Hahaha. . Hygea sio nyie wanaume ndo mnapenda kulalia nyama choma na bia alafu wali wa samaki nyumbani mnaona sio kitu? Binafsi nasikitika sana kuona watu wanakimbia vyakula vizuri na fresh vyote tulivyobahatika kuwa navyo alafu wanajaza vitu visivyo vizuri sana kwa afya ya mwili. Yani mimi ningeweza ningekua nakula mboga za majani asubuhi, mchana na jioni. Kitu ambacho wengi hawataki, wao ni nyama, nyama, nyama tuu basi.
Nyie wanaume nanyi kuweni responsible. . .
Kama tatizo ni chakula cha nyumbani hakinogi basi ongea na mkeo aboreshe mapishi yake, omba upikiwe vyakula (vya maana) upendavyo na ujitahidi kuwa hata unatembea kidogo mida ya jioni. Unaweza ukafanya iwe family activity, mama na watoto wote mnaungana. Kama mna kauwanja kenu chezeni hata mpira na watoto wenu.
Sema hayo hapo juu yanahusu yu iwapo wewe ni mtu wa familia, kama hupendi kutumia muda na familia yako endelea tu kujaza nyama/ndizi kavu na ngumu pia machips yaliyojaa mafuta tumboni day in day out. Matokeo yake utayaona soon enough.
Hehehe ndio na somo linahusu, yale nayo ni mazoezi!!