VUTA-NKUVUTE
JF-Expert Member
- Nov 25, 2010
- 6,140
- 18,004
Sisi wananchi tunataka kuwa katika upande mmoja.Upande wa kuamini au wa kutoamini. Lakini,tunaitegemea Serikali ituaminishe au itufanye tusiamini. Serikali ya chama chetu cha Mapinduzi inazunguka.Inajikanyaga.Inajiuma.Inazunguka mbuyu tu.Haina kauli moja.Haina usawa wa hoja na majibu. Inapishana kutoka huyu hadi yule. Kizungumkuti. Mchafukoge.
Ni kuhusu UDA. Wapo wanaosema mauzo yamefanyika. Mnunuzi ni Saimon Group inayomilikiwa na Robert Kisena. Wapo wanaosema kuwa mauzo hayakufanyika na Kisena na Kampuni yake hawana hata hisa moja. Wapo wanaosema kuwa suala hili lipo TAKUKURU kwakuwa kuna harufu ya rushwa. Wapo wanaosema Serikali itakuja na jibu moja.Wapo waliokana uwepo wa UDA katika Wizara zao. Tuamini au tusiamini?
Tuamini au tusiamini kuwa Serikali haijui kinachoendelea na kilichotokea UDA? Suala hili la UDA linaiaibisha Serikali na chama cha Mapinduzi.Kinaanika udhaifu wa kiuongozi katika Taasisi na Idara za kiserikali zinazoshughulika na UDA katika maisha ya kila siku.
Wananchi wa Tanzania wanataka kujua.Kujua kuhusu UDA.Kujua kuhusu kilichotokea na kinachoendelea UDA. Kumjua mmiliki,mnunuzi,mwendeshaji na kadhalika. UDA haina ukubwa wowote wa kuogofya. Haina ukubwa wowote wa kuwafanya viongozi wetu wapishane katika kauli. Ishughulikiwe haraka.
Tunataka kuamini kuwa Serikali ni moja na inaweza.
Mzee Tupatupa wa Lumumba,Dar es Salaam