Tucheze na vyote, si Mahakama | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tucheze na vyote, si Mahakama

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by FIKRA MBADALA, Nov 10, 2011.

 1. FIKRA MBADALA

  FIKRA MBADALA Senior Member

  #1
  Nov 10, 2011
  Joined: Jun 30, 2008
  Messages: 167
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  John Bwire

  gazeti la raia mwema 9 - 15 novemba, 2011

  DALILI za wazi zimeanza kujitokeza kwa baadhi ya wanasiasa kuanza kudharau Mahakama. Baadhi yao, wamekuwa wakifanya hivyo kwa sababu za kisiasa.

  Lakini wengine wamekuwa wakihusisha dharau hiyo dhidi ya Mahakama kwa kile wanachokiita, kupigania haki. Kimsingi, dharau yoyote inayoweza kufanywa dhidi ya Mahakama ni mbaya.

  Si jambo la kujisifia wala kupongezana. Ni suala la kukemewa. Sababu kubwa inatokana na ukweli kwamba, Mahakama ndiyo muamuzi wetu kwa pamoja kuhusu hisia zetu iwe hisia za kisiasa, kidini au vyovyote vile.

  Lakini kubwa zaidi, kwa viongozi wa Serikali na hata wanasiasa moja ya vipimo muhimu vya ukomavu wao ni namna wanavyoweza kuishi kwa kuheshimu Mahakama.

  Hata hivyo, tunatambua kuwa baadhi ya watendaji wa Mahakama ni dhaifu kimaadili, wanatia doa Mahakama kama mhimili wa Taifa na kimsingi, hawapaswi kuvumiliwa kwa mujibu wa taratibu, kanuni na sheria za kazi.

  Lakini udhaifu huu si kigezo cha kufikia hatua ya kudharau Mahakama. Taratibu ziko wazi, usiporidhika na ngazi moja ya Mahakama, milango ya ngazi nyingine iko wazi.

  Tunapenda kuwaambia wanasiasa ndani ya vyama vya upinzani pamoja na chama tawala, watumishi wa umma na sekta binafsi na wananchi kwa ujumla, kwamba hakika hatuna sababu za msingi kuanza kudharau Mahakama.

  Mahakama zinazojengewa mazingira ya dharau ndiko baadhi ya masikini wanatarajia kupewa haki zao walizoporwa. Kwa hiyo, wanasiasa wanapofanya matukio yenye tafisiri ya kudharau au kuingilia uhuru wa Mahakama, watambue hilo.

  Harakati za siasa zenye tafsiri ya kuingilia uhuru wa Mahakama, hazijengi nchi wala kuweka misingi ya kuimarisha utoaji haki na utawala bora nchini. Kinyume chake, harakati hizo mbele ya macho ya wadau wa utawala bora na wanasheria makini, zinawadhalilisha wanasiasa husika.
   
 2. Ringo Edmund

  Ringo Edmund JF-Expert Member

  #2
  Nov 10, 2011
  Joined: May 10, 2010
  Messages: 4,895
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 0
  mahakana ilikaa usiku katika kesi ya waalimu dhidi ya serikali hakuna kujidharaulisha zaidi ya hapo.
   
 3. THINKINGBEING

  THINKINGBEING JF-Expert Member

  #3
  Nov 10, 2011
  Joined: Aug 9, 2010
  Messages: 2,726
  Likes Received: 854
  Trophy Points: 280
  Mahakama yetu imeshajizalilisha na kujidunisha yenyewe.
  Mahakama kwa sasa si mahali pa mnyonge kutarajia kupata haki.
  Ni jambo la kushangaza kuwataka watu waheshimu kitu kisichojiheshimu.
   
 4. Mohammed Shossi

  Mohammed Shossi Verified User

  #4
  Nov 10, 2011
  Joined: Jan 17, 2011
  Messages: 3,986
  Likes Received: 123
  Trophy Points: 160
  Mleta mada umenikumbusha kesi ya TID jamaa alifanya jeuri na kuuliza kwani kama ninakosa faini shs ngapi! hakimu wakati anatoa hukumu alitaja mvua tu bila faini!
   
 5. s

  seniorita JF-Expert Member

  #5
  Nov 10, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 674
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Napita
   
 6. Micro E coli

  Micro E coli JF-Expert Member

  #6
  Nov 10, 2011
  Joined: Oct 31, 2011
  Messages: 943
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Mahakama za Tanzania hakuna kitu ndio maana Mwalimu hakuziachia zitoe hukumu dhidi ya walarushwa waliwahukumu kwanza yeye mwenyewe kwa viboko na kuwafukuza kazi hadhalani hata mbele ya wananchi,mahakama hizi za uccm hamnakitu.
   
 7. Fyengeresya

  Fyengeresya JF-Expert Member

  #7
  Nov 10, 2011
  Joined: Oct 10, 2011
  Messages: 702
  Likes Received: 158
  Trophy Points: 60
  Nashukuru kwa uchambuzi wako ni kweli tumefikia mahali pabaya kwa kudharau chombo ambacho ilitakiwa kuwa kimbilio la wanyonge. Nasema ilitakiwa kwa sababu hata Jaji mkuu mstaafu amekiri katika moja ya 'presentation' zake kwamba aliwahi kuagizwa au kushinikizwa kutoa uamuzi kinyume cha taaluma yake. Je katika hali hiyo unategemea watumishi wengine wa Mahakama watakuwa katika hali gani kama sio kutekeleza amri hizo? Inapotokea uamuzi wa mahakama unatolewa katika ngazi za chini lakini unafutwa au kugeuzwa ngazi za juu hawa wananofungwa miaka mingi kwa kukosa kukata rufaa kutokana na uwezo wao mdogo wa kiuelewa wa sheria na kiuchumi bado mahakama ipo salama? Nafikili tunatakiwa pamoja na kujizuia kuidharau mahakama lakini tuiambie namna tunavyoona utendaji wake kwamba si wa kuridhisha.
   
 8. N

  Ninaweza JF-Expert Member

  #8
  Nov 10, 2011
  Joined: Dec 14, 2010
  Messages: 7,164
  Likes Received: 1,167
  Trophy Points: 280
  Mahakama nayo inajijua kuwa haipo huru, mtoa mada haishi tz.
   
 9. Kinyungu

  Kinyungu JF-Expert Member

  #9
  Nov 10, 2011
  Joined: Apr 6, 2008
  Messages: 4,380
  Likes Received: 3,339
  Trophy Points: 280
  Hivi Tanzania nako kuna mahakama?
   
 10. C

  Cipro Senior Member

  #10
  Nov 10, 2011
  Joined: Aug 8, 2011
  Messages: 159
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  kitu kikiwa kibovu lazma kidharaulike,sio mahakama tu,serikali kwa ujumla ni mbovu na inadharaulika,huduma za afya na hospitali ni mbov na zinadharaulika,system za elimu kuanzia msingi mpk chuo ni mbovu na zinadharaulika,jeshi letu ni bovu na linadharaulika.mambo yetu mengi ni mabovu na tunayadharau.
   
 11. M

  Mindi JF-Expert Member

  #11
  Nov 10, 2011
  Joined: Apr 5, 2008
  Messages: 1,393
  Likes Received: 945
  Trophy Points: 280
  nina tatizo kubwa na Raia Mwema. wamekuwa wakitoa tahariri ambazo haziendani na rekodi yao kwa ujumla. kwa mfano walisifia mkutano wa uwekezaji wa mikoa ya Ziwa Tanganyika ulioitishwa na Mh. Pinda. kwa gazeti kama hilo, lilitakiwa kuchambua rekodi ya uwekezaji katika nchi hii, kuonesha upotovu ulioko katika hoja nzima ya "kuwaletea watu maendeleo" kwa kutumia "wawekezaji". sifa zilizotolewa na Tahariri ya Raia mwema kuhusu suala hilo ilikuwa haina uchambuzi wa kina. katika hili la mahakama, ajenda sio utawala wa sheria, bali ni jinsi sheria na taratibu zake zinavyotumika kukandamiza watanzania hasa wanyonge. vyombo vya dola vimekuwa vikitumiwa kulinda maslahi ya tabaka la viongozi na wenye nacho. sasa hiyo siyo mahakama tena. kwa mujibu wa katiba, mamlaka yapo kwa wananchi. kama inawezekana chama au kikundi cha watu kikawashawishi watanzania kwamba mahakama zao hazitendi haki kwa mujibu wa katiba yao, hiyo itakuwa ni huduma nzuri sana kwa watanzania.

  kwa maneno mengine, kitendo kinachofanywa na vikundi au vyama, mfano CHADEMA, kuonesha udhaifu wa mahakama zetu, ni kitendo cha kimapinduzi na kinachopaswa kupongezwa. wanaoweza kulalamikia kitendo kama hicho ama ni wale wanaofaidika na utaratibu uliopo sasa hivi, ama hawaelewi wanachozungumza. kwa Raia Mwema, nadhani wana lengo lao. sina tatizo na makala zao zingine, lakini Tahariri kwa kweli zina matatizo
   
 12. kichomiz

  kichomiz JF-Expert Member

  #12
  Nov 10, 2011
  Joined: Feb 28, 2011
  Messages: 11,992
  Likes Received: 2,650
  Trophy Points: 280
  Eeeh mbona zipo nyingi tu mahakama za Tanzania ni kwa ajili ya kuwanyanyasa wanyonge tu.
   
 13. Mzee wa Rula

  Mzee wa Rula JF-Expert Member

  #13
  Nov 10, 2011
  Joined: Oct 6, 2010
  Messages: 8,177
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  Chunguza utendaji kazi wa mahakama umejaa harufu ya rushwa, kesi zote ambazo hazina interest na serikali basi mahakimu hapo ruksa kuchukua rushwa na kesi yoyote inayokuwa na interest na serikali basi maamuzi huyolewa kwa shinikizo. Mfano wa kesi hizo ni zilezinazohusu ichaguzi, na vyama vya upinzani.
   
 14. Mzee wa Rula

  Mzee wa Rula JF-Expert Member

  #14
  Nov 10, 2011
  Joined: Oct 6, 2010
  Messages: 8,177
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  Chunguza utendaji kazi wa mahakama umejaa harufu ya rushwa, kesi zote ambazo hazina interest na serikali basi mahakimu hapo ruksa kuchukua rushwa na kesi yoyote inayokuwa na interest na serikali basi maamuzi hutolewa kwa shinikizo. Mfano wa kesi hizo ni zilezinazohusu uchaguzi, na vyama vya upinzani.
   
 15. u

  utantambua JF-Expert Member

  #15
  Nov 10, 2011
  Joined: Aug 1, 2011
  Messages: 1,373
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Kuheshimu mahakama? Tumsome carl Marx ili tujue mahakama zipo kwa nani na kwa ajili ya nini. Kuanzia hapo ndio tujenge msingi wa hoja na maswali kama alivyoleta muanzisha thread
   
 16. Perry

  Perry JF-Expert Member

  #16
  Nov 10, 2011
  Joined: Feb 24, 2011
  Messages: 10,028
  Likes Received: 853
  Trophy Points: 280
  Toka lini tanzania kukawa na mahakama jaman au mnaizungumzia ICTR?
   
Loading...