TTCL kuzindua huduma ya 4G leo

TTCL kuzindua huduma ya 4G leo

Hivi TTCL lina uongozi? Kama lina uongozi, wana mission na vision? Ni ajabu kuna watz hasa wa kizazi cha sasa hawafahamu kama tuna shirika la mawasiliano la taifa
 
Hivi TTCL lina uongozi? Kama lina uongozi, wana mission na vision? Ni ajabu kuna watz hasa wa kizazi cha sasa hawafahamu kama tuna shirika la mawasiliano la taifa

TTCL inafahamika zaidi na corporate customers.....mtu wa kawaida ni ngumu kuifaham maana haikua serious kwenye mobile business...sasa ndio muda wa kuitambua kampuni yenu
 
Tujiulize kama hizi bei za vifurushi vyao zimekaa kiushindani kweli na makampuni mengine binafsi. Mimi naona bei ziko juu sana.
 
Tatzo hawajitangazi kabisa nimeingia website yao sijaona hiyo habari ya 4G...kwa nini ttcl hawauzi line za simu kama haya makampuni mengine?

Haya Mimi nimekutana na kadhia hiyo, kwenye web site yao hawajatangaza!
 
Hii laana tulioirithi ya kutokuwa na uzalendo inatufanya tushindwe kuthamini mashirika yetu mfano TTCL wana bei nafuu kuliko makampuni yote ya simu lakini sisi hatuoni ilo tunabakia kuumizwa na wezi w mchana kina voda tigo na airtel. MUNGU atukomboe toka laana hiyo.

TTCL siwajui, kama hawafanyi kama wanavyofanya washindani wenzao unadhani wateja watawapata wapi.
 
Haya Mimi nimekutana na kadhia hiyo, kwenye web site yao hawajatangaza!

nadhani wataupdate baadae kdogo...la muhimu ni kwamba wanazindua na wateja mkae mkao wa kula maana sasa mtajua ni namna gani Smile,Tigo na Smart walikua wanawaibia mchana peupee...na speed fake za 4G
 
Habari niliyoipata hivi punde!!!.
Afisa Mtendaji mkuu wa TTCL Kamugisha Kazaura kazindua huduma ya 4G LTE makao makuu ya TTCL.Tunaomba watu wa TTCL watwambie line zinapatikana wapi na ni bei gani maana naona Tarrif ya data tena kwa wiki,vipi kwa siku!!.Vipi kuhusu voice tarrif!!!
 
Sisi tutakuwa wazalendo kama hao ttcl wataonesha juhudi. Tatizo viongozi wengi wana conflict of interest ,wana ubia na tigo, voda, airtel.

Ni bora ninunue Gb ttcl kwa 2000 maana najua pesa itabaki hapa, kuliko ninunue 1gb tigo pesa iende kwa tajiri mzungu ulaya
 
conflict of interest ndio sababu kwa sababu viongozi wana share Vodacom, Tigo, Airtel , tena mkakati wao ulikuwa ni kuiua kabisa ila wafanyakazi ndo waliiokoa

Ndiyo hiyo ninayoisemea kuwa Viongozi wana interest kwenye hayo makampuni na TTCL kama Tanesco wafanyakazi walikomaa ndo maana wana survive vinginevyo tungeshawasahau siku nyiingi!
 
Sisi tutakuwa wazalendo kama hao ttcl wataonesha juhudi. Tatizo viongozi wengi wana conflict of interest ,wana ubia na tigo, voda, airtel.

Ni bora ninunue Gb ttcl kwa 2000 maana najua pesa itabaki hapa, kuliko ninunue 1gb tigo pesa iende kwa tajiri mzungu ulaya
Angalia vizuri bei za vifurushi vyao. Hakuna kifurushi cha 2,000/=.
 
Hakuna laana yoyote ila wenye laana ni Ttcl wenyewe. Walitutesa sana hawa jamaa,ilifika wakati uhonge milioni upate laini ya simu. Hawana tofauti na Tanesco. Unadai shirika halina pesa,mtu akitaka huduma yako ili upate pesa unataka rushwa. Huu ni wazimu. Ttcl wao walitakiwa kuwa wa kwanza kwa simu za viganjani lakini kutokana na rushwa hawakujali hilo,ilivyoanza Mobitel (sijui hata kama wengine wanaijua) walitumia gateway ya Ttcl kwa huduma zao. Cha kujiuliza hapo kwa nini kama walikuwa na facilities hizo hawakuanzisha simu za viganjani wakati ule? Rushwaaaaa
Ni kama unaisoma akili yangu. Kama kuna shirika lililo wanyanyasa watanzania wazalendo na kuthamini wahindi ni hili TTCL. Walishawahi kubambika wateja bili zisizowahusu. kifupi hawa na Tanesco hakuna tofauti. Linaongozwa na waswahili na mambo yake ni hovyo. Wabaki na mkongo wa taifa, mambo mengine hawataweza.
 
Tujiulize kama hizi bei za vifurushi vyao zimekaa kiushindani kweli na makampuni mengine binafsi. Mimi naona bei ziko juu sana.

Ni kweli mkuu, hapo wamekosea sana!! Hii inanikumbusa majibu ya Mvietnam, niliwahi kumuhoji hivi inakuwaje bei zenu za vifurushi havina tofauti kubwa na providers wengine - unajua alinijibu nini? Hapana, hapana sisi hatuwezi kwenda kinyume na VodaCOM - nilishangaa sana, nikawa najiuliza maswali mengi hivi hawa Vodacom ndio wamechukuwa majukumu ya TCRA au Wizara ya Mawasiliano au wanawatishia wengine wasiwe na bei tofauti na wao au kuna Cartel ya aina fulani hivi!!

Sasa kama Shirika la UMMA linataka kuhiga wenzao basi hapo tumeliwa.
 
Sisi tutakuwa wazalendo kama hao ttcl wataonesha juhudi. Tatizo viongozi wengi wana conflict of interest ,wana ubia na tigo, voda, airtel.

Ni bora ninunue Gb ttcl kwa 2000 maana najua pesa itabaki hapa, kuliko ninunue 1gb tigo pesa iende kwa tajiri mzungu ulaya
nakubaliana nawe mkuu, lakini Viongozi wenye shares kwenye Makampuni hayo si wanajulikana, nafikiri Dk.Magufuli na Waziri wake Mkuu wanapaswa kuwambia Viongozi wenzao wachague moja: kuendelea na ajira Serikalini au kuhachia ngazi na kwenda kufanya biashara kwenye makampuni hayo.
 
Mbarawa karudi tena sjui atabadilisha nn safari hii
 
Ni kweli mkuu, hapo wamekosea sana!! Hii inanikumbusa majibu ya Mvietnam, niliwahi kumuhoji hivi inakuwaje bei zenu za vifurushi havina tofauti kubwa na providers wengine - unajua alinijibu nini? Hapana, hapana sisi hatuwezi kwenda kinyume na VodaCOM - nilishangaa sana, nikawa najiuliza maswali mengi hivi hawa Vodacom ndio wamechukuwa majukumu ya TCRA au Wizara ya Mawasiliano au wanawatishia wengine wasiwe na bei tofauti na wao au kuna Cartel ya aina fulani hivi!!

Sasa kama Shirika la UMMA linataka kuhiga wenzao basi hapo tumeliwa.

Juzi kwa kipindi cha baragumu mkuu wa masoko aligusia kwa mbali kuwa TCRA ndio kikwazo wanadhibiti bei za 4g. tz hakuna soko huria!
 
Juzi kwa kipindi cha baragumu mkuu wa masoko aligusia kwa mbali kuwa TCRA ndio kikwazo wanadhibiti bei za 4g. tz hakuna soko huria!

Mkuu TCRA nayo inapaswa kushughulikiwa na Dk.Magufulini fasta, makampuni ya simu yamekwisha wateka nyara - we fikiria utawasikia wakisema hawewezi kufanya mahamuzi yoyote bila ya kuwashirikisha stake holders kwanza hapo wanamaanisha makampuni ya simu sio watumiaji? Wewe utakwendaje kuomba ushauri kwa watu unaoa wasimamia na kuwalipisha kodi - hii inaingia akilini kweli?

Makampuni haya yanapata faida kubwa sana lakini ulipaji kodi wao hauendani na faida wanayo vuna - TCRA wala TRA hawako overly concern na loopholes zinazo tumiwa na makampuni haya kufanya ujanja wa kutuacha solemba na kodi kiduchu.

Mtu ungetegemea TCRA na TRA watembelee Kenya na Rwanda ili wajifunze mbinu zinazo tumiwa na Mataifa hayo kuyabana Makampuni ya simu ili zilipe kodi stahiki - hilo hawalichangamkii hata kidogo, akili zao zipo kuhangahika kudhibiti simu fake - sijui fake wana maana gani kama simu unaweza kuweka sim card ikazungumza kupitia mtandao wowote huo u-fake unatoka wapi kwani si zote zinatumia hardware zinazotumika kwenye branded handsets - kupoteza muda tu kwenye vitu vidogo dogo na kuvipatia publicity stunts zisizo na tija!

Nasema hivi TCRA na TRA wafanyie kazi mapendekezo ya Mzalendo Hazan Zungu aliyo toa Bungeni kuhusu chombo cha kusaidia kukokotoa kodi halisi ya makampuni ya simu - aliwahi kutaja na kampuni inayohusika na uhundwaji wa system hiyo kama sikosei, alisema Kenya na Rwanda wamefaidika sana kutokana na kutumia system hiyo, kwa bahati mbaya sikuona kama Wizara specifically TCRA au TRA wakichangamkia wazo hilo lenye mshiko kwa Taifa letu, sio kwamba hawajui umuhimu wa kukusanya kodi stahiki - hawataki tu 4 some reason - sasa kwa nini Dk.Magufuli hasiwachukulie hatua kali watu ambao wataka kukwamisha juhudi za Taifa letu kukusanya kodi, makampuni ya simu yasijifanye ni Govt within a Govt.

Ufagio ulio ikumba TRA unapaswa kupitishwa vile vile TCRA jamaa hao wamejisahau sana - kutochangamkia mapendekezo za Mbunge wa Ilala Mh.Zungu uliniacha najiuliza maswali mengi kuhusu umuhimu/utendaji kazi wa TCRA, sijui priorities zao kuu ni zipi kama sio kuzibana/kufatilia kwa karibu kampuni za Simu na Utangazaji TCRA wasifanye urafiki nazo - urafiki uwe confined kwenye business and not otherwise.
 
Juzi kwa kipindi cha baragumu mkuu wa masoko aligusia kwa mbali kuwa TCRA ndio kikwazo wanadhibiti bei za 4g. tz hakuna soko huria!

Nakwambia kuna Cartel ya aina fulani si bure, Serikali ikifatilia kwa karibu wanaweza kubaini wahusika wakuu wa umafia huu ni akina nani - TCRA inatumiwa tu ndio maana nasema nayo inapaswa kufumuliwa na JPM. Kwani Serikali inaposema siku hizi biashara huria inaruhusiwa TANZANIA wana maana gani au biashara huria zinahusu nguo/vitenge na mazao - tunataka watufafanulie.
 
Back
Top Bottom