Tuacheni udhalilishaji, imetosha sasa

Tuacheni udhalilishaji, imetosha sasa

Juliana Shonza

JF-Expert Member
Joined
Dec 19, 2012
Posts
2,009
Reaction score
1,607
Yapo mambo mengi yamekuwa yakiendelea katika kipindi hiki, ambapo mengi katika mambo hayo ni ya hovyo, machafu na yasiyofaa katika jamii lakini yanahalalishwa kwa jina SIASA. Mambo yenye kushusha heshima ya mtu, kudhalilisha utu wake na kufedhehesha jamii yake siku hizi hayakemewi tena, sio na watu wenyewe ama taasisi bali hata Serikali yenyewe imekalia kimya mambo hayo na jamii wameyapa jina jipya, hauitwi tena UDHALILISHAJI bali inaitwa SIASA CHAFU.

Kwa muda mrefu, binafsi nimekuwa nikitukanwa sana hapa jamvini, tena na watu wenye heshima zao na wengine nawajua kwa sura na majina halisi lakini hata hawashtuki, nao huingia kwenye mkumbo huu wa matusi, kunidhalilisha na kunishushia heshima..wakati mwingine tunalazimika kuvumilia kwa sababu ndivyo ilivyo jamii yetu lakini hakika ni lazima tukemee tabia hizi zinazoimarika ndani ya jamii yetu...Watanzania walikuwa ni watu wenye kutolewa mfano kwa kuheshimiana, kupendana na kuishi kijamaa lakini hali ya sasa ni ya mazungumzo ya chuki, uhasama, kudhalilishana na kuvunjiana heshima.

Nimeiona VIDEO inayozunguka kwenye mitandao ya kijamii, ikimdhalilisha Mama Regina, huyu ni Mwanamke mwenzangu lakini pia ni kama Mama yangu mzazi kwa umri wake na mtu mwenye heshima ya kipekee katika jamii yetu, si jambo jema hata kidogo, Mimi nalipinga jambo hili kwa namna yeyote ile itakavyotafsiriwa.

Hii sio siasa, na nawaonya Vijana wenzangu wa CHAMA CHA MAPINDUZI (CCM) ikiwa wao ndio wanaozisambaza video hizi, wajue wanafanya makosa kisheria na ni kukosa adabu na heshima kwa wazazi wetu. Nimewataja Vijana wenzangu wa CCM kwa sababu VIDEO hiyo nimeiona kwenye simu ya mmoja wao akidai ametumiwa na kijana anayeitwa Peter Kasera (ambaye nae ni kijana wa UVCCM) hizi sio tabia za wanachama ama Vijana wa CCM, MNATUDHALILISHA. Na nimeamua kukutaja kwa jina halisi ili uone haya kokote ulipo na ujutie kitendo chako, ikiwezekana uombe radhi kwa kitendo hicho.

Lakini pia hawa wapiga picha wanaokuwepo kwenye shughuli za CHADEMA na UKAWA hivi mnaishi nao vipi..? maana event ile ni ya "wanamabadiliko" imekuwaje VIDEO ile imevuja..? It's obviously kuwa mpigaji picha deliberately ameamua kuitoa kwa maslahi yake na ya wale anaowajua yeye.

Maoni yangu:
Watu hawa wote wachukuliwe hatua, kuanzia yule aliyefanya kitendo kile, aliyevujisha VIDEO pamoja na hawa wanaoendelea kusambaza..kwani ni hatua ya juu kabisa ya UDHALILISHAJI aliyofanyiwa Mama Regina.

NB:
Sitoiweka VIDEO hiyo hapa, na siitaji mtu yeyote katika uzi huu ama mwingine aweke VIDEO hiyo ama yenye mfano wa hiyo, hata kama ni SIASA jamani kuna maisha baadae..TUACHE UDHALILISHAJI, imetosha sasa.
 
Kwani hiyo video ina maudhui gani?
ili tupate picha halisi...
 
Vipi na matusi na dhihaka za Abdallah Bulembo na Mwigullu Nchemba?! Nape na Musukuma je vipi na wao?! Wewe Juliana ulikuwa kinara wa matusi dhidi ya Slaa ila kama kweli unaanza kuingia kwenye u-motherhood na kutambua ushenzi wenu ni wa hovyo na kipumbavu basi nakusamehe!!

Hakuna Mkutano wa CCM uwe wa mbunge au ******** unafanyika bila matusi,tena CCM mmefikia hatua ya kuandaa matusi na kuwalipa watu waje wayanene huku mkiwalipa na kulipia TV ionyeshe mattusi!!
 
Yapo mambo mengi yamekuwa yakiendelea katika kipindi hiki, ambapo mengi katika mambo hayo ni ya hovyo, machafu na yasiyofaa katika jamii lakini yanahalalishwa kwa jina SIASA. Mambo yenye kushusha heshima ya mtu, kudhalilisha utu wake na kufedhehesha jamii yake siku hizi hayakemewi tena, sio na watu wenyewe ama taasisi bali hata Serikali yenyewe imekalia kimya mambo hayo na jamii wameyapa jina jipya, hauitwi tena UDHALILISHAJI bali inaitwa SIASA CHAFU.

Kwa muda mrefu, binafsi nimekuwa nikitukanwa sana hapa jamvini, tena na watu wenye heshima zao na wengine nawajua kwa sura na majina halisi lakini hata hawashtuki, nao huingia kwenye mkumbo huu wa matusi, kunidhalilisha na kunishushia heshima..wakati mwingine tunalazimika kuvumilia kwa sababu ndivyo ilivyo jamii yetu lakini hakika ni lazima tukemee tabia hizi zinazoimarika ndani ya jamii yetu...Watanzania walikuwa ni watu wenye kutolewa mfano kwa kuheshimiana, kupendana na kuishi kijamaa lakini hali ya sasa ni ya mazungumzo ya chuki, uhasama, kudhalilishana na kuvunjiana heshima.

Nimeiona VIDEO inayozunguka kwenye mitandao ya kijamii, ikimdhalilisha Mama Regina, huyu ni Mwanamke mwenzangu lakini pia ni kama Mama yangu mzazi kwa umri wake na mtu mwenye heshima ya kipekee katika jamii yetu, si jambo jema hata kidogo, Mimi nalipinga jambo hili kwa namna yeyote ile itakavyotafsiriwa.

Hii sio siasa, na nawaonya Vijana wenzangu wa CHAMA CHA MAPINDUZI (CCM) ikiwa wao ndio wanaozisambaza video hizi, wajue wanafanya makosa kisheria na ni kukosa adabu na heshima kwa wazazi wetu. Nimewataja Vijana wenzangu wa CCM kwa sababu VIDEO hiyo nimeiona kwenye simu ya mmoja wao akidai ametumiwa na kijana anayeitwa Peter Kasera (ambaye nae ni kijana wa UVCCM) hizi sio tabia za wanachama ama Vijana wa CCM, MNATUDHALILISHA. Na nimeamua kukutaja kwa jina halisi ili uone haya kokote ulipo na ujutie kitendo chako, ikiwezekana uombe radhi kwa kitendo hicho.

Lakini pia hawa wapiga picha wanaokuwepo kwenye shughuli za CHADEMA na UKAWA hivi mnaishi nao vipi..? maana event ile ni ya "wanamabadiliko" imekuwaje VIDEO ile imevuja..? It's obviously kuwa mpigaji picha deliberately ameamua kuitoa kwa maslahi yake na ya wale anaowajua yeye.

Maoni yangu:
Watu hawa wote wachukuliwe hatua, kuanzia yule aliyefanya kitendo kile, aliyevujisha VIDEO pamoja na hawa wanaoendelea kusambaza..kwani ni hatua ya juu kabisa ya UDHALILISHAJI aliyofanyiwa Mama Regina.

NB:
Sitoiweka VIDEO hiyo hapa, na siitaji mtu yeyote katika uzi huu ama mwingine aweke VIDEO hiyo ama yenye mfano wa hiyo, Mods stay alerted...hata kama ni SIASA jamani kuna maisha baadae..TUACHE UDHALILISHAJI, imetosha sasa.
Daah Vijana wa yote yanatokana na migogoro ya ndani ya Ukawa mpaka wanamdharirisha Mama Regina hakika dhambi baada ya uchaguzi wataijutia na inaweza kusababisha Mama Regina kugombana na Vijana wa Chadema wanaomfanyia mambo ya kiuni kiasi hiki.....
 
Kiukweli hizi siasa zinapokwenda si mahala salama, kwanini tunadhalilishana kiasi cha kutoa video ambayo mwanamke mwenzangu anafanyiwa kitu kama hicho,hii sio sawa kama ungekua wewe au ni mzazi wako ungeiweka? tuache hizo mambo. alie record hiyo video achukuliwe sheria
 
Aliyempiga dole Mama Lowassa ni kijana wa CHADEMA, tangu Lowassa aje CHADEMA kuna wanachama wenzetu wanafanya kila wawezalo ili wamuangushe Lowassa. Hii siyo adabu hata kidogo, yule ni sawa na Mama zetu wengine tunaoishi nao kwenye jamii zetu.

Kama humtaki Lowassa bora ukae kimya au ukimbie kama walivyokimbia wanachama wengine wakaenda fisiemu. Jana mumempiga dole, najua ipo siku nyingine mutamfanyia kitu kikubwa zaidi, sijui munategemea nini mtu aliyewahi kupigwa dole hadharani siku moja akisimama kama 1st lady.
 
Udhalilishaji mbaya sana tilianza kusikia kua vijana wanapewa viroba watu tukabisha lakini tukaletewa ushahidi kumbe kweli wanawapa vijana hizo pombe kali hatari baadae tena ushahidi mwingine wanamdhalilisha mama Lowassa hii si alama nzuri hata kidogo kama Watanzania
 
Hakika umenena maneno yenye hekima... Maana kuna maisha baada ya uchaguzi, kuwa tofaut ki itikadi isiwe chanzo cha kudhalilishana na kutoheshimiana.
Nakukubalia kabisa kuwa huyo aliyehusika kumdhalilisha mama Regina Lowassa na huyo aliyetuma hiyo video mpaka kusambaa wachukuliwe hatua za kisheria
 
huo ni mpango mkakati wa vijana wa chadema ambao nafasi zao zimechukulia na kundi ambalo ndio vinara wa kampeni za lowassa kitu ambacho kimewafanya vijana hao kukosa maslahi na kuamua kutoa hiyo video kama pay back. tunawaomba muache hiyo tabia yakudhalilisha mama zetu na kututukana wanawake.jeshi la polisi tunaomba mfatilieni alie record ile video achukuliwe hatua.
 
Kwasababu mwanamke mwenzako amefanyiwa hivyo ndo umekuja kukemea hapa?
Wakati Lowasa anadhalilishwa ulikuwa wapi?
CCM mmeanzisha hizi siasa. Anza kuwakemea Nape na wenzake.
 
Hapa kuna jambo,huyu dada alieanzisha hii mada si wa kumwamini alishajivunjia heshima yake,hastahili hata kuwa kiongozi,na hii mada ameianzisha kwa malengo anayoyajua
 
I wish ningekuepo eneo la tukio kwa maana iyo ingekuwa kesi yangu ya kwanza ya kujeruhi mpaka kutaka kuua, ccm mnasiasa za kipuuz sana na nyinyi ndio mnaoshangalia huu ujinga na ndio maana hawa vijana wanafanya upuzi kwa sababu viongozi wakubwa wanafanya ujinga huo huo kiongozi anapomtukana mtu na heshima zake hana tofauti na jambo alilolifanya huyo kijana mfike mahali mjitafakari huu sio wakati wa ushenzi na upuuzi mliwanyima watz elimu na ndio maana hawa wanaofanya haya wanaona ni sawa tu.
 
Udhalilishaji umeuasisi wewe ulipotua rasmi CCM! Umesahau? Tumeshavumilia tumechoka sasa tutapambana!

Natoa onyo kali kwa FaizaFoxy na wahuni wenzake waache kuchezea utu na dini za watu! Tunawaangalia kwa umakini mkubwa sana na hilo walielewe! Hatutothubutu kuwaacha waendelee kudhalilisha utu wa mtu eti kwa sababu ya imani tofauti na itikadi tofauti! Tusije kulaumiana!!
 
Last edited by a moderator:
Some time mtu anadhalilishwa kulingana na vile anavyojidhalilisha yeye binafsi.

Ukiangalia mara nyingi vitu unavyopost hapa jukwaani Dada yangu wewe na kulingana na Credibility uliyokuwanayo huko nyuma kabla hujajiunga na ccm, ni kweli kuwa ulikuwa ukijidhalilisha, hivyo kwa mtu kukudhalilisha pia ilikuwa kanakwamba ni sawa tu.

Inaeleweka wazi Mama Regina Lowassa ni Mama Mstaarabu, Mtulivu na ambaye hajawahi kukwaruzana na watu. Yeyote aliyeweka video hiyo ya kumdhalilisha kwasababu za kisiasa, kwanza anjikosea heshima mwenyewe, kumkosea heshima Mama Regina na Jamii kwa ujumla. Naamini kama kunakitendo chochote cha kudhalilisha kwenye video hiyo, basi kimetokea kwa bahati mbaya. Hii ni kama mimi kutembea mtaani nikiwa nimesahau kufunga zipu hivyo kuacha maungo au nguo yangu ya ndani ikionekana. Kitendo kama hiki ni bahati mbaya, yeyote atakayetumia nafasi hiyo kunidhalilisha ni juu ya uelewa wake na wazazi wake waliomzaa.

Kama umeamua kutumia kitendo hicho cha vijana wa ccm kwa upuuzi walioufanya ili kuomba radhi ni vyema. Lakinu naamini hutatumia kitendo hicho kama kinga ya wewe kuendelea kudhalilisha watu hapa kwa minajiri yoyote ile.

Mtu mzima hujikosoa, Naamini umejitathimini na kujitambua. Ni juu yako kurudi kwenye Maadili mema uliyolelewa na wazazi wako na jamii ya watu uliyokuwako hapo awali.(Chadema) Hongera angalau kwa leo.

BACK TANGANYIKA
 
wakiwa wameshindwa hata walau kumstiri; mama wa watu??? mpaka wamevujisha video za huyo mama??? migogoro yenu ndo inazidi kwadhoofisha; mjipange upya tar 25 magufuli anapewa nchi yake
 
Kama hujui basi tambua hilo, siasa chafu za mitandaoni na majukwaani zinafanywa na Makada wa CCM kwa uratibu wa CCM makao makuu, hakuna kiongozi yoyote wa juu wa CCM aliyekemea, na zaidi wanafurahi na kushangilia kabisa.
Sahara media kupitia StarTv, RFA, Kiss Fm, pia Radio Uhuru na Clauds media ndio vinara wa hii michezo.

Nina uhakika kabisa hata wewe Juliana Shonza unajua hayo tena huenda hata inayafurahia ila hapa umekuja kutuzuga tu, ili ujifanye haulewi hayo.

Kwa mfano siku ya Jana, Mwigulu Nchemba alikuwa Mbeya na wewe ulikuwepo, alichokisema jukwaani ni kile kile ambacho kinaenezwa mitandaoni, lakini kwa furaha na hamasa wanaCCM walishangilia, sikuona any negative reaction toward to such speech kutoka kwako au kada mwingine wa CCM.
 
Last edited by a moderator:
vijana wamedhaliwa wakati wa giza mimi ni ccm asilia siasa kama hizi Hatuna tunkaosa radhi kwa mama na ya dunia kushindwa kumsitiri mama yetu..
 
Naoma wameshukiwa tu CCM, ila nadhani matusi na dharau yapo kila sehemu wale waliosema WATANZANIA WAKIMCHAGUA LOWASSA, WAKAPIMWE AKILI!?? that means wanaomshabikia LOWASSA hivi sasa wote akili zao zina matatizo, ni bora ukamtusi na kumdharau mmoja, kuliko kuwatusi na kiuwadharau wengi amabao wao ndio wanakupa kula yako ya kila siku. Huku ndiko kudharauliana, wananchi tunafanywa kama watu tusiokuwa na akili timamu
 
Uchuguzi una mengi Kama una Roho nyepesi wallah unajitundika mume anadhalilishwa Kwa kujitakia maana Ni ukweli ila Kwa upande hasa wa huyu Mwana mama mie Leo imeniuma kabisa na Hawa vijana wa Chadema Hawa Kama hamumpendi Lowassa msimdhalilishe Mkewe!
 
Back
Top Bottom