Tufanye fundraising kuwasaidia waJapan | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tufanye fundraising kuwasaidia waJapan

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Game Theory, Mar 15, 2011.

 1. G

  Game Theory JF-Expert Member

  #1
  Mar 15, 2011
  Joined: Sep 5, 2006
  Messages: 8,571
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 0
  lakini kabla hatujafanya hivyo kwanza hebu tufanye valuation wao wanatusaidia vipi

  I can only imagine publicity itakayo generate how people from the poorest country in the world are helping one of the richest in the world

  mansemaje?
   
 2. samirnasri

  samirnasri JF-Expert Member

  #2
  Mar 15, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 1,377
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Kumbe jibu unalo sasa umeweka mada ya nini mkuu.
   
 3. G

  Game Theory JF-Expert Member

  #3
  Mar 16, 2011
  Joined: Sep 5, 2006
  Messages: 8,571
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 0
  lipi hilo?
   
 4. Z

  Zion Daughter JF-Expert Member

  #4
  Mar 16, 2011
  Joined: Jul 9, 2009
  Messages: 8,936
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145
  Kutoa ni moyo na si utajiri.Na formula mojawapo ya maisha ,jinsi utuavyo na ndivyo ubarikiwavyo...
  Mungu akuongoze unatoa wapi na kwa nia gani...
   
 5. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #5
  Mar 16, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,435
  Likes Received: 19,783
  Trophy Points: 280
  tatizo sisi tunapenda kusaidiwa tu ila hatupendi kusaidia tunaweza kuwapa hata kidogo hicho tulicho nacho kitawasaidia
   
 6. Shedafa

  Shedafa JF-Expert Member

  #6
  Mar 16, 2011
  Joined: May 21, 2008
  Messages: 802
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 35
  Kama inaweza kupatikana NGO itakayoweza kuratibu litakuwa jambo jema, wenzetu wanahitaji msaada hata huo mdogo utawasaidia. Kwa hiyo kimsingi umetoa wazo zuri, utekelezaji ndio utata.
   
 7. Washawasha

  Washawasha JF-Expert Member

  #7
  Mar 16, 2011
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,699
  Likes Received: 416
  Trophy Points: 180
  ina maana baada ya maafa haya jamaa watashuka kiuchumi au wataendelea ktk nafasi yao ya sasa? Na je wao wenyewe wanafanya jitihada gani kujisaidia?
   
 8. Shedafa

  Shedafa JF-Expert Member

  #8
  Mar 16, 2011
  Joined: May 21, 2008
  Messages: 802
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 35
  Nafikiri la msingi hapa si nafasi ya kiuchumi, haya ni maafa yamewapata wenzetu. Nafasi ya kiuchumi inayosemwa is just a position, has nothing to do with this!. Kama wao wakati wote wamekuwa wakijali tunapokosa chakula na kutuletea mchele tena bure, nafikiri kama binadamu inabidi tuiangalia hali yao katika jicho lingine. Hawa ni watu katika hali ya kawaida wasingehitaji msaada wa mtu yeyote, lakini hapa yamewakuta (sehemu ya jamii yao hawana pa kuishi, hawana chakula, maji, umeme, gas n.k). So kama kuna anayeweza kuratibu wakati ndio huu, sababu - anayetusaidia wakati wote leo naye ni muhitaji!.
   
 9. Duduwasha

  Duduwasha JF-Expert Member

  #9
  Mar 16, 2011
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 5,139
  Likes Received: 2,175
  Trophy Points: 280
  Nadhani Japan wanahitaji Msaada wa Nguvu za watu wenye uwezo wa kusaidia katika kujenga kuokoa waliosalia na kutafuta miili ya watu kwa muda huu kwanza. Hivi Japan wanasaidia wananchi wa Tanzania Au Serikali naomba ufafanuzi... Hawa wafadiri wanaosaidia upitia Serikali mie Siwaafiki kwani hakuna kitu tunachopata. Watoe misaada kwa wahusika Direct kuliko kupitia mikonono mwa mafisadi
   
 10. PPM

  PPM JF-Expert Member

  #10
  Mar 16, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 839
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Unafiki huo, mbona ukuanzisha mada ya kuchangia wahanga wa Gongo la Mboto, Kilombero. n.k
   
 11. Technician

  Technician JF-Expert Member

  #11
  Mar 16, 2011
  Joined: Mar 30, 2010
  Messages: 843
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Hata ukitoa shiling mia moja ni msaada mkubwa sana wa kujali maisha ya watu wengine.
  Wazo zuri sana Slidingroof,Lazima utakuwa mwanachama wa CHADEMA
  Naunga mkono wazo kwa 1200%
   
 12. meddie

  meddie JF-Expert Member

  #12
  Mar 16, 2011
  Joined: Oct 21, 2010
  Messages: 413
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 35
  ni kweli kwa wajapani tutakuwa tunakosa fadhira na utu, tukiishia kutoa salaam za rambirambi! hii si tu kutokana na ukubwa wa janga lenyewe bali ukweli kwamba wamekuwa msaada mkubwa sana kwetu. Kwa jinsi ninavyoona jamaa baada ya kutoa salaam za rambirambi hana tena la zaidi! Napendekeza kama ilivyokwisha ongelewa kwamba kutoa ni moyo na kidogo tutakachoweza kutoa kitakuwa ni msaada mkubwa kwa wenzetu kutokana na hali waliyonayo, CHADEMA watuongoze kuweza kutoa michango hii kwa wenzetu. I hope CHADEMA kunakitengo cha maafa!
   
 13. njiwa

  njiwa JF-Expert Member

  #13
  Mar 16, 2011
  Joined: Apr 16, 2009
  Messages: 11,076
  Likes Received: 1,811
  Trophy Points: 280
  kama ni pesa.. pia tuangalie uthamani wa Tshs Against JPY! .. inawezekana 100Tsh kwa wenzetu hainunui hata kahawa
   
 14. T

  TUWEKANE BAYANA Member

  #14
  Mar 16, 2011
  Joined: Mar 10, 2011
  Messages: 45
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  We sema unataka tuchangie ule wewe.. Japan visenti vyako hana shida navo.. Wewe ukishaoneshwa kuguswa tu na maafa kwa taifa kama lile inatosha.. I lived in japan for 6 years.. Trust me mchango kwa taifa kama letu wataona aibu kupokea.. Manake wakituangalia hata umeme hatuna na hatujapata maafa.. Tuchangeni tulipe dowans umeme uwake
   
 15. M

  Mfwatiliaji JF-Expert Member

  #15
  Mar 16, 2011
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 1,325
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Ama kweli akili ni nywele, kila mtu ana zake!!
  Naweza kuamini huu usemi walau kwa sasa.. Wajapani wamekumbwa na majanga ambayo binadamu hawezi kuyaelezea kwa lugha ya kawaida.
  Lakini wameona jinsi ulimwengu ulivyoduwaa na kupelekea masoko ya hisa kuyumba na kuporomoka ghafla dunia nzima.
  Nimefuatilia kwa karibu impact na kwenye mtandao inaonekana tangu juzi wame-pump karibu ya $350,000,000,000 ($350 Bil) kwenye world stock market ili ku-stabilize na kupunguza maafa ya kurudi tena kwenye mdororo wa uchumi wa dunia (world economic recession).
  Na kweli leo stock markets zimepanda ghafla dunia nzima!
  Tanzania je??!
   
Loading...