Abdul Nondo
JF-Expert Member
- Oct 28, 2016
- 515
- 2,874
Suala la tume huru ni suala nyeti sana ,sio suala la vyama vya siasa tuu ,sio suala la chama kimoja kimoja tuu, sio suala la wanaharakati tu, sio suala la Azaki tuu,ni suala jumuishi linalotakiwa kujumuisha watu wote na taasisi zote.
Ila ili huu ujumuishi (inclusiveness) uweze kufanikiwa kirahisi na kwa uimara zaidi ni vyema sasa wale main actors (MA) katika sphere hii kuanza mchakato wakulifanya suala hili kuwa jumuishi na sio binafsi. Main actors ni vyama vya siasa.
Tusikimbilie kusema " *suala hili sio la vyama tuu ,tusitegemee vyama.Bali hata wewe dai tume huru* " Ndio ninadai na tunadai Ila kwa mpangilio upi ? ,Lazima kuwe na mpangilio na uratibu wa pamoja ili sauti zetu zote zisikie kwa pamoja ,sauti zisizo na mpangilio ni fujo.Vyama vya siasa hili ni jukumu lao kubwa kuratibu kuweka watu na taasisi pamoja.
Kilichoniuma sana ni kuona pia waziri mkuu akijibu swali la Mh.@freemanmbowetz kivyepesi kabisa kama kauli au msimamo wa serikali alafu wala hakuna mjadala ulioibuka kumpinga na kumkosoa waziri mkuu juu ya kauli yake.
Watu walichukulia simple tuu ,alafu kesho yake naendelea kuona watu baadhi wanapost tume huru ,tume huru .Mzizi ungetakiwa kwa umoja kauli ya waziri mkuu kama kauli ya serikali kusema" tuna tume huru inayofanya kazi bila kuingiliwa "siku ile ile hii kauli ilipaswa kuoingwa kila Kona na watu wote.
Na kuonesha namna gani kauli yake ni ya upotoshaji ,nilijiaribu kuandika kuonesha hili Ila watu hawajali, watu wanadhani tume huru ni agenda ya kikundi fulani kwamba ukisema ,utaonekana umeiba agenda ya kikundi fulani na hicho kikundi fulani kitaona umeiba agenda yao,this is childish.
Tunaomba vyama pinzani (opposition parties) na Mabaraza ya vijana yote ya vyama pinzani (The party Youth leagues /wings) nchini miongoni mwao kwanza yangekutana haraka yakajadili namna ya ku mobilize vijana wao nchi nzima, namna ya kushirikiana na Azaki , taasisi za dini na wanaharakati na watu wengine.
Ili kuwe na Agenda moja ya kitaifa kuelekea uchaguzi mkuu.Lazima uratibu huu ufanyike sababu ni nje ya muda ingawa sote kwa pamoja hatujachelewa.tulitarajia this movement ya kudai Tume huru ingeanza muda miaka nyuma 2016/2017/2018/2019 kwa Sasa 2020 jambo hili linahitaji umakini na umoja wa hali ya juu sababu huu mwaka una mambo mengi sana.
Azaki pia hazipaswi kubakizwa nyuma ,zinapaswa kushiriki kikamilifu ingawa ni Azaki chache zipo active zingine nyingi zina hofu kwamba kudai Tume huru ni kujihusisha na siasa ,sababu Agenda hiyo ni ya wanasiasa nadhani kama kuna wanaodhani hayo ,wana uwelewa mdogo tuu wa mambo .Tume huru ya uchaguzi ni moja ya nyenzo kubwa ya uchaguzi huru na haki, uchaguzi huru na haki ni moja ya msingi mkubwa wa Demokrasia .Demokrasia kwa upana wake inajumuisha haki za binadamu katika upande wa haki za kisiasa na kiraia (Civil rights and political liberty).Kama Azaki zinahisi kudai tume huru ni jukumu la vyama vya siasa tuu zinajipotosha zenyewe.
Sisi wananchi,lazima tutambue tume huru ndio nyenzo ya uchaguzi huru na haki, uchaguzi huru na haki ndio mlinzi mkubwa wa kura yako,ndio msingi wa mamlaka kwa kiongozi umpendaye ,ndio mlinzi wa uzito wa kura yako kwa kiongozi umtakae,mara nyingi sisi wananchi aidha CCM, ACT , Chadema ,NCCR au chama chochote,hata wasio na chama huwa tunaona mambo ya tume huru ni mambo ya vyama vya siasa hii sio kweli.Haya mambo yanatuhusu sote.
Kupitia uwepo wa tume huru ya uchaguzi ,tutakuwa na uchaguzi huru na haki ,kupitia uchaguzi huru na haki tutapata kuchagua viongozi tunaowataka ,watakaochaguliwa kwa uzito wa kura zetu . Viongozi hawa watakuwa wanyenyekevu kwetu wananchi na watakuwa wawajibikaji na ataongoza baada ya yeye kupata baraka na mamlaka kutoka kwetu, soma ibara ya 8(a) katiba yetu ya 1977, Kiongozi huyo sababu amechaguliwa kwa uchaguzi wa haki atawiwa kututumikia kwa ustawi wetu sisi wananchi (Soma ibara ya 8 b ya katiba ).
Wananchi bila kujali vyama vyetu,lazima tutambue kuwa serikali ya sasa haitaki kusikia neno tume huru sababu ya maslahi yao binafsi ,sababu wanahisi ndio njia ya wao kupoteza vyeo vyao,ndio maana kwa kujihami wanatangaza kufuta mfumo wa vyama vingi kwa njia mbali mbali .
a)kuzuis mikutano iliyopo kisheria kwa vyama vingine.
b)Kufungulia kesi viongozi vyama pinzani.
c).Kutumia polisi katika chaguzi.
d)Kununua wawakilishi wa wananchi kutoka vyama vingine.
e) Kufanya figisu katika chaguzi (Manipulations /riggings).
f)kutosikia neno tume huru .
g) kutishia watu wenye mlengo wa upinzani.
Lengo ni kuifanya Tanzania kuwa nchi ya chama kimoja "De facto single party state " ndio maana kauli kila siku ,tutafuta vyama pinzani na wananchi tunacheka ,kufuta vyama pinzani ni kufuta mfumo wa vyama vingi.
Na hayo Serikali hii ya CCM inaweza kuyatimiza bila uwoga kama sote tukiendelea kutoa meno nje na kuchekacheka.Pius Msekwa katika kitabu chake cha "The Reflections on the first Decade of Multiparty Politics in Tanzania" kurasa ya 327 "The future of Multipartism in Tanzania will depend on these three factors a)The Strength and seriousness of Political parties (b) the delivery of free and fair elections (c) A vibrant Parliament . Yaani uhai wa vyama vingi unategemea vitu vitatu uimara na nguvu kwa vyama pinzani (umoja),(b) uchaguzi huru na haki (c)Bunge machachari.
Yaani kama vya pinzani visipokuwa imara na mshikamano kipindi hiki kwa kuratibu vyema inclusiveness ya kudai Tume huru na namna nzuri ya kushiriki uchaguzi mkuu.Hakika Demokrasia yetu itazikwa rasmi.
Hatupaswi kuombea hayo ,tunatumai mambo yataenda sawa sawia kwa vyama vyetu kuwa imara ,kuwa na uratibu imara pia kuzidisha mahusiano mazuri miongoni mwao.
Shukrani.
Abdul Nondo.
0772151432.
abdulnondo10@gmail.com
Sent using Jamii Forums mobile app