Tuanze kupata background ya Mulongo

Tuanze kupata background ya Mulongo

Lukansola

JF-Expert Member
Joined
Sep 5, 2010
Posts
5,435
Reaction score
1,611
Nili m-google huyu jamaa ndo nikapata hii nikaone niwashirikishe. Soma

MKUU WA MKOA WA ARUSHA AONYWA






mkuu wa mkoa wa Arusha Magesa Mulongo
KAMATI tendaji ya jumuiya ya tawala za mitaa nchini(Alat) imemwonya mkuu wa mkoa wa Arusha,Magesa Mulongo kuacha kujichukulia sheria mikononi kwa kuamuru mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Monduli kukamatwa na kuwekwa ndani kitendo ambacho wamedai ni udhalilishaji dhidi ya mtumishi huyo wa umma.

Pia,imesikitishwa na kitendo cha serikali kufuta ruzuku za jumla kwa halmashauri mbalimbali nchini kwa kuzitaka halmashauri hizo kukusanya fedha zao kupitia kodi za leeni na kusema kwamba kitendo hicho kinaleta changamoto katika shughuli za uendeshaji wa halmashauri zao.

Hivi karibuni mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Monduli mkoani Arusha,Samwel Mlay alikamatwa na jeshi la polisi na kisha kuwekwa ndani kwa agizo la mkuu wa mkoa wa Arusha baada ya kudaiwa kushindwa kuwawajibisha watumishi waliohusika na uchakachuaji wa mashine ya Excavator.

Akitoa tamko jijini Arusha,mwenyekiti wa Alat taifa,Didas Masaburi ambaye meya wa jiji la Dar es salaam mbele ya wajumbe wa jumuiya hiyo kutoka kila kanda nchini alisema kwamba kamati tendaji ya chama chao imesikitishwa na kitendo kilichofanywa na mkuu wa Arusha kuagiza kukamatwa mkurugenzi wa halmashauri ya Monduli na kisha kuwekwa ndani.

Alisema kwamba kitendo kilichofanywa na mkuu huyo wa mkoa wa Arusha kinawapa mashaka mazito huku akisisitiza kuwa kuwa mkurugenzi wa halmashauri isiwe chanzo cha kuwekwa kizuizini.

"Inapofikia mkuu wa mkoa anaagiza mkurugenzi akamatwe inatupa mashaka sana,naomba ieleweke kwamba kuwa mkurugenzi wa halmashauri isiwe chanzo cha kuwekwa kizuizini"alisema Masaburi

Hata hivyo alisisitiza ya kwamba kuna taratibu mbalimbali za kiutawala za kuwawajibisha watumishi wa halmashauri mbalimbali nchini vikiwemo vikao vya kiutawala na kushangaa kitendo kilichofanywa na mkuu huyo wa mkoa.

Alisema kwamba jumuiya yao haina lengo la kutetea uovu wa iana yoyote lakini umejidhatiti kutetea haki za wanachama wao pale zinapominywa huku akibainisha kuwa wamejipanga kusimamia haki za wanachama wao kikamilifu.

Katikaa hatua nyingine,Masaburi alilaani mauaji ya wenyeviti wawili wa halmashauri ya Rukwa na Uyui hivi karibuni na kusema kwamba jumuiya yao imesikitishwa na mauaji hayo na kuitaka serikali ichukue hatua kukomesha mauaji hayo.

Alisema kwamba jumuiya yao imesikitishwa na mauaji ya wenyeviti hao yaliyofanyika katika kipindi cha miezi sita huku akisema kwamba serikali inatakiwa ichukue jitihada kukomesha mauji hayo ama sivyo huenda yakazidi kuendelea.

Wakati huo huo,mwenyekiti huyo alisisitiza kwamba wana wasiwasi kwamba serikali ina nia ya kuua halmashauri mbalimbali nchini kwa kuwa awali walianza kuwanyang"anya madaraka,kuwazuia kuajiri na sasa wanazinyima ruzuku katika halmashauri zao.

Mkuu wa mkoa wa Arusha,Mulongo alipotafutwa kwa njia ya simu yake ya mkononi na gazeti hili simu yake iliita muda mrefu bila kupokelewa.
 
Ni nani huyu mtu? wanaomfahamu vizuri watupe japo A,B,C kuhusu background yake hasa kazi alizowahi fanya huko nyuma, elimu yake, uhusiano na wakubwa (kama upo zaidi ya ule wa kikazi), n.k
 
Ni nani huyu mtu? wanaomfahamu vizuri watupe japo A,B,C kuhusu background yake hasa kazi alizowahi fanya huko nyuma, elimu yake, uhusiano na wakubwa (kama upo zaidi ya ule wa kikazi), n.k

Nami nasubiri kwa hamu, maana maajabu aliyofanya Arusha mmmhhh...
 
Simfahamu, na in fact mtu huhitaji kumfahamu ili ujue kuwa mulongo hafai hata kuwa balozi wa nyumba 10!
 
ana elimu gani huyu?
ameshawahi kufanya kazi zipi zaidi ya kuwa RC?
 
ana elimu gani huyu?
ameshawahi kufanya kazi zipi zaidi ya kuwa RC?

mi najua kabla ya kuwapromoted na uvccm na mkulu kutoka huko kwao wanakotaka kujenga bandari mpya alikuwa mkuu wa wilaya yao....ila kabla ya hapo i guess alikuwa mchesha chai lumumba
 
Hii inashangaza. Kwani alipoteuliwa hakupewa 'Job description?' Na kama hakuielewa si aulize waliomtangulia? Kumbukeni alikuwa DC Bagamayo kabla hajateuliwa kwenda Arusha. Labda watu wa Bagamoyo wanaweza kuelezea japo kwa ufupi utendaji kazi wake.
 
Pole wakazi wa arusha tatizo ni matumizi mabaya ya nguvu za dola na hakuna cha kushangaa kumbe ameweza kuwaweka wasaidizi wake lokapu anahitaji ushauri
 
Inamaanisha wewe umeyatoa wapi haya majungu kwani ulikuwepo na katika kikao hicho unaweza ukawa na ripoter wako wa binafsi hakikisha taarifa unayoirusha unauhakika nayo hebu tupe kazi za mkuu wa mkuakam unazifahamu vizuri
 
Na kama kuna anayejua kama ana matatizo yoyote ya kiafya kama Kisukari N.k , Maana matatizo kama ya Diabetes yanaweza kumsababishia mgonjwa kupoteza kumbukumbu , hivyo moja kwa moja kuathiri utendaji kazi wa Mhusika .
 
Hii inashangaza. Kwani alipoteuliwa hakupewa 'Job description?' Na kama hakuielewa si aulize waliomtangulia? Kumbukeni alikuwa DC Bagamayo kabla hajateuliwa kwenda Arusha. Labda watu wa Bagamoyo wanaweza kuelezea japo kwa ufupi utendaji kazi wake.
Tatizo wanapoambiwa kwamba wao ni wenyeviti wa kamati ya ulinzi na usalama wa mikoa wanadhani basi wao wanaweza kumchukulia hatua kila mtu, wakati hapo kiutaratibu alitakiwa atoe mapendekezo kwa bosi wake kuhusu utendaji kazi wa huyo mkurugenzi for action maana huyu mkurugenzi ni mtendaji wa serikali ambayo ni kazi professional na mkuu wa mkoa ni mtawala (nafasi ya kisiasa na ya kuteuliwa), yeye anaowawajibisha ni ma-Dc, makatibu tarafa, ma-RAS, ma-DAS na wenyeviti wa vijiji but based na sheria ya nchi ikiwa sambamba na kuitisha vikao. Alivyoambiwa ana uwezo wa kumweka ndani mtu kwa 14 days basi anajua ukiamua tu unamweka mtu ndani. Inanikumbusha sakata la Ole Sendeka na mkuu wa mkoa wa Manyara (Shekifu enzi hizo) alifumfuza Ole Sendeka mbele ya wapiga kura wake jamaa likagoma
 
Na kama kuna anayejua kama ana matatizo yoyote ya kiafya kama Kisukari N.k , Maana matatizo kama ya Diabetes yanaweza kumsababishia mgonjwa kupoteza kumbukumbu , hivyo moja kwa moja kuathiri utendaji kazi wa Mhusika .
Ana miwaya a.k.a ngoma
 
alisababisha mama msemwa aliyekuwa DED BAGAMOYO kufikishwa mahakamani, kwa wasiomjua MULONGO MAGESA kabla yakuwa DC BAGAMOYO alikuwa anafanya kazi TISS
 
Kumbe amezoea kutoa amri za kuweka watu NDANI!
 
Alikuwa mfanyakazi wa TTCL mbeya kabla haja-side na JK na kupewa zawadi. Ni mtu wa usalama
 
Back
Top Bottom