kbm
JF-Expert Member
- Oct 5, 2012
- 5,224
- 1,687
Tucta yaitega serikali:
Shirikisho la Vyama Vya Huru vya Wafanyakazi Tanzania (Tucta) kimeibuka kuitega serikali kwa kuipa mwaka mmoja kuhakikisha wafanyakazi katika sekta zote wanalipwa kima cha chini cha mshahara kinachokidhi mahitaji ya msingi ya maisha kinyume na hapo halitasita kuchukua hatua za mgomo shinikizi.
Aidha, limeitaka serikali kupunguza kiwango cha kodi kinachotozwa kwa wafanyakazi kufikia asilimia 11 kwa vile wamevumilia hadi wamechoka kwa wafanyakazi kubebeshwa mzigo mkubwa wa kodi huku wafanyabiashara wakubwa wakisamehewa kodi na kulipa kodi ndogo isiyoendana na biashara zao na kama bajeti ya serikali ya mwaka 2013/14 haitazingatia hilo, watalazimika kuchukua hatua kupinga uonevu huo.
Hayo yalisemwa Jijini Dar es Salaam jana na Katibu Mkuu wa Tucta, Nicolaus Mgaya, alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kuelezea maazimio ya Baraza Kuu la Tucta katika kikao chao cha 14 kilichoketi Machi 28, mwaka huu.
Alisema bado wanaendelea kufanyamazungumzo na serikali kwa muda mrefu ndio maana wamekaa kimya kuitaka kutekeleza mapendekezo ya mshahara wa kima cha chini cha Sh. 315,000 ambacho kimepitwa na wakati na wanafanya utafiti ili kuja na kima kipya cha chini cha mishahara.
"Tumeipa serikali mwaka mmoja kuhakikisha wafanyakazi katika sekta zote wanalipwa kima cha chini cha mshahara, kinachokidhi mahitaji ya msingi ya maisha kinyume na hapo hawatasita kuchukua hatua za mgomo shinikizi wakati tukiendelea kufanya utafiti wa kima kipya cha mshahara," alisema Mgaya.
Aliongeza kuwa Baraza Kuu limebaini kuwapo na hatua chanya za kuboresha mifuko ya Hifadhi ya Jamii nchini na kasi ya maboresho ni ndogo kwani wafanyakazi wengi wanaendelea kustaafu kwa malipo kidogo ya pesheni huku mifuko ikiendelea kuneemeka na kuitaka serikali kukamilisha maboresho yake kwa kipindi cha mwaka mmoja.
Akizungumza kukoma kwa uongozi wa Rais Shirikisho hilo, Omari Ayoub Jumaa, alisema amemaliza muda wake kwa sababu za kikatiba kifungu namba 16.6 hadi 16.6.8.
Alisema Baraza Kuu limeazimia kuwa Maadhimisho ya Mei Mosi kitaifa mwaka huu yafanyike mkoani Mbeya.
CHANZO: NIPASHE