Trump na Putin kukutana wiki ijayo

Trump na Putin kukutana wiki ijayo

Jize one

Member
Joined
Jul 8, 2025
Posts
16
Reaction score
20
Naibu balozi wa urusi katika umoja wa mataifa Dmitry Polyanskiy amesema Rais wa Urusi Vladimir Putin huenda akakutana na Rais wa Marekani Donald Trump
Hatua hiyo inaleta matumaini makubwa katika kumaliza mgogoro unaendelea kati ya Urusi na Ukraine, licha ya kutokuwepo kwa taarifa rasmi za ushiriki wa Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskiy
Unatamani kusikia muafaka gani ukifikiwa na Marais Hawa wawili watakapokutana?

Source:Officialzungu_
Screenshot_20250808-084540.png
 
Natamani EU wasiwahisishe
Hata mimi mkuu, lakini kwa bahati mbaya kumbuka Uingereza,Ufaransa na Ujerumani ndio washauri wakuu wa Zelensky na hawataki mgogoro huu huishe/sitishishwe watamshauri Zelensky akatae ushauri wa Trump, wao watamsadia kuishinda kivita Urusi, ndio walivyo, nafikiri hata Trump amekwisha washtukia.
 
Naibu balozi wa urusi katika umoja wa mataifa Dmitry Polyanskiy amesema Rais wa Urusi Vladimir Putin huenda akakutana na Rais wa Marekani Donald Trump
Hatua hiyo inaleta matumaini makubwa katika kumaliza mgogoro unaendelea kati ya Urusi na Ukraine, licha ya kutokuwepo kwa taarifa rasmi za ushiriki wa Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskiy
Unatamani kusikia muafaka gani ukifikiwa na Marais Hawa wawili watakapokutana?

Source:Officialzungu_View attachment 3435517
Viongozi wa nchi zinazopigana watakutana lini ?
 
Viongozi wa nchi zinazopigana watakutana lini ?
Bado haijajulikana ni lini hasa watakutana lakin kupitia kikao hiki kati ya trump na Putin bila shaka kitaleta muafaka wa Kujua ni lin watakutana kwa mataifa yanayopigana (Ukraine &urusi)
 
Bado haijajulikana ni lini hasa watakutana lakin kupitia kikao hiki kati ya trump na Putin bila shaka kitaleta muafaka wa Kujua ni lin watakutana kwa mataifa yanayopigana (Ukraine &urusi)
Yaani Putin na Trump waamue lini Putin na Zelensky wakutane?
 
Zee Trump oga sana,si alisema atapeleka silaha nzito Ukraine.
 
Hata mimi mkuu, lakini kwa bahati mbaya kumbuka Uingereza,Ufaransa na Ujerumani ndio washauri wakuu wa Zelensky na hawataki mgogoro huu huishe/sitishishwe watamshauri Zelensky akatae ushauri wa Trump, wao watamsadia kuishinda kivita Urusi, ndio walivyo, nafikiri hata Trump amekwisha washtukia.
Hivi kwa akili zako hao EU wanaweza msaidia Ukraine aishinde urusi!?...huyo mume wao trump anataka mazungumzo
 
Hivi kwa akili zako hao EU wanaweza msaidia Ukraine aishinde urusi!?...huyo mume wao trump anataka mazungumzo
Mkuu, soma na ku-digest nilicho kiandika hapa nilikuwa na maanisha nini siyo unakurupuka tu na kuanza kuhoji akili za watu, kwanza hilo linaonyesha kwamba wewe si mstaarabu na uheshimu binadamu wenzako!! Wapi nisema Ukraine inaweza kuishinda URUSI kivita, wapi??

Nimesema washauri wakuu wa Zelezensky wanaotoka EU na Uingereza hao ndiyo wanaweza kumposha kwamba hasikubali kusitisha vita, watamsaidia kushinda vita dhidi ya Putin.

Ninayo yasema hapa siyo kwamba nayabuni tu, miaka ya nyuma huyu huyu Zelezensky aliwahi
kuzungwa na Waziri Mkuu wa Uingereza kwamba akatae/puuzia mazungumzo ya kuleta amani baina ya Urusi na Ukraine wakasema EU na Uingereza watamsaidia kushinda vita dhidi ys Urusi na Zelensky kwa ujinga wake kakubali akaondoka kwenye meza ya mazungumzo!!

Sasa nini kinaendelea hivi sasa, Ukraine inapigwa vibaya sana na Urusi wamepoteza wanajeshi wengi wa Ukraine na wakukodi, hawa ambao walijifanya wange msaidia Zelensky kijeshi wanampatia silaha tu lakini sio wanajeshi na majimbo mengi ya Ukraine kusini yamekwisha twaliwa na Urusi.
 
Back
Top Bottom