Trust katika Mahusiano

hehehehehehe! Mwali upo?? Ni salamu tu wangu! Salamu kwa mume wetu na wanangu!
nyie nanyi karibu nitawatimua na huyo mume wenu, ndo maana kuutwaa mnadanganywa mwili na roho, lol!
 
Niliposoma kichwa cha mada nilidhan ni ya zamani kumbe ni yajana tu
'
Dah!Jambo gumu hili,trust!!!!
ha haaa, rafiki ni jambo gumu, lakini tunapaswa kulizingatia sana
 
ha haaa, rafiki ni jambo gumu, lakini tunapaswa kulizingatia sana

Nikuambie kitu,nina zaidi ya miaka 30,lakini kwenye suala la mahusiano sijawahi kukutana na mkweli na zaidi hakuna kitu kinachoitwa trust,hakipo kabisa!
 
ha haaa, kila la heri best, pata ambaye mtakuwa mnajieleza wote, lol!
ukiangalia sana hapa ndo unaweza kumhisisha mwenzi wako kuwa una mambo/ajenda za siri.... kwa nini unadanganya movements? kama unaenda sokoni, sema naenda sokoni na uende sokoni........
kuna ile aga ya "natoka kidogo" bila ya kusema unaenda wapi, hiyo naona ingefaa kama hutaki mtu ajue unakoenda, ingawa kuna ving'ang'anizi utasikia "unaenda wapi"
mimi kuna muda nakuwa sijui mume wangu kaenda wapi, either anaweza kuniambia location lakini nasahau muda huohuo au anaweza kusema natoka kidogo jibu langu always linakuwa "uende salama". kizaazaa kinakuja mtu au mtoto ananiuliza baba ameenda wapi halafu natoa jibu sijui, mtu akirudia "hujui?" ndo kila kitu kinarudi sasa.... kumbe nilipaswa ku-cram....., lol!
 
Nikuambie kitu,nina zaidi ya miaka 30,lakini kwenye suala la mahusiano sijawahi kukutana na mkweli na zaidi hakuna kitu kinachoitwa trust,hakipo kabisa!
ha haaa, una mahusiano ya kudumu?
 
Last edited by a moderator:
mimi naona upo sahihi kabisa hapa......
hapo kwa RED ni muhimu sana, kujenga mazingira ya kuaminiwa........
utakuta mtu unampigia simu anakuambua nipo kwa mama wakati kwa nyuma unasikia muziki mkubwa....au kelele nyingi kama yupo disco au bar, hapo unamweka mpenzi wako kwenye mstari gani? aamini upo kwa mama wakati anasikia hizo fujo zote? mtu anawaza kwa nini ananidanganya? anaona mimi siwezi kufikiria?
 

Kwa hiyo hata nikiulizwa umetoka wapi? Nitowe kavu kavu NATOKA KUNYA, eti sababu nimetokea chooni,
nikisema nimetoka kujisaidia itakuwa "too general"
 
ila ujue kuwa huyo unayemdanganya kwa kuepusha drama, akijua umendanganya yatakuwa ni majaaaaaaaaaaaaaaaaaanga sasa.
 
ha haaa, ndo maana nikawaita warembo wangu mujionee mwenyewe denti, msije ingia kwa choo cha kiume, lol!

ila kuna uongo hua unafaida
unaweza sema uongo kuepusha kitu flani
so kuna faida na hasara pia za uongo!!
 
Kwa hiyo hata nikiulizwa umetoka wapi? Nitowe kavu kavu NATOKA KUNYA, eti sababu nimetokea chooni,
nikisema nimetoka kujisaidia itakuwa "too general"
mada inaongelea sema unaenda chooni, siyo umetoka wala siyo kufanya nini.....umenipata?
 

ila kuna uongo hua unafaida
unaweza sema uongo kuepusha kitu flani
so kuna faida na hasara pia za uongo!!
Msome royna hapo juu ya post yako......
huo uongo unaoona una faida je siku mtu akigundua ulidanganya atajisikiaje?
 
Last edited by a moderator:

haina madhara ndio, lkn kwanini udanganye? Kwa case yako hiyo ya kuongeza miaka lengo lake ni nini?? Na wewe unajaribu kuprove kuwa mkubwa kuliko hali halisi????? Sikuachi leo mpaka unipe majibu yatakayoniridhisha. LOL
 
leo naomba niseme hii, tangu nimeingia JF miongoni mwa wadada ninao wapenda ww ni mmoja wao. Unajua kwann? Bse una mambo kadhaa ambayo ninayapenda. Maisha yako huigizi (nionavyo mm)
Huu uzi umenigusa sn ila ctachangia bse nimelate na najua wadau wengi watakuwa wamesema mengi.
Ila unajua nn FP, uaminifu ni kitu kizur sn na unakuwa huru na maisha yako. Yaan huna hofu na uyatendayo.
Naunga mkono mada ni nzur.
 
Hivi trust ni ipi?
Ni kuiacha simu ya mpenzio iite aje apokee mwenywe hata wa manane?
Au kung'ang'ana kuipekenyuwa akiiacha mezani, labda kenda kuoga tu ivi?

Akumulikae mchana usiku atakuchoma!
 
hata sijui niseme nini hapa...... hii ni surprise.
nimefurahi kutambua unafurahia michango yangu hapa JF, asante sana.
Ukweli huwa nasemaga kama kuna mtu ananifahamu kiuhalisia akisoma post zangu lazima atajua ni mimi. sijawahi kufaulu somo la kuigiza, lol! na najiona nina amani sana kuwa real kuliko kuigiza...
Ukweli watu wengi tunapenda sana kuaminiwa na wenzetu na pia kuwa na mazingira ambayo unajua mwenzio ni mwaminifu, ingawa ni ngumu mno
 
Hakuna kitu kibaya katika mahusiano kama kusema uongo au kugundua umedanganywa...inapunguza trust kati ya wawili
Ni vyema mtu akawa muwazi kwani inaleta uhuru na itamfanya mtu kufanya mambo kkwa uwazi
If you are committed to someone kwanini unafichaficha vitu? Binafsi nalaani mauongo uongo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…