Huwa mimi kwenye ununuzi wa simu kitu cha kwanza ninachoangalia ni soc, ukipatia hapa then ndio unaanza kuangalia mambo mengine.
Kwenye Upper midrange simu za laki 7 mpaka 1m hivi kwa Snapdragon angalia sd 778G ni soc kali sana, Huhitaji battery kubwa hata 4000mah inatosha simu itakaa na chaji sana, alternative kwa Mediatek ni Dimensity 920/900.
Kwa simu za laki 4 na kitu hadi laki 6 hivi ambayo nahisi ni Budget yako Tafuta Snapdragon 695 ni soc nzuri sana nayo, ila ina weakness kubwa hairecord 4k video, hii soc ni efficient sana simu zake zinakaa na Charge pia ina nguvu sana compare na competition at Same price. Alternative yake ni Mediatek Dimensity 810.
Kwa laki 3 mpaka 4 hapa kama unapata Snapdragon 680 ni vyema, Otherwise Mediatek G80/G85/G88 si mbaya. Pia zipo Unisoc T606/610/700 etc nazo ni alternative nzuri.
Kwa chini ya laki 2 nusu unisoc T310 ina make sense zaidi sema simu chache sana wanatumia, Most of time ni eneo la kukimbia hakuna simu nzuri kivile, hope Samsung A03 itakuwa eneo hili (sio A03s)
Ukishapata soc of your choice sana una narrow down Choice zako. Mfano una 1m, Sd 778G ipo karibia Brand zote Samsung Ana A52s na M52, Xioami ana Mi 11 lite 5g ne, Kuna realme GT master etc. Kutokana na matumizi ndio unachagua inayokidhi, kama unakaa field wiki kadhaa huna umeme battery life itakua priority, upo dukani picha unapiga sana Camera itakuwa priority etc.