Tuache unafiki, tuseme kweli...

Kilemakyaaro

JF-Expert Member
Jul 19, 2016
4,366
2,000
Hivi majuzi tu tumeona Rais Magufuli akiwateua wapinzani kushika nyadhifa nyeti Serikalini. Tumeshuhudia Prof. Kitila akipata uteuzi kuwa Katibu mkuu wa Wizara nyeti, Mama Anna Mghwira nae kapata Ukuu wa Mkoa na Dr. Slaa akateuliwa kuwa Balozi. Kwa ujumla ukiangalia historia za watu wote hawa ni nzuri katika vyama vyao na hata Taifa, wameonyesha utendaji mzuri walipokua ambao nafikiri ulimshawishi Rais kuwapa nafasi hizo.

Ila pamoja na hayo ukweli unabakia palepale kua siasa hususan ya Afrika, uwe unatoka chama Tawala au upinzani imezungukwa na utafutaji wa maisha kwa maana kuwa wanasiasa wanaichukulia kama kazi inayowaingizia kipato hivyo mwanasiasa akipata nafasi ndio maana hata waliomzunguka wanafurahi, wanafanya tafrija maana wanajua upatikani wa rizki utaongezeka.

Sasa naomba kuuliza ukiweka uchama pembeni, kama kuna mtu ambaye humu JF nani ambaye leo angekuwa mtoto wa Dr. Slaa au Anna Mghwira au Kitila Mkumbo angeweza kumshauri au kumkataza huyo mzazi wake akatae hiyo nafasi ya uteuzi, wakati baadae kuna maisha na majukumu ya kifamilia!
 

MIGNON

JF-Expert Member
Nov 23, 2009
3,542
2,000
Wapo wengi tu!!Ulishawahi kusikia neno "Maskini jeuri?".Si watu wote wanapendelea vyeo hasa vile ambavyo vinawafanya wasutane na dhamira zao.
Unachotakiwa kuelewa ni kuwa sio wapinzani wote ni wapinzani kweli,wengine wanatusaidia kuangalia usalama wetu kwa mapana yake.
 

Kilemakyaaro

JF-Expert Member
Jul 19, 2016
4,366
2,000
Hiyo user name yako nasikia ndiyo chanzo cha neno "Kilimanjaro" baada ya wazungu kukurupuka kama "BWANA YULE"
Inawezekana kweli lkn jikite kwenye mada wee Kitila au Slaa angekua babaako ungemshauri akatae ile teuzi, alaf wakati huohuo ukumbuke kuwa Familia ya Slaa wanakua nao wana hadhi ya kidiplomasia kuanzia pasi za kusafiria mpaka kila kitu
 

Mgibeon

JF-Expert Member
Aug 7, 2011
8,926
2,000
Mkuu tupo wengi tu, binafsi siwezagi kabisa kabisa kupingana na nafsi yangu, nishaacha deal moja kubwa sana na cheo kizuri kwaajili tu ya misimamo yangu!

Hujiulizi kwanini Mtu kama Nyerere alikufa maskini? Unafikiri alishindwa "kujipongeza"? Angeamua hata UDSM ingekua mali yake!

Achana kabisa na Dhamira!!!
 

Kilemakyaaro

JF-Expert Member
Jul 19, 2016
4,366
2,000
Mkuu tupo wengi tu, binafsi siwezagi kabisa kabisa kupingana na nafsi yangu, nishaacha deal moja kubwa sana na cheo kizuri kwaajili tu ya misimamo yangu!

Hujiulizi kwanini Mtu kama Nyerere alikufa maskini? Unafikiri alishindwa "kujipongeza"? Angeamua hata UDSM ingekua mali yake!

Achana kabisa na Dhamira!!!
Mpo wachache sana kama unasema kweli lkn mie sutaki kuwa mnafiki ningeshindwa
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom