Tuache kupotoshana, bongo kutafuta pesa online ni ngumu sana kutoboa, sidhani hata kama yupo anaeingiza milioni 20 kwa mwezi. Ni heri ufanye kilimo

NetMaster

JF-Expert Member
Sep 12, 2022
1,454
4,853
Kaka millard ni exception, katoka mbali sana huyu.

Nimekuwa nikiona baadhi ya vijana hasa hawa wa chuoni na wahitimu wenye kujua jua kutumia vilaptop wanapotoshana mambo ya youtube, blogging, sijui app, adsense, n.k. kwamba kuna pesa

Ni kweli haya mambo kwa wenzrtu huko yanalipa na watu wamebadili maisha lakini kwa bongo hii Bin No!

Kwa bongo kutoboa online ni ngumu sana, utaona tu picha zao insta ila maisha halisi ni tofauti sana, ukifatilia wale wenye nazo wanaona aibu hata kuweka wazi jinsi wanavyozipata (kushare picha za uchi kwenye account za fb wanazoziiba, kufoji vitambulisho kutapeli watu, tuma kwa ile namba, ponzi schemes, n,k).

Ni heri ufanye kilimo, tunawaona watu wamechana msamba.

Ni heri ufungue mgahawa, tunawaona watu wana range zao za milioni 200

Ni heri ufungue duka lako la hardware, mdogomdogo una grow ndani ya miaka 10 kuna chance ya kufika mbali
 
Wanatumia nguvu kubwa sana ku weka picha za magari, party, kurusha pesa, n.k.
Mkuu Netmaster nakubaliana nawe kitu kimoja kwamba bado biashara za kiteknolojia kama vile kutengeneza App hazilipi kabisa. Ila ukitumia mtandao kuji-brand na kutangaza biashara yako itakuletea matokeo kirahisi sana. Kwa mfano kama ni mkulima ukaamua kweli uko serious na huna longolongo basi mitandao itakufikisha mbali.
 
Fursa za online zinalipa sana, sanaaa!! lakini kwa Tanzania bado sanaa, sanaaa!!

Kwa hii Tz ukiingia kwenye kilimo kuna mifano kabisa hai ya waliopiga hatua na madon waliochana msamba walioanza chini hata kama ni miaka 15 iliyopita ila sasa wanapiga pesa, mtu akiingia huku angalau pana possibility (sio guarantee) ya kutoboa, wapo wanaouza mayai pia kwa muda waliofanya biashara wamejenga connections wanapiga pesa, wapo wenye migahawa wana uhakika wa kuweka lita 20 kwenye range zao daily, n.k. angalau unaona biashara unayofanya kuna matop basi nawe hata ukipambana upate robo ya wanachopata basi sio haba, lakini online hio utaona tu picha zao insta ila maisha halisi ni tofauti sana
 
Wengi wapiga domo tu huko online hawapati hata hela ya vitumbua ila utawaona wanashawishi watu wafanye ila maisha yao magumu sana
Kama una ujuzi ni rahisi sana kupata pesa kupitia blogging na youtube.

Hakuna kutumia adsense wala matangazo yoyote.

Ila km hauna ujuzi itakugharimu sana. Utaona km wapiga domo
 
Me mwenyewe ni mhanga wa ishu za online, nimepiga ishu nyingi Sana , Nina account fiver, Upwork, Windsor brokers, affiliate marketing nazo nimezipiga zimekaa kitapeli tu, nilikuwa nashinda mtandaoni Kila siku nasearch online jobs.

sijui survey sijui kufungua account YouTube, finally nimekuja ku conclude kwamba kupata pesa mtandaoni ni Kazi Sana Bora hata kilimo. Ila ishu moja niliyowahi kupiga online nikafurahi ni ishu ya kuuza mabando ya airtel kabla sijafungiwa , nilikuwa napata Hadi laki mbili per day,wakanipiga ban wakafunga na account zangu.

Tangu hapo sijawahi kupata job nyingine online inayopay real money
 
Me mwenyewe ni mhanga wa ishu za online, nimepiga ishu nyingi Sana , Nina account fiver, Upwork, Windsor brokers , affiliate marketing nazo nimezipiga...
Hio ya airtel tunaweza kuiweka kundi la uwakala, na kwakweli wapo mawakala waliowahi kuotea hizi ishu wamepiga aisee! Kuna moja anajiita kaga huko twitter alichapa milioni 80 zile vocha za airtel uni akajiroga kwenda kuwaambia airtel wamrahisishie iwe kwa wanampa namba za vocha sio vocha za kukwangua.

Ishu ni huko kwenye online hizo za blogging, affiliate, up work, n.k. unakuta mtu akikaza sana yani wale wachache wanaopiga basi ndio wanaongiza milioni 1 na nusu kwa mwezi, hawa wengine hali ni mbaya, mtu yupo na pc kama kawekewa gundi ila anaingiza chini ya laki 5 kwa mwezi.

Wanaopiga piga hizi milioni 4 hadi 6 wapo wapo lakini wengi hawawezi kuwaambia hata watoto wao wanachofanya, wapo wanaoiba account za fb za watu hata wachungaji wanaanza kuzitumia ku share picha za ngono ili wapate click, wapo wanaofoji vitambulisho feki kuiba pesa za wengine, wapo wanao tapeli mitandaoni tuma ile namba, n.k.

Ubaya wa huku ni kwamba pesa zake zikikauka watu wanapauka hadi huruma. mtu ashazoea shortcut za kihuni, mrija ukibanwa ni ngumu sana ku adapt kuja kwenye shughuli halali hata kama ni za online
 
Bongo ujuaji mwingi sana. Asilimia kubwa ya vijana hawataki kujishughulisha wakishatoka vyuoni badala yake wanaanza mambo ya wizi wa mitandaoni mwisho wanakuwa Wauza ODDS, wauza accounts za youtube magemu na kadhalika yani kiufupi wanajifunza mbinu zautapeli zakila namna.

Wanunua Odds wameshapigwa sana na wale waliolizwa kimtandao wanaelewa . na ndio haohao vijana wa vyuoni waligundua "ILE HELA ITUME KWENYE HII NAMBA...."
 
Na nidhamu ya pesa huwa ni ndogo sana kundi hili sijawahi kujua kwanini
 
Online uza huduma, bidhaa au kipaji chako.

Ukiingia online kutaka mafanikio ya HARAKA ndiyo mwisho unaishia kulalamika hakuna pesa online.

Weka malengo ya kueleweka utaweza kuona matokeo.

Nenda Google search "Musabskilld" pitia tovuti na pages zote utakazoletewa.

Nimekutana na watu na kufanya kazi na tahasisi ambazo sikuwahi kufikiria kufanya nao kazi.

Ukiwa na kitu chako una nia ya dhati ya kukifanya usikatishwe tamaa kwamba online hauwezi kufanikiwa.

Vijana wengi wapo wamejulikana na kupata deals za maana kutokea mtandaoni.

Shida ni kufuata mkumbo na kuweka malengo ambayo hayaeleweki.
 
Kaka millard ni exception, katoka mbali sana huyu.

Nimekuwa nikiona baadhi ya vijana hasa hawa wa chuoni na wahitimu wenye kujua jua kutumia vilaptop wanapotoshana mambo ya youtube, blogging, sijui app, adsense, n.k. kwamba kuna pesa

Ni kweli haya mambo kwa wenzrtu huko yanalipa na watu wamebadili maisha lakini kwa bongo hii Bin No!

Kwa bongo kutoboa online ni ngumu sana, utaona tu picha zao insta ila maisha halisi ni tofauti sana, ukifatilia wale wenye nazo wanaona aibu hata kuweka wazi jinsi wanavyozipata (kushare picha za uchi kwenye account za fb wanazoziiba, kufoji vitambulisho kutapeli watu, tuma kwa ile namba, ponzi schemes, n,k).

Ni heri ufanye kilimo, tunawaona watu wamechana msamba.

Ni heri ufungue mgahawa, tunawaona watu wana range zao za milioni 200

Ni heri ufungue duka lako la hardware, mdogomdogo una grow ndani ya miaka 10 kuna chance ya kufika mbali
Kama mtu anaweza kumake milion moja hadi 3 kwa mwezi ni sawa tu maana hata kazi za kawaida hazilipi hivyo
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom