we upo ktk siasa! Kwa uzowefu wangu hoja muflisi kama hii yako huwa inatolewa na kundi hilo. Vinginevyo ungeungana na watanzania wenzio wengi kulia na kupiga yowe la maisha kuwa magumu. Ni wanafanya siasa peke yao ndo hawaisikii sauti ya walio wengi kuwa hali ya maisha ni ngumu kwa walio wengi.
  Acha kutukana wavuja jasho na watanzania wenzako mkuu!
   
Loading...