Hakuna hoja ya Rules of origin hapa. Rules of origin kazi yake ni kutambua mzigo unatoka wapi ili ijulikane kama una stahili preferential tarriffs ama sio.
Kwa mfano, kutokana na umoja wa kiforodha Africa Mashariki, mizigo ya iliyotengenezwa Kenya au Uganda itakuwa na viwango vyake vya kodi tofauti na mizigo kutoka nje ya umoja huo. Mizigo ya SADC vilevile.
Swala la mafuta kama ni ghafi au sio ghafi limeelezwa kwenye Common External Tarrifs..hiki ni kitabu ambacho kina bidhaa zote amabzo zinatambulika kwa namba maalum HS CODEs.
Mfano: Mafuta ya alizeti(sun flower oil)
Bidhaa HS CODE customs duty
Crude oil........................1512.11.00.................................10%
Refined oil......................1512.19.00...............................25%
Process ya kurefine ndo inaamua kama mafuta ni ghafi ama sio ghafi.
Process ya refine mafuta inahusisha kufanya chemical treatment ili kuondoa impurities na toxic substances. Process ina husisha bleaching, deodorization and cooling. Process inabadili muundo wa mafuta kikemikali.
Hivyo kinachotofautisha crude na refined ni chemical composition ambayo TBS ndo wanapima maabara.
Je kama ni ishu ya kemikali, TRA kwanini wanapinga majibu ya TBS ilhali hawana maabara? TRA wanaamini huko TBS huenda mtu kashkishwa cha juu na kutoa ripoti ambayo sio. Wanaamini process ya refining ishafanyika kwa asilimia kubwa, hivyo hayafai kuitwa ghafi. Naamini uchunguzi unaendelea.
SINTOFAHAMU:
1. Watu wanadhani mafuta ghafi hayafai kwa matumizi binadamu...yanafaa sana, tena yanashauriwa kitaalamu kwa afya. Ukiweza kukamua mafuta yako mwenyewe ya nazi au mawese, fanya hivyo. Kitaalamu yanaitwa virgin...kama ushaskia virgin olive oil.
2. Kwa nini sasa haya ya viwandani yawe refined? Inatokana na mazingira yaliyovunwa na kukamuliwa. Kwa vile yanavunwa na kukamuliwa on a commercial scale, yanakuwa na uchafu mwingi sana. Vile vile bila kurefine hayawezi kukaa mda mrefu bila kuharibika.
Nawasilisha