Tuache Desturi na Mila mbaya za wazee wetu! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tuache Desturi na Mila mbaya za wazee wetu!

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Topical, Jan 16, 2012.

 1. T

  Topical JF-Expert Member

  #1
  Jan 16, 2012
  Joined: Dec 3, 2010
  Messages: 5,176
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Kuna makabila mengi Tanzania bado wana mila na desturi mbaya; na kuna watu bado hawataki kuacha destruri na mila hizo. Napenda kuwafahamisha kuwa si lazima kuwafuata wazee wako walikuwa wanaamini nini? au wanafanya nini fanya utafiti mwenyewe tafuta ukweli kabla ya kifo; maana kila mtu atabeba mzigo wake ahera..

  1. Chunguza kama dini za wazee wako ni sahihi i.e. usikubali kuabudu mizimu, sanamu wala usimshirikishe Mwenyezi na kitu chochote. Si lazima kufuata dini za wazee kama wanaabudu mizimu, sanamu maana utaulizwa mwenyewe tu wala kufuata baba yako haitakuwa sababu ya kutosha siku hiyo..

  2. Usikubali kuonea wanawake na watoto; kuna makabila watoto wa kike hadi leo wanaonewa, na wanawake hawapewi stahili zao; hakuna mgawanyo wa mali; nimekutana na kesi moja huku Dodoma wanaume tu ndio wanaridhi maliya baba kama ng'ombe na ardhi lakini wasichana hawapati chochote.

  3. Mnaweza kuongeza mila na desturi mbovu......mnazojua???
   
 2. Gaijin

  Gaijin JF-Expert Member

  #2
  Jan 16, 2012
  Joined: Aug 21, 2007
  Messages: 11,850
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 0
  Siku ipi?
  Yaani unatuambiwa tujiulize kuhusu mila za mababu zetu lakini hapo hapo ushatupa jibu kuwa tufate unachotaka wewe!

  *ni mirathi sio miradhi
  (kwa Waswahili miradhi hutumika kumaanisha maradhi ya kila aina wakati)
   
 3. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #3
  Jan 16, 2012
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  2. Kuhakikisha hiyo haitokei inabidi na dini fulani nayo iangaliwe maana inakandamiza sana wanawake na sehemu ya watoto.
   
 4. Gaijin

  Gaijin JF-Expert Member

  #4
  Jan 16, 2012
  Joined: Aug 21, 2007
  Messages: 11,850
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 0
  Unaweza kutusaidia kutujuza hizo baadhi ya dini na namna zinavyokandamiza sana wanawake na watoto?
   
 5. Erickb52

  Erickb52 JF-Expert Member

  #5
  Jan 16, 2012
  Joined: Oct 31, 2010
  Messages: 18,566
  Likes Received: 112
  Trophy Points: 160
  Nafasi ya mwanamke iko palepale tu,kamwe hawezi kuwa sawa na mwanaume hata ufanyaje,wazee walikuwa sahihi ila kwa kuwa siku hizi mnaleta uma-gharibi ndo maana mambo yanaonekana tofauti,wazee walikuwa makini sana na busara nyingi kuliko watu wa sasa.Unyanyapaa wa wanawake ulianza tangu zamaniiiiiiiii na hata utake kuuondoa huwezi coz ndo imeumbwa iwe hivyo.
  Halafu mwanamke ukimpa nafasi ana manyanyaso sana,hivi si ushasikia kuwa hata wao wanashauri USIOE MWANAMKE ALIYEKUZIDI KIPATO AU ELIMU??? Hujiulizi kwanini??? then pata picha wanawake wote wawe na elimu na pesa dunia itakuwaje?
  Wacha ile kwao hivihivi.
   
 6. Gaijin

  Gaijin JF-Expert Member

  #6
  Jan 16, 2012
  Joined: Aug 21, 2007
  Messages: 11,850
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 0
  Imeumbwa iwe hivyo na nani?
   
Loading...