Mwanakulipata
JF-Expert Member
- Jul 17, 2018
- 718
- 1,202
Habari wana JF, katika harakati za kutafuta ajira unaweza kupata nafasi ya kufanya interview kwa ajili ya ajira, share nasi interview ambayo hutokaa huisahau katika maisha yako
Mimi yangu ilikuwa hivi, baada ya kumaliza elimu ya sekondari na kutofanikiwa kuendelea na masomo kwa muda nikaamua nijikite kutafuta ajira, nilifanikiwa kufanya interview 2 ambazo sitokaa nizisahau
Ya kwanza ilikuwa tigo customers service wenyewe wanaita PCCI, nilikuwa na wenge sijawahi kufanya hizo mambo niliwahi mapema kabisa nilivyofika kwenye kile chumba nikakutana na wale wanaohoji wa 3 nikasema hapa nikichomoka sijui, nikaulizwa kwanini unaitaka hii kazi nikajibu kwa kuzunguka weee mara maisha ya mtaani magumu mara sina hela walibaki wanacheka tu na ndo ikawa tamati yangu
Ya pili kuna bro alikuwa Engineer alinifanyia mpango kwenye kampuni flani hivi ya ujenzi walikuwa wanataka Storekeeper, nikajua nitakuwa pekee yangu kufika nakuta tupo 2 mimi na mdada kuna jamaa mfanyakazi akasema tulitegemea aje mmoja lakini kama mpo wawili sio mbaya tutafanya ka interview kadogo, akaanza yule mdada baadae nikafata mimi baada ya mahojiano madogo nikatoka nikaambiwa nisubirie nje then akatoka akanambia kusema ukweli mdogo wangu interview umefaulu lakini wewe bado mdogo sana muachie yule dada hii kazi anamajukumu nikamwambia bro mimi mwenyew naitaka hii kazi akaondoka nilichukia nikamfikishia ujumbe yule bro aliyenipa mchongo akasema huyo jamaa anapenda sana wanawake huenda aliona ampe yule dada kwa kusudi flani.
Wewe yako unayoikumbuka ilikuaje?