TUCTA yasalimu amri

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,319
33,125
headline_bullet.jpg
Yaondoa kusudio la kutaka kumshtaki Waziri Ghasia



RwegasiraTRAWU%281%29.jpg

Kaimu Katibu Mkuu wa Tucta, Silvester Rwegasira



Katika hatua inayoashiria kusalimu amri, Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi (Tucta) jana lilitangaza kuondoa kusudia lao la kutaka kumshtaki Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Utumishi wa (Umma) Hawa Ghasia kwa kushindwa kuwapa tuzo ya mazungumzo yao na serikali.
Tucta ilitoa siku saba kwa, Ghasia ambazo zilimalizika jana ili awe amewapa majibu ya mazungumzo hayo (tuzo), hatua ambayo imetekelezwa na serikali kabla ya muda walioutoa kumalizika.
Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake jana, Kaimu Katibu Mkuu wa Tucta, Silvester Rwegasira alisema hawana sababu ya kuendelea kumbana waziri huyo kwa kuwa ameishatekeleza madai yao.
Kwa upande wa bajeti iliyosomwa wiki hii na serikali mjini Dodoma, alisema bado Tucta haikubaliani na kipengele cha kupunguza kodi kwa asilimia moja.
Alisema kiasi hicho ni kidogo na kwamba hakiwezi kumsaidia mfanyakazi na badala yake alisema wao walitaka kiwango cha kodi katika mishahara kitozwe chini ya asilimia 10 kutoka 15 iliyokuwepo.
Serikali ilipunguza kiasi cha kodi kutoka asilimia 15 hadi 14 hatua ambayo wanasema bado hawaikubali.
Aliongeza kuwa kama serikali haitaongeza kima cha chini cha mishahara kwa wafanyakazi kwa kiwango cha kuridhisha, watakutana na wanachama wao ili kujadili hatua za kuchukua.
Alisema wanataka angalau serikali iwalipe Sh. 250,000 kwa mwezi kama kima cha chini endapo itakataa kiwango chao walichopendekeza cha Sh. 315,000.
Tucta ilitangaza kufanya mgomo kwa nchi nzima Mei 5 mwaka huu ili kuishinikiza serikali kupandishia kima cha mishahara pamoja na kupunguza kodi katika mishahara ya wafanyakazi.
Hata hivyo, hawakutekeleza mgomo wao baada ya Rais Jakaya Kikwete kuingilia kati na kuiwaonya kutofanya hivyo kwani suala hilo litamalizwa kupitia mazungumzo.



CHANZO: NIPASHE JUMAPILI
 
........sinema hii ya tucta na sirikali yaitwaje?? Director? Producer? Music by? Duration? Starring? Ina part ngapi?
 
Back
Top Bottom