Epuka kula junk foods na vyakula vingi vya supermarkets (vingi ni GMOs ambazo zina madhara sana kwa afya ya mwanadamu).
Tumia karanga mbichi,asali,maziwa ya mgando,matunda,mboga za majani,karoti et al. katika milo yako yote.
Epuka kula vyakula vyenye mafuta mengi (haswa vyenye mafuta ya kutokana na wanyama). Ukiweza tumia sunflower oil na vizuri kabisa,tumia olive oil.
Epuka kula read meat sana,nyama ya ng'ombe na mbuzi sana. Ni heri nyama nyekundu ya pori kuliko hizo. Tumia white meat kama mbadala. Ila husiendekeze sana nyama hata hiyo nyeupe!
La msingi zaidi fanya mazoezi (ukiweza kila siku,angalau kwa nusu saa). Unaweza fanya aidha asubuhi kabla ya kwenda kwenye mihangaiko au jioni baada ya kutoka kwenye mihangaiko.
Naelewa watu wa DSM watasema hawana muda kutokana na kuamka kwao saa 10 za usiku kuwahi foleni,na kurudi nyumbani saa 4 za usiku kutokana na foleni.
Sawa,lakini kuna jumamosi na jumapili,ukitenga muda wa saa moja na nusu kwa jumamosi na jumapili,inakua umefanya mazoezi ya masaa 3 kwa juma ambayo si mbaya kwa afya ya mwanaume.
Pia ukiwa kwenye mihangaiko,badili aina ya maisha unayoishi. Mfano,tumia ngazi badala ya lift;tembea kwa miguu badala ya kutumia gari kwa sehemu ambayo ni rahisi na fupi kwenda kwa miguu;tumia maji sana kama kinywaji badala ya soda na bia.
Ukifanya hakika heshima yako kwa mkeo lazima irudi.