TUCTA ya beza hutuba ya Rais Kikwete

TUCTA ya beza hutuba ya Rais Kikwete

PISTO LERO

JF-Expert Member
Joined
Mar 8, 2011
Posts
2,819
Reaction score
1,458
SIKU moja baada ya Rais Jakaya Kikwete kulifungua Bunge Maalumu la Katiba mjini Dodoma, hotuba hiyo imebezwa na viongozi wa vyama vya wafanyakazi, wakidai amepuuza maoni ya Watanzania.

Walisema, hotuba ya mkuu huyo wa nchi imejaa siasa na kubeza kazi nzuri iliyofanywa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba chini ya uenyekiti wa Jaji mstaafu Joseph Warioba.

Kwa nyakati tofauti, viongozi hao waliwataka wajumbe wa Bunge hilo wasusie mjadala huo kwa kuwa maoni ya wananchi kutaka muundo wa serikali tatu yamepuuzwa.

Katibu wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania (TUCTA) Mkoa wa Dodoma, Ramadhani Mwendwa, alisema hayo jana wakati akitoa maoni yake kwa mwandishi wa habari hizi mjini hapa, kuhusu hotuba ya ufunguzi wa bunge hilo.

Katika maoni yake, Mwendwa ambaye pia ni Katibu wa Chama cha Wafanyakazi wa Taasisi ya Juu, Habari na Utafiti (RAAWU), Kanda ya Kati alisema kitendo cha Rais Kikwete kupuuza maoni ya Watanzania wanaotaka serikali tatu, kinakinzana na dhamira halisi ya taifa kupata katiba inayotokana na matakwa yao.

Alieleza kwamba kwa vile serikali na Chama Cha Mapinduzi (CCM) wanataka muundo wa serikali mbili kinyume na matakwa ya wananchi wanaowaongoza ni wazi kwamba hata vitatumika vitisho kwa wananchi wakati wa kuipigia kura ya maoni rasimu hiyo baada ya kupitishwa bungeni.

“Msimamo wa serikali mbili kwa wananchi ni wa kulazimishwa na dola. Hii inatokana na kwamba dola haitambui raia wake kwamba wana haki ya kusikilizwa na kutimiziwa natakwa yao… inawezekana kabisa Rais Kikwete anaamini alichaguliwa kwa bahati mbaya.

“Halafu kama serikali mbili ni nzuri mbona Rais Kikwete ameshindwa kueleza uzuri na matatizo yake badala yake amezungumzia matatizo ya serikali tatu tu?” alisema Mwendwa.

Alimpongeza mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Warioba na kusema: “Mzee Warioba kwa mawazo yake mazuri ya taifa hili… ana busara lakini baadhi ya viongozi ndani ya CCM na serikali ni mafisadi.”
 
Uongo mwingike huu hao tucta wamekutana lini kuponda hotuba kwa nini vijana wa bavicha wengi mnapenda uongo na kupotosha watu hakuna hotuba bora kama aliyotoa rais siku ile.
 
Huyu ndiye wa kupongezwa? Kwa kipi kwanza wakati ni mpotoshaji mkubwa tu.
 
Usilitumie vibaya jina la Taasisi. Huwezi kuchukuwa maoni ya Individuals ndaninya taasisi ukasema ni maoni ya taasisi. Maoni ya Taasisi lazima yaoneshe sehemu yalipotolewa, kama ni mkutano wa kawaida au dharura, idadi ya waliohudhuria nk. Mjifunze misingi imara ya uandishinwa habari
 
SIKU moja baada ya Rais Jakaya Kikwete kulifungua Bunge Maalumu la Katiba mjini Dodoma, hotuba hiyo imebezwa na viongozi wa vyama vya wafanyakazi, wakidai amepuuza maoni ya Watanzania.

Walisema, hotuba ya mkuu huyo wa nchi imejaa siasa na kubeza kazi nzuri iliyofanywa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba chini ya uenyekiti wa Jaji mstaafu Joseph Warioba.

Kwa nyakati tofauti, viongozi hao waliwataka wajumbe wa Bunge hilo wasusie mjadala huo kwa kuwa maoni ya wananchi kutaka muundo wa serikali tatu yamepuuzwa.

Katibu wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania (TUCTA) Mkoa wa Dodoma, Ramadhani Mwendwa, alisema hayo jana wakati akitoa maoni yake kwa mwandishi wa habari hizi mjini hapa, kuhusu hotuba ya ufunguzi wa bunge hilo.

Katika maoni yake, Mwendwa ambaye pia ni Katibu wa Chama cha Wafanyakazi wa Taasisi ya Juu, Habari na Utafiti (RAAWU), Kanda ya Kati alisema kitendo cha Rais Kikwete kupuuza maoni ya Watanzania wanaotaka serikali tatu, kinakinzana na dhamira halisi ya taifa kupata katiba inayotokana na matakwa yao.

Alieleza kwamba kwa vile serikali na Chama Cha Mapinduzi (CCM) wanataka muundo wa serikali mbili kinyume na matakwa ya wananchi wanaowaongoza ni wazi kwamba hata vitatumika vitisho kwa wananchi wakati wa kuipigia kura ya maoni rasimu hiyo baada ya kupitishwa bungeni.

"Msimamo wa serikali mbili kwa wananchi ni wa kulazimishwa na dola. Hii inatokana na kwamba dola haitambui raia wake kwamba wana haki ya kusikilizwa na kutimiziwa natakwa yao… inawezekana kabisa Rais Kikwete anaamini alichaguliwa kwa bahati mbaya.

"Halafu kama serikali mbili ni nzuri mbona Rais Kikwete ameshindwa kueleza uzuri na matatizo yake badala yake amezungumzia matatizo ya serikali tatu tu?" alisema Mwendwa.

Alimpongeza mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Warioba na kusema: "Mzee Warioba kwa mawazo yake mazuri ya taifa hili… ana busara lakini baadhi ya viongozi ndani ya CCM na serikali ni mafisadi."
Unafaa sana kujiunga na mashauzi classic bandi ili umsaidie isha mashauzi kutunga mipasho make ulichoaandika ni zaidi ya mipasho pole mkuu.
 
Unafaa sana kujiunga na mashauzi classic bandi ili umsaidie isha mashauzi kutunga mipasho make ulichoaandika ni zaidi ya mipasho pole mkuu.
Tehetehetehe, hakika Mashauzi Classic ndo habari ya MACHADEMA
 
Usilitu,ie vibaya jina la Taasisi. Huwezi kuchukuwa maoni ya Individuals ndaninya taasisi ukasema ni maoni ya taasisi. Maoni ya Taasisi lazima yaoneshe sehemu yalipotolewa, kama ni mkutano wa kawaida au dharura, idadi ya waliohudhuria nk. Mjifunze misingi imara ya uandishinwa habari
Sure mkuu huyu kakaa chumbani kwake kashiba uji anaanza kutunga uongo wake halafu anatwambia mawazo ya tucta bavicha ni vijana wa ajabu sana mimi naamini kuwa yeyote anayepinga hotuba ya rais lazima awe na shida kidogo kichwani mwake.
 
Hivi huko Jehannam kuna nafasi ya kutosha kwa wasema uongo na wasengenyaji?
 
Unafaa sana kujiunga na mashauzi classic bandi ili umsaidie isha mashauzi kutunga mipasho make ulichoaandika ni zaidi ya mipasho pole mkuu.

Kuna mipasho gani zaidi ya aliyotoa mwenyekiti wa ccm mbele ya kile kinachoitwa bunge la katiba.
 
Unafaa sana kujiunga na mashauzi classic bandi ili umsaidie isha mashauzi kutunga mipasho make ulichoaandika ni zaidi ya mipasho pole mkuu.

Na alichoongea mwenyekiti wenu pale bungeni kilikuwa ni mashairi ya nini?
 
Uongo mwingike huu hao tucta wamekutana lini kuponda hotuba kwa nini vijana wa bavicha wengi mnapenda uongo na kupotosha watu hakuna hotuba bora kama aliyotoa rais siku ile.

Ulitagemea wakutumie barua kwanza kabla ya kukutana?!
 
Sio bure watanzania tumelogwa,inaonyesha wazi watanzania tuko mambumbu wa kutupa.Tangu lini na wapi uliona katiba ya nchi ikatengenezwa na rais wa nchi au chama na kama sio wananchi?Watu wanaleta ushabiki wa kijinga tu hapa lakini hawataki kukubali ukweli kwamba rais amekosea kwa asilimia mia zote,na kwa nini asijiuzulu ?Ujinga mtupu eti katoa hotuba ya mwaka kwa lipi la maana alilosema kma sio ushabiki.Na hao wajumbe kama wanazo akili timam kuanzia keho wangerudi majumbani kwao wakaendele na shugli zao kwani ccm wamekwishatoa katiba ya nchi.
 
Uongo mwingike huu hao tucta wamekutana lini kuponda hotuba kwa nini vijana wa bavicha wengi mnapenda uongo na kupotosha watu hakuna hotuba bora kama aliyotoa rais siku ile.
MMOJA AWEZA WAKILISHA MANENO YA WENGI, KAMA AFANYAVYO NDUGUYENU KIKWETE, aliyoyazungumza bungeni aliitisha kikao cha NEC??????????????/, Acheni uvivu wa kufikiri.
 
Hawa TUCTA hawana adabu.
Nasema tena ni vyema hoja za Mh Rais zikapanguliwa kwa hoja si kushauri watu wakimbie mijadala.

Jk katoa hoja zake na nyie toeni hoja zenu sisi wananchi tutapima na kufanya maamuzi.

Na kama mtu anaona bunge la katiba halimfai ni vyema akafunga virago na kuondoka asisubiri kushauriwa kuondoka.
 
Back
Top Bottom