TTCL to TCC: Kauli ya Mopao "Tanzania iwe Ethiopia" yaelekea kutimia

Jan 24, 2018
15
12
Moja ya njia ya kuwatambua viongozi na muelekeo wao ni kupitia kauli zao. Si mara ya kwanza kumsikia 'mopao' akizungumzia makosa ya ubinafsishaji holela hasa sekta ya mawasiliano. Akitolea mfano wa Ethiopia kuwa na kampuni moja ya umma tu ya mawasiliano. Kisha akazilazimisha kampuni za mawasiliano kujisajili DSE.(akiwindwa zaidi 'DAVO').

Baadae ikawalazimu kusajili taarifa zao kwa mfumo mpya wa kielekroniki (huku ttcl ndio 'mbunifu' wa mfumo huu). Punde Airtel ni mali ya TTCL. Leo kampuni mpya 'yenye meno zaidi' imezaliwa.

Kama ambavyo 'Mopao' alivyotamani nakufanikiwa kuminya 'mainstream medias',-kwa sababu zile zile-ndivyo anavyotaka kuminya sekta ya mawasiliano.

'Nothing is coincident', makampuni binafsi yamawasiliano yajiandae kumpisha TCC kwani 'Mopao' is at work kuifanya 'Tanzania kuwa kama Ethiopia.'

Ni utabiri tu kama wa Sheikh Yahya!
 
Sasa kuna ubaya gani hilo likitokea. Wewe unafurahia huu ujambazi unaofanywa na haya makampuni ya simu? Tunahangaika na kodi kutoka kwa wamachinga huku makampuni kama Airtel hayalipi kodi.

Mimi naona yafe tu hayo makampuni yenu ya mabeberu. Hayana faida yoyote zaidi ya kuwanyonya watanzania. Yafe tu. Yafe tu. Hakuna namna. Tumechoka.
 
Sasa kuna ubaya gani hilo likitokea. Wewe unafurahia huu ujambazi unaofanywa na haya makampuni ya simu? Tunahangaika na kodi kutoka kwa wamachinga huku makampuni kama Airtel hayalipi kodi. Mimi naona yafe tu hayo makampuni yenu ya mabeberu. Hayana faida yoyote zaidi ya kuwanyonya watanzania. Yafe tu. Yafe tu. Hakuna namna. Tumechoka.
Kiukweli Karibu shirika jipya la mawasiliano?
 
Sasa kuna ubaya gani hilo likitokea. Wewe unafurahia huu ujambazi unaofanywa na haya makampuni ya simu? Tunahangaika na kodi kutoka kwa wamachinga huku makampuni kama Airtel hayalipi kodi. Mimi naona yafe tu hayo makampuni yenu ya mabeberu. Hayana faida yoyote zaidi ya kuwanyonya watanzania. Yafe tu. Yafe tu. Hakuna namna. Tumechoka.

Swali la msingi, tunaouwezo wa kudeliver? Chukua case study ya hii ttcl ya sasa. Mwaka juzi/jana walianza kuifufua upya lakini nashindwa kuelewa kama wako serious kiasi gani.
1 . coverage yao mbovu. Uko mwanza mjini lakini ukitoka km 10 nje(nyegezi) hakuna service.

2 inafanya kazi kwenye sim za 3+ G tu. Ikiwa baadhi ya sim za line 2 haifanyi kazi.

Bahati nzuri nimekua mteja wa ttcl since 2010, kwa ujumla wana vimasharti ambavyo ni vikwazo katika ushindani wa kibiashara(2010 nilinunua modem ya ttcl-ili kupata bundle ilikua unaandika barua ya maombi kwa meneja-case haikovhivyo leo lakini biashara siku zote inajengwa na vile umeianza day one) . though sisemi kuwa makampuni binafsi hayana matatizo yao
 
Sasa kuna ubaya gani hilo likitokea. Wewe unafurahia huu ujambazi unaofanywa na haya makampuni ya simu? Tunahangaika na kodi kutoka kwa wamachinga huku makampuni kama Airtel hayalipi kodi.

Mimi naona yafe tu hayo makampuni yenu ya mabeberu. Hayana faida yoyote zaidi ya kuwanyonya watanzania. Yafe tu. Yafe tu. Hakuna namna. Tumechoka.
Kama kampuni hailipi kodi unailaumu vipi kampuni ikiwa sheria zipo na wasimamia ulipaji wapo?

Naona hoja yako haijajua imlenge nani.

Ikiwa unafurahia sekta binafsi kufa jua kua sekta binafsi ina mchango mkubwa kwenye maendeleo.

Na ushindani wao ndiyo unasababisha wewe leo kuweza kujiunga hata kifurushi cha mia tano zamani ilikua unaweka mia tano halafu unapiga simu kidole kipo kwenye button ya kukatia.

Tanesco wako wenyewe na delivery yao ni mbovu unadhani kutakua na tofauti huku ttcl?
 
1. Hoja yangu inalenga hayo hayo makampuni ya simu yanacheza na vitabu vya uhasibu. Kila kukicha, yanasema yamepata hasara. Sheria inasema unatoza kodi pale unapopata faida. Sasa kama umechezea vitabu vya uhasibu na ukaonesha kuwa umepata hasara, hiyo kodi unaipata wapi hapo?

2. Sifurahi sekta binafsi kufa. Natambua mchango mkubwa wa sekta binafsi katika uchumi popote duniani. Ninafurahi kuona wafanyabiashara wanaoliibia taifa kwa kupitia mwamvuli wa sekta binafsi wanafariki kifo cha mende. Sekta binafsi inayofanya kazi kwa uadilifu ndiyo tunayohitaji tanzania ya leo.

3. Tanesco ni habari nyingine.
 
Swali la msingi, tunaouwezo wa kudeliver? Chukua case study ya hii ttcl ya sasa. Mwaka juzi/jana walianza kuifufua upya lakini nashindwa kuelewa kama wako serious kiasi gani.
1 . coverage yao mbovu. Uko mwanza mjini lakini ukitoka km 10 nje(nyegezi) hakuna service.

2 inafanya kazi kwenye sim za 3+ G tu. Ikiwa baadhi ya sim za line 2 haifanyi kazi.

Bahati nzuri nimekua mteja wa ttcl since 2010, kwa ujumla wana vimasharti ambavyo ni vikwazo katika ushindani wa kibiashara(2010 nilinunua modem ya ttcl-ili kupata bundle ilikua unaandika barua ya maombi kwa meneja-case haikovhivyo leo lakini biashara siku zote inajengwa na vile umeianza day one) . though sisemi kuwa makampuni binafsi hayana matatizo yao

Tupishe, hama nchi!
 
Ufanisi na ubunifu ni mojawapo ya changamoto zinazoyakabili mashirika yetu ya umma...
 
1. Hoja yangu inalenga hayo hayo makampuni ya simu yanacheza na vitabu vya uhasibu. Kila kukicha, yanasema yamepata hasara. Sheria inasema unatoza kodi pale unapopata faida. Sasa kama umechezea vitabu vya uhasibu na ukaonesha kuwa umepata hasara, hiyo kodi unaipata wapi hapo?

2. Sifurahi sekta binafsi kufa. Natambua mchango mkubwa wa sekta binafsi katika uchumi popote duniani. Ninafurahi kuona wafanyabiashara wanaoliibia taifa kwa kupitia mwamvuli wa sekta binafsi wanafariki kifo cha mende. Sekta binafsi inayofanya kazi kwa uadilifu ndiyo tunayohitaji tanzania ya leo.

3. Tanesco ni habari nyingine.

Mkuu makampuni binafsi kuchezea vitabu vya uhasibu suluhu yake ndio 'kuyaua'?
 
Hiyo ni sehemu ya adhabu. Ni fundisho kwa makampuni yanayobaki hai. Kwamba, nikirudia makosa ya kampuni X, adhabu yangu ni kifo. Hakuna binadam asiyeogopa kifo. Labda wewe mwenzetu.
 
Sasa kuna ubaya gani hilo likitokea. Wewe unafurahia huu ujambazi unaofanywa na haya makampuni ya simu? Tunahangaika na kodi kutoka kwa wamachinga huku makampuni kama Airtel hayalipi kodi.

Mimi naona yafe tu hayo makampuni yenu ya mabeberu. Hayana faida yoyote zaidi ya kuwanyonya watanzania. Yafe tu. Yafe tu. Hakuna namna. Tumechoka.

Wala sio hivyo mkuu.

Tatizo la wizi ni UDHIBITI.

Sio kubadili mmiliki wa kampuni,mwizi ni mwizi tu.Ukiigeuza kampuni au mfumo wa kibiashara ukawa wa kiserikali,hapo unakaribisha mediocre business performance,na hakuna guarantee eti hawataiba.

Cha msingi angesimamia sector ipasavyo,kusiwe na wizi wa aina yoyote wala ujanja wa aina yoyote.Hapo tu.

UDHIBITI ndio kazi ya serikali!Sio kubadili na kupora makampuni ya watu.
 
Hiyo ni sehemu ya adhabu. Ni fundisho kwa makampuni yanayobaki hai. Kwamba, nikirudia makosa ya kampuni X, adhabu yangu ni kifo. Hakuna binadam asiyeogopa kifo. Labda wewe mwenzetu.

Mkuu mwizi haibi hadi aone sehemu ya kuiba na mazingira umemtengenezea ya kuiba. Sekta binfsi ni wafanyabiashara(analenga kupunguza cost na kuongeza faida), sasa kama tuna mifumo dhaifu ya kisheria na kiutendaji, unategemea kweli tusiibiwe?
 
Sawa nakubali hoja yako. Ina mantiki. Ndiyo maana hapo juu nikasema, kuua hayo makampuni ni SEHEMU ya adhabu. Otherrise, nakubiliana nawe kwa asilimia 250
 
Wala sio hivyo mkuu.

Tatizo la wizi ni UDHIBITI.

Sio kubadili mmiliki wa kampuni,mwizi ni mwizi tu.Ukiigeuza kampuni au mfumo wa kibiashara ukawa wa kiserikali,hapo unakaribisha mediocre business performance,na hakuna guarantee eti hawataiba.

Cha msingi angesimamia sector ipasavyo,kusiwe na wizi wa aina yoyote wala ujanja wa aina yoyote.Hapo tu.

UDHIBITI ndio kazi ya serikali!Sio kubadili na kupora makampuni ya watu.

Sawa nakubali hoja yako. Kuna udhaifu mkubwa katika usimamizi wa makampuni hayo. Uadilifu umekosekana kwa baadhi ya watumishi serikalini. Wanashirikiana na haya makampuni kulitia taifa hasara.
 
Back
Top Bottom