Mi nadhani hatua madhubuti ya kuchukua ni kama vyama vya wafanyakazi katika nchi zingine, haswa nchi zenye viwanda vingi duniani
TUCTA wanatakiwa waweke msimamo kuwa kama serikali (ya CCM) haitarekebisha mishahara ya wafanyakazi basi wanachama hawataipigia CCM kura kwenye uchaguzi ujao.
Huo ndio msimamo. Halafu sasa inatakiwa vyama vya upinzani vitumie mgogoro huu katika kampeni (si kampeni tu, pia wahakikishe wanatimiza ahadi iwapo watachaguliwa, si tena ahadi za 'maisha bora....'!)
Kwa nini CCM inabembelezwa? Au viongozi wa TUCTA wana uanachama CCM hivyo wanaogopa kukorofishana?[/QUOTE]
Mkuu Injinia,
Hiyo statement yako (in bold) ndio ukweli wenyewe. Hatuna vyama huru vya wafanyakazi Tanzania, hata kimoja. Hizo zote wanazozifanya ni siasa tu!!! Nasikia Mgaya ana mpango wa kugombea ubunge kwenye jimbo mojawapo wakati wa uchaguzi mkuu mwaka huu. Sasa tutarajie nini kutoka kwa kada wa CCM? Hatasimama vipi kuipinga serikali/kugoma dhidi ya serikali inayoongozwa na chama ambacho yeye ni kada wake? Changa la macho kwa wafanyakazi!!!!!
Tiba