Binti wa zamani
Platinum Member
- Nov 19, 2011
- 11,763
- 27,150
Ushabiki wa kisiasa pembeni, nafikiri mahojiano haya yametupa taarifa nyingi mpya za maisha binafsi na ya kifamilia ya Hayati Magufuli ambazo zilikua hazifahamiki hapo kabla.
Kipi umejifunza kuhusu hayati Magufuli na familia yake kupitia hii interview?
Binafsi kwa mara ya kwanza nimejua kuhusu;
Tupia yako uliyookota kwenye Part 1 ya interview hii.
Cc:
Aaliyyah , bonjov , makutupora , Half american , To yeye , Poor Brain , ledada
Kipi umejifunza kuhusu hayati Magufuli na familia yake kupitia hii interview?
Binafsi kwa mara ya kwanza nimejua kuhusu;
- Namna alivyozingatia tamaduni na miiko ya familia kama watoto wake kuja kumsalimia kila siku asubuhi saa kumi na mbili - hata alipokua ikulu.
- Historia ya jina la Magufuli na kwamba halikua jina halisi la ukoo wao na lilitokana na babu yake aliyekua akicheza ngoma na makufuli 🔒🔓🔐.
- Picha za vipindi mbalimbali vya maisha yake na mkewe mama Janet, kutotumia vilevi kama pombe na kurudi nyumbani saa kumi na mbili jioni ili kuwa na muda na familia yake. Kuna la kujifunza hapa kwa vijana ambao mmeoa au bado hamjaoa.
- Sikujua kama mazingira tatanishi ya kifo chake yalileta sintofahamu kwa familia yake pia, baadhi ya watoto na ndugu hawakupata taarifa za msiba mpaka walipoona mitandaoni.
- Hakua baba wa kudekeza watoto wala kupenda kuwalimbikizia mali. Watoto wake kupewa zawadi za magari ya kawaida kama Toyota Raum na IST hata alipokua Raisi ambaye anamudu kifedha kuwanunulia magari ya kifahari.
- Hobbies - hata alipokua Raisi, kwenye muda wake binafsi aliendelea kufanya vitu binafsi vya kumfurahisha kama ufugaji wa ng’ombe na kuvua samaki, I hope tunalibeba hilo kama funzo pia.
Tupia yako uliyookota kwenye Part 1 ya interview hii.
Cc:
Aaliyyah , bonjov , makutupora , Half american , To yeye , Poor Brain , ledada