Kilemakyaaro
JF-Expert Member
- Jul 19, 2016
- 5,050
- 5,078
Hivi majuzi tu tumeona Rais Magufuli akiwateua wapinzani kushika nyadhifa nyeti Serikalini. Tumeshuhudia Prof. Kitila akipata uteuzi kuwa Katibu mkuu wa Wizara nyeti, Mama Anna Mghwira nae kapata Ukuu wa Mkoa na Dr. Slaa akateuliwa kuwa Balozi. Kwa ujumla ukiangalia historia za watu wote hawa ni nzuri katika vyama vyao na hata Taifa, wameonyesha utendaji mzuri walipokua ambao nafikiri ulimshawishi Rais kuwapa nafasi hizo.
Ila pamoja na hayo ukweli unabakia palepale kua siasa hususan ya Afrika, uwe unatoka chama Tawala au upinzani imezungukwa na utafutaji wa maisha kwa maana kuwa wanasiasa wanaichukulia kama kazi inayowaingizia kipato hivyo mwanasiasa akipata nafasi ndio maana hata waliomzunguka wanafurahi, wanafanya tafrija maana wanajua upatikani wa rizki utaongezeka.
Sasa naomba kuuliza ukiweka uchama pembeni, kama kuna mtu ambaye humu JF nani ambaye leo angekuwa mtoto wa Dr. Slaa au Anna Mghwira au Kitila Mkumbo angeweza kumshauri au kumkataza huyo mzazi wake akatae hiyo nafasi ya uteuzi, wakati baadae kuna maisha na majukumu ya kifamilia!