Tuache maneno tuweke ushahindi, njaa hii hapa shibe hii hapa

tikatika

JF-Expert Member
May 6, 2011
2,330
4,115
Kuna sintofahamu imetawala, na kuna uhalisia umetupata. Tunashindwa kuwa na kauli moja kama Taifa. Hebu njoon hapa tuweke uhalisia wa hali halisi ya chakula.

Je, kuna njaa au hakuna njaa hapa Tanzania?

Weka ushahidi wa kile unachokiamini hapa baadaye tutapata picha kama njaa ipo au haipo.

Kwa wale walio vijiji au mashambani weken picha za ukame au mazao kukauka.

Kwa wale tulio mijini tuweke bei ya vyakula tuweke na tofauti ya hapo kabla.

Naanza mimi kutoa mfano. Hapa Dar es salaam unga kilo ilikua sh 800 kwa sasa ni sh 1600.

Mchele safi ulikuwa 1600 kwa sasa 2400.

Kwangu mimi hii ndio njaa yenyewe. Maana njaa sio lazma chakula kikosekane sokoni ila ni pale mimi nitakapo kosa uwezo wa kumudu bei maana kipato changu ni kile kile hakijaongezeka. Kwa lugha rahis demand and supply vimegongana. Supply imekua ndogo kuliko demand.

Tukumbuke huko vijijini hutegemea chakula kama ndio hela yao na chakula chao . Akikosa chakula shambani usimwambie kanunue maana amekosa hela iliyokua shambani. Maana hutegemea avune kingine atunze huku kingine auze kwa kupata mahitaji mengine.

Nataraji kwa wale watakao tetea kuwa njaa hakuna wataweka bei za chini na mazao yalio stawi huko mashambani.

Kupitia hapa tutamwonyesha rais wetu uhalisia wa nchi yetu. Maana tukiwasubiri waandishi wa habari anasema wamenunuliwa. Lakn pia hata wao wanaweza kuogopa kulipoti njaa maana hawachelewi kuwaweka ndani.

Karibuni tulijenge taifa letu.
 
Mtoa mada uongo unakusaidia nini? Hivi kweli unga utoke 800-1600, mchele utoke 1600-2400?
Uhalisia uliopo ni kuwa kuna mchele chenga 1600 na hapo grade zinaenda zinapanda mpaka 2000-2200.
Eneo ninaloishi hapa Sinza nimenunua mchele mzuri grade 1 kwa tsh. 2000.

Sembe bei uliyotaja umeweka mbwembwe sio halisi.

Mwisho nakushauri acha chuki. Hata kama kuna njaa na ukame lakini vyakula havijapanda kiasi hicho.
 
Uku kwetu babat tulipata mahindi sana.na tumeuza nje ya nchi sana, mbaya atukuweka akiba.Tukisema tuna njaa hakika tutakuwa tunamkufuru Mungu.tuseme sisi ni wajinga!!! Atukujua kesho.naunga mkono hoja akuna njaa tz.
Unaongelea babati ipi?
 
Utakuwa unakula kwa baba na bei chakula huijui,Hongera yako
 
Uku kwetu babat tulipata mahindi sana.na tumeuza nje ya nchi sana, mbaya atukuweka akiba.Tukisema tuna njaa hakika tutakuwa tunamkufuru Mungu.tuseme sisi ni wajinga!!! Atukujua kesho.naunga mkono hoja akuna njaa tz.
Umeambiwa wapo wakulima hayo mazao ya chakula ndio anayategemea pia auze watoto waende Shule, matibabu na mahitaji mengine sasa nlitaka asiuze sehemu ya mazao yake?
 
Mtoa mada uongo unakusaidia nini? Hivi kweli unga utoke 800-1600, mchele utoke 1600-2400?
Uhalisia uliopo ni kuwa kuna mchele chenga 1600 na hapo grade zinaenda zinapanda mpaka 2000-2200.
Eneo ninaloishi hapa Sinza nimenunua mchele mzuri grade 1 kwa tsh. 2000.

Sembe bei uliyotaja umeweka mbwembwe sio halisi.

Mwisho nakushauri acha chuki. Hata kama kuna njaa na ukame lakini vyakula havijapanda kiasi hicho.
Simple commerce hiyo ya form II
Kama supply inakuwa ndogo demand inakuwa kuwa na bei kubwa.Huu ni msimu wa kulima sio wa kuvuna,aliweka stock ndio anatamba.sio uchawi wala kosa la Magufuli ni somo la commerce linatuambia hivyo.
Mmmesahau mwaka jana mlikuwa mnalia kuwa serikali inanunua mahindi kwa bei ya chini,mkataka watu waruhusiwe kuuza mahindi nje.
Kuweni watulivu,wenye serikali yao wamesema wanajua nini wanafanya
 
Mtoa mada uongo unakusaidia nini? Hivi kweli unga utoke 800-1600, mchele utoke 1600-2400?
Uhalisia uliopo ni kuwa kuna mchele chenga 1600 na hapo grade zinaenda zinapanda mpaka 2000-2200.
Eneo ninaloishi hapa Sinza nimenunua mchele mzuri grade 1 kwa tsh. 2000.

Sembe bei uliyotaja umeweka mbwembwe sio halisi.

Mwisho nakushauri acha chuki. Hata kama kuna njaa na ukame lakini vyakula havijapanda kiasi hicho.
Bukoba zile za rambirambi mlishapewa?
 
Screenshot_20170112-121703.png
FB_IMG_1484211246126.jpg

Sijasema kama kuna njaa,mi sijasema
 
Uku kwetu babat tulipata mahindi sana.na tumeuza nje ya nchi sana, mbaya atukuweka akiba.Tukisema tuna njaa hakika tutakuwa tunamkufuru Mungu.tuseme sisi ni wajinga!!! Atukujua kesho.naunga mkono hoja akuna njaa tz.
Sasa kama hamna akiba ndo mna njaa bro/sista
 
I
Uku kwetu babat tulipata mahindi sana.na tumeuza nje ya nchi sana, mbaya atukuweka akiba.Tukisema tuna njaa hakika tutakuwa tunamkufuru Mungu.tuseme sisi ni wajinga!!! Atukujua kesho.naunga mkono hoja akuna njaa tz.
... Ni hivi unategemea mkulima mwenye ekari 2 au 4 alime mahindi halafu akivuna asiuze je mahitaji mengine ya kifedha atajikimu vipi? Kama soko la ndani wanakopwa mazao na kumetokea bei nzuri nchi jirani, tena cash asiende kuuza? Yaaani bata mle nyinyi tuu mjini...

Kwa kanuni za nguvu ya soko (supply na demand); bei zikipanda sokoni lazima kuna upungufu wamazao ambao unaweza kuwa umesababishwa na uhaba mashambani (ukame) au kukatika kwa miundo mbinu ya usafirishaji! Kwa sasa bei zimepanda kutokana na uhaba mashambani uliosababishwa na ukame period!
 
Mtoa mada uongo unakusaidia nini? Hivi kweli unga utoke 800-1600, mchele utoke 1600-2400?
Uhalisia uliopo ni kuwa kuna mchele chenga 1600 na hapo grade zinaenda zinapanda mpaka 2000-2200.
Eneo ninaloishi hapa Sinza nimenunua mchele mzuri grade 1 kwa tsh. 2000.

Sembe bei uliyotaja umeweka mbwembwe sio halisi.

Mwisho nakushauri acha chuki. Hata kama kuna njaa na ukame lakini vyakula havijapanda kiasi hicho.
WE UPO TANDALE UZURI SWEET CORNER SIYO SINZA!
KWANINI WATU WALE MCHELE CHENGA KWA NINI WASILE MCHELE MZIMA?
 
Back
Top Bottom