Tuandamane mpaka ikulu tarehe 30 August 2008

MiratKad

JF-Expert Member
May 2, 2008
294
3
Kuna Watu Wanaota Tukatane Mapanga Angalau Wapate Ukimbizi Mahali Fulani Hali Ya Uchumi Sio Salama Hili Ndilo Swala Lenyewe Au

Nani anaota wewe, unafikiri kila mtu anatafuta ukimbizi au makata tamaa kama wewe. Wengine wanaona mbali kama huwezi kuonyesha uzalendo kwa vitendo we kaa uangalie, na siku ikifika itabidi ujifinye kama unayoyaona yanatokea kweli ama la. Haya ni maandamo ya amani. Mapanga umeyatoa wapi?
 

Gembe

JF-Expert Member
Sep 25, 2007
2,502
153
Gembe to hell with your masters

Shalom!
you had good idea,ila hii imeharibu kila kitu.You just go to hell yourself..Nimebaki kumsaidia marehemu Wangwe na sitakuwa mtumwa wa kuwatetea mnaotaka nyie iwe
 

Gaijin

JF-Expert Member
Aug 21, 2007
11,815
5,244
wazo zuri sana iwapo litafanyika kwa amani.
tatizo ahpa JF watu wengi wapo nje ya nchi na wanaogopa kusema watu wakaandamane wakati wao hawatakuwepo na likitokea tatizo wakawa na jukumu.
 

Mavanza

Member
Jun 12, 2008
38
0
Watanzania wapo tayari na ugumu wa maisha umekwisha wafundisha. Shida kubwa ni viongozi wa kuipindua nchi, hao ndio wanakosekana. Unajua viongozi wetu wa upinzani wame-loose credibility kwa watu kutokana na malumbano yao yasiyoisha. Watanzania wako tayari kuingia barabarani lakini waanzie wapi? Hii inanikumbusha maandamano ya wanafunzi wa chuo kikuu mwaka 1992 (kama sijakosea) yaliyoongozwa na Mbatia na wenzake kwenda ikulu wakidai madaktari waliofungwa Ukonga waachiwe.

Hakuna njia nyingine ya kuikomboa nchi hii isipokuwa nguvu ya wananchi ya kuingia barabarani. Tume-debate sana, lakini amini usiamini hoja za EPA, Richmond ndio zimefikia mwisho wake na hakuna atakayechukuliwa hatua na watanzania tutakaa kimya.

Na hata siku moja usitegemee kuwa mapinduzi yanafanywa na watu millioni, ni watu wachache tena wa mijini walitayari ku-dare ndio wanaoleta mapinduzi. Tutafute kianzio tu ili mabadiliko yaje, ila tukumbuke kuwa ni lazima watokee watakao tolewa kafara kwa manufaa ya Tanzania bora baadaye.

Naunga mkono isipokuwa nina shaka na tarehe kwani hili ni jambo kubwa linalohitaji mipango.
 

Mnyisunura

Member
Aug 3, 2008
69
7
Mimi naamini mambo yote yanawezekana. Watu wanajua matatizo yaliyopo. Hata hivyo nadhani bado kidogo watu hawajaonja jote ya jiwe. Mtu anayeuliza kwanini tuandamane maanayake hana matatizo. Itakapofika kuwa watu wengi wanahesabu siku za kula au hata wewe hivyo vijisenti ulivyonavyo havifiki mwisho wa mwezi na huna mtu wa kumkopa wala namna ya kuvipata, watu wakikushauri tuandamane utakubali. Jamani Yanayotokea zimbabwe ni makubwa ni kuwa mtu unatoka kwenye nchi ya asali na maziwa halafu ghafla inakuwa jangwa na msababishi upo. Zimbabwe leo hakutamaniki lakini ni sababu ya uongozi mbovu. Hawa nugu zetu wa kenya nao kwa watu waliokaribu nao ni kuwa walikuwa kwenye hali ngumu ndo maana wakafikia hali ile.
Watanzania bado kidogo. Ikifika wakati watu watatia adabu wenyewe. Ukitaka kujua kuwa bado hebu angalia ziara za huyu Vasco Dagama vijijini watu wanavyompaparikia! Kwakweli nachukia sana tena sana kwa herufi kubwa! Ilitakiwa watu wasiende kwenye mikutano yake waendelee na shughuli zao na ikiwezekana ni vibaraka wake tu wawepo kwenye mikutano.
Kama alivyosema mkuu mmoja. Mapinduzi ni kazi ya kujitolea. Kama hata maafisa usalama ni corrupt! Ujue hatuna nchi na wala viongozi. Wasiwasi wangu ni kuhusu hawa wapinzani wetu. Bado mtazamo wao ni w Kidar-es salaam tu. Kumbukeni wapigakura wako vijijini.
Tatizo jingine ni taarifa! Nakumbuka wakati fulani nilipokuwa kahama magazeti tulikuwa tunayapata siku moja baada ya gazeti kutoka. Hata hivyo yalikuwa yanaishia mjini tu! Kibaya zaidi hata redio zilizopo sanasana ni TBC zao hizo.
Nawapongeza wanachadema kwa kazi kubwa waliyoifanya mwakajana hasa baada ya kusimamishwa ZITTO bungeni. Nilihisi taswira ya watanzania inabadilika sasa ingawa bado inazimwa. Hivyo kazi kubwa tunayotakiwa kufana sasa ni kama ile waliofanya mwakajana akina zitto kuzunguka nchi nzima kueleza uozo uliopo. Hilo linahitaji sehemu ya kusimamia na kujibu mbele ya farao!
 

Ben Saanane

JF-Expert Member
Jan 18, 2007
14,588
18,045
Tunaandamana juu ya nini?


wanafunzi wa elimu ya juu wanabaguliwa kupewa mikopo.


Akina mama wanakufa hospitalini kwa kukosa Nyembe wakati wa kujifungua.

wamachinga wananyanyaswa bila kutoa suluhisho la matatizo yao.

Kumlazimisha JK na serikali yake kumchukulia hatua rais Mstaafu na watuhumiwa wa ufisadi waliokua na walioko serikalini.


Pia,kulaani kauli ya Rais eti Watanzania wavumilie njaa na maisha makali,kauli inayopingana na kauli mbiu yake iliyomwingiza madarakani ya maisha bora kwa kila mtanzania.


Hata hivyo,maandamano yasiyokua na kiongozi yanaweza kuwa ni mkusanyiko wa genge la wahuni kwani waandamanaji hawatakua wakiandamana kutimiza lengo maalum bali kupiga kelele na kuchochea Ghasia
 

Shalom

JF-Expert Member
Jun 17, 2007
1,315
112
Mlichokifanya wewe na Mag3 ndicho cha maana ...Lakini kina Nziku na wengineo waliotangulia walimkatisha tamaa ndugu yetu Shalom...Sasa hapo ndio unapojuwa hii jf...Ndugu yangu kama hayajakukuta basi huwezi kusema kitu...Ukweli uko wazi.

Jmushi mimi sikatishwi tamaa na hao watu kwa sababu najua kanuni za kimungu hivyo hao wanadamu si rahisi kunikatuisha tamaa. hebu angalia chini hata mungu mwenyewe anajua jinsi umoja unavyoweza kufanya kazi kwenye Mwanzo 11:1-7 na anakili kuwa mkiwa na umoja hamna kitu kitakacho wasimamisha. Nimetumia basic english version

11:1 And all the earth had one language and one tongue.
11:2 And it came about that in their wandering from the east, they came to a stretch of flat country in the land of Shinar, and there they made their living-place.
11:3 And they said one to another, Come, let us make bricks, burning them well. And they had bricks for stone, putting them together with sticky earth.
11:4 And they said, Come, let us make a town, and a tower whose top will go up as high as heaven; and let us make a great name for ourselves, so that we may not be wanderers over the face of the earth.
11:5 And the Lord came down to see the town and the tower which the children of men were building.
11:6 And the Lord said, See, they are all one people and have all one language; and this is only the start of what they may do: and now it will not be possible to keep them from any purpose of theirs.
11:7 Come, let us go down and take away the sense of their language, so that they will not be able to make themselves clear to one another.
 
0 Reactions
Reply
Top Bottom