Tubadili mfumo wa Uongozi. Twendeni kwenye uhalisia wenyewe

FAHAD KING

JF-Expert Member
Sep 14, 2017
301
373
Nafahamu Katiba si kipaumbele cha Raisi wa awamu hii ya 5 Mh. Rais John Pombe Magufuli. Na pia nafahamu wanadamu tumeumbwa kusahau lakini kwa watanzania huenda tumeumbwa zaidi kusahau. Kwanini nasema hivi, tumesahau mchakato mzima wa katiba. Hatuna haja nalo tena. Limetupitia kushoto kabisa.

Tumekumbwa na janga la ugonjwa wa Corona. Nafahamu sio kwetu tu ni dunia kwa ujumla. Nimefarijika pale serikali imejitahidi kuchukua hatua kadhaa kuzuia maambukizi ya Corona. Jitihada zitaleta matunda tu endapo wahusika ambao ni sisi tukiuvaa uhusika wenyewe kwa asilimia 100 bila kujali huyu kafanya nini? Tumeona shule kufungwa, uhimizaji wa kunawa mikono kwenye mabenki, mahoteli, vituo vya daladala na usafiri kwa ujumla, kila sehemu japo hatuna imani kama kutazuia lakini hata kupunguza maambukizi ni faraja kwa watanzania. Tujipe Kongole kwelikweli.

Shida ni pale tunachanganya Siasa na U-profesional kwenye janga kama hili. Hapo ndo nachoka kabisa. Wanasiasa wengi sio wasomi wala hawatakiwi kujadili mambo ya kitaalamu mbele ya kadamnasi sababu tutakaoangamia wengi ni sisi wasikilizaji. Hatujui chochote kuhusu Corona. Napata sana kujaribu kuwaelewa Wanasiasa kuongelea hili suala nyeti linalogharimu uhai wa watu.Hivi kuna umuhimu wa wataalamu wa afya nchini? Hata kwenye suala nyeti kama hili, nani alipaswa kua kifua mbele kujadili janga hili kati ya wataalamu wa afya na wanasiasa?

Ni bora sekta nyeti ziende kwa wataalamu husika. Mfano Wizara ya viwanda na Biashara iende kwa mfanyabiashara mzoefu, wizara ya afya na ustawi wa jamii iende kwa mtaalamu wa afya. Tusifanye mambo kwa kubahatisha. Tusifanye mambo kiholela eti kwakua tu jirani yangu kafanya. Tufanye mambo kwa asilimia 100 tukisubiri impact zake kwa jamii. Tusikurupuke tu nasi tukafanya.

Je, katiba inazingatia hili? Kuna haja ya katiba kubadilisha sifa za mtu anaepaswa kua kiongozi. Wasomi wengi hawana kazi, madegree Holders kibao, Masters na PhD holder's pia wote hawana kazi tena wenye fani tofauti. Kwanini tusibadilishe kipengele cha yoyote tu anafaa kua kiongozi kwakua anajua kusoma na kuandika? Kwanini tuendelee kushika bango na kung'ang'ania watu wanaosoma tu kushika nyadhifa nyeti huku tunaacha wataalamu wenyewe Jobless? Mmewapa ujuzi wa nini?

Ifike mahala Mambo ya uchumi na viwanda wajadili wasomi waliosomea uchumi wenyewe, mambo ya afya wajadili wataalamu wa Afya lakini si wanasiasa ili kuepekuka kubahatisha bahatisha kama tunavyofanya sasa. Hii ni dhambi tuileayo. Tutaangamia sio sababu hatuna maarifa, hapana bali tutaangamia kwa kua na maarifa tele.

Nawasilisha

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom