TTCL ina deni la bilioni 403 ilhali mtaji bilioni 243

If a company's liabilities exceed its assets, this is a sign of asset deficiency and an indicator the company may default on its obligations and be headed for bankruptcy. ...

Red flags that a company's financial health might be in jeopardy include negative cash flows, declining sales,

and a high debt load.

So based on what is happening at Ttcl, it's definite that the company is already in the limbo ready only for the interment. Next on the list will be Atcl, another of the remaining white elephant 🐘 projects draining the country's coffers.
 
Sijui kama umeelewa hoja ya mleta thread au uccm umekula ubongo wako. Hoja ni kwamba ttcl wakati WA ngosha walikuwa wanatoa gawio lakini Leo wanadai Wana deni lisilolipika. HATA atcl hivyohivyo lakini kumbe zilikuwa mbwembwe.
Hakuna shirika lolote la serikali lililowahi kufanya vzuri Zaidi ya kubebesha mzgo watanzania.

Maccm must go to hell.
Wewe huelewi mambo ya siasa.Kwani nani anakwambia kuna hata shirika moja la serikali linamake profit.zile zilikuwa ni mbwembwe za kisiasa ambazo zilikuwa obvious.hapa nazungumzia hiyo point ya negative net assets iliyoletwa na mtoa maada akimnukuu Hasunga
 
Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) imesema Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) limelemewa na deni la Sh403 bilioni ilhali mtaji ilionao ni wa Sh243.

Makamu Mwenyekiti wa kamati hiyo, Japhet Hasunga amesema hayo jana Jumatano Oktoba 20, 2021 baada ya kuipitia ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) ya mwaka 2019/20 ambapo amesema wamebaini kuna viashiria katika Shirika hilo kutofanya vizuri kwakuwa lina mtaji hasi wa Sh132 bilioni na madeni makubwa kuliko mtaji wake.

“Hicho ni kiashiria kuwa bado shirika haliendi vizuri. Shirika letu linalipa hadi kodi lakini mapato yao hayajaingizwa katika vitabu vyao,” amesema Hasunga.

=====

Pamoja na nia njema ya JPM, mashirika ya umma yamekuwa yanakula pato la Taifa bila kuleta tija. Tubaki na Tanesco yenye maslahi mapana ya Taifa, haya mengine tukihitaji uzalendo tuwape wafanyabiashara wazawa wajaribu bahati yao.

TTCL ndio ina mkongo wa Taifa wa Data, pamoja na advantage hiyo kibiashara wameshindwa kabisa kutawala soko la internet, yaani mwingine ananunua kutoka kwao halafu anawagaragaza sokoni, tumeshindwa.
Ni jpm pekee anajua deni hilo limetoka wapi na fedha zilikwenda wapi.
 
Kwann wasibinafsishe au waingie ubia na kampuni zinazoeleweka.

Hili shirika si waliuziwa wahindi wakijulikana kama CELTEL na ISSA ambae ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa bodi ya TANESCO akiwa ndio dalali wa kuliuza shirika? Magufuli alipoingia akawalipa hela zao na kulirudisha shirika serikalini na kutangaza kuwa shirika lilikuwa linatengeneza faida na kutoa gawio kwa serikali!!!

Imekuwaje sasa shirika lililosifiwa na Magufuli hata miaka miwili haijapita linakuwa na madeni kuliko mtaji wake?
 
Bwana yule ameiingiza hii nchi hasara kubwa

Hivi wale waliopokonywa koroshow zao tayari washalipwa ama bado uhakiki wa mashamba unaendelea kule kaburini Chato
Magufuli aliikuta TTCL imeshajifia miaka mingi tu iliyopita. Amehangaika nayo mpaka hapo ilipofika. Awamu wa sita nao wafanye kitu kwa TTCL tuone.
Tusibeze juhudi za JPM kuifufua TTCL. Alijitahidi kwa wakati wake
 
TTCL ndio mtandao pekee ambao hauna huduma ya 4G ndani ya baadhi ya makao makuu ya mikoa

Hizi hasara zinatoka wapi kama huduma shindani hawana!

Au ndio wale wakurungezi wanajigawia tu mishahara!
 
TTCL,ATCL,TANESCO etc yaani yote yanaaingiza hasara serikali...Tunajifunza ni nin hapo? Serikali haiwezi kufanya biashara!! Wakusanye Kodi tu!
 
Hivi ubahabari Tanesco haijawahi kupata faida tangu limeanzishwa??? Tanesco linafanya kazi nje ya nchi eti??? Tulikuwa tunaishi zama za ulimbukeni sana

Huezi kuripoti loss report kwenye shirika linalomilikiwa 100% na serikali, huo ni upumbavu na ujinga wa hali ya juu na kutokujua aspect za uchumi, ni sawa sawa na zile hospitali znazotoa huduma bure vijijini kuziandikia balance sheet kwamba znapata hasara! Deni linalomatter ni la nje, hakunaga deni la ndan ya nchi linatumika kama siasa na sio ukweli wenyewe
 
If a company's liabilities exceed its assets, this is a sign of asset deficiency and an indicator the company may default on its obligations and be headed for bankruptcy. ...

Red flags that a company's financial health might be in jeopardy include negative cash flows, declining sales,

and a high debt load.

So based on what is happening at Ttcl, it's definite that the company is already in the limbo ready only for the interment. Next on the list will be Atcl, another of the remaining white elephant 🐘 projects draining the country's coffers.

ni TTCL ndo anaekufanya mpaka unaandika comment apa, akiamua kuanza kujiendesha kwa faida hutakaa uguse mtandao
 
TTCL,ATCL,TANESCO etc yaani yote yanaaingiza hasara serikali...Tunajifunza ni nin hapo? Serikali haiwezi kufanya biashara!! Wakusanye Kodi tu!

bana weee, serikali haiwezi kutengeneza loss katika uchumi unaoumiliki, TTCL inaweza kuendelea kuwepo miaka yote unlike ATCL ambayo itatoka nje ya nchi hence kuhitaji foreign currency
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom